Rais amchagua Abdala Mtonga kuwa Internal Auditor General

Hebu mpongezeni aliyeteuliwa na tumwombee kila la kheri atende kazi aliyopewa. tuache mambo ya udini hapa. nadhani wenye kujadili dini mahala pa kazi ni wazembe na wenye upeo mdogo wa kifikra. Ni hao wanaodhani kuwa macho yao yanapoishia kuona ndiyo mwisho wa dunia.
Tufikirie mambo yenye kutujenga, hebu tuainishe sehemu ambazo zina shida ambayo inatakiwa IAG aanzie.
Kwa mfano aanzie kwenye PAYE ya TRA zimeliwa na akina na nani na wamechukuliwa hatua gani,
mwingine ongeza sehemu nyingine zenye shida....
Tuwe positive thinkers badala tu ya kuwa great thinkers (you can be a great thinker but retrogressively always and you add nothing to the community)
 
we ritizi una matatizo yako,ni wapi na ni mchangia yupi kasema waislam hawakusoma?na nani kaweka neno kunywa/kahawa?? Kweli? Au ndugu unataka kutueleza reality? Aya endelezen chuki na ligi zenu!

Gsana, kuwa mkweli hivi unataka kutetea hilo? au kwa makusudi tu unajifanya ujui kuhusu matusi yanayotukwana Waislam humu JF?
 
Nimeisoma hii thread kwa makini sana nilichokiona ni chuki walionayo Wakristo dhidi ya Waislam sijui kwa nini, mnasema Waislam awajasoma kazi yao kuuza kahawa, akitokea mwenye elimu akachaguliwa mnasema kachaguliwa kwa Uislam wake.
Kweli sasa naweza kuamini ni vigumu kutofautisha Chadema na Kanisa

Inasikitisha sana kuona watu wanaingiza udini, itikadi za vyama, kabila etc! Mtoa mada hii hakugusia any of those in any way, cha ajabu watu wamezuka tu mara dini, kabila, chama.....aibu! Humu ndani kuna wachangiaji wanaonekana waliwapa shida sana walimu wao darasani kuelewa. Kuna watu wanaonekana wana mawazo mgando na hiyo ni inferiority complex!

Kama mtu kachaguliwa/kateuliwa kuna mawili; kwanza kwa merits zake, kwamba anaqualify na pili, ni kwa matumizi mabaya kwa wenye decision making kuteua watu kwa interest zao ( na hili ndilo linalotuharibia maana hakuna delivery). Nadhani tungejadili uwezo wake zaidi kuliko dini, kabila, itikadi au pumba nyinginezo maana haijalishi ni wa katokea wapi kama huna qualifications - OUT! Msitake watu wapewe tu eti kwa kuwa ni Mkristo au Muislamu ionekane hakuna ubaguzi, hatutafika.

Kwangu mie hainipi tabu awe wa dini, kabila, itikadi yoyote ili mradi ana uwezo apewe. Kikubwa tumpe ushirikiano na muda afanye kazi ndipo tuanze kubwabwaja!
 
Kuna baadhi ya "wasomi" waliochangia mjadala huu ambao hawajaelimika bado. Tukianza kunyoosheana vidole kwa misingi ya dini na vigezo vingine visivyokuwa na uhusiano katika utendaji hatutofika mahala. Zaidi, tutazidi kuonyesha udhaifu wetu. Watanzania ni vyema tukajihadhari na dhambi ya ubaguzi maana kama Mwalimu alivyosema, haina mwisho.
 

Nadhani tunapoteza muelekeo wa mjadala huu kama tunajikita katika kuijadili dini yake pekee.
Pili nadhani tutapoteza muelekeo zaidi kama tutaridhishwa na kiwango cha Elimu kilichoainishwa katika taarifa hii.

Nadhani cha msingi kabisa ambacho inabidi tuangalie ni utendaji wake katika maeneo mbalimbali aliyopita. Tuangalie uwezo wake wa kimenejimenti katika nafasi hiyo aliyoteuliwa na pia tutazame rekodi zinamwonyesha ni mtu wa namna gani katika ujenzi wa ofisi mpya ambayo inatakiwa kuwa huru na yenye kuisaidia na kuikosoa Serikali ili kuboresha utendaji wake.

Nidhani tutazame mapungufu yake na utendaji wake katika kipindi chote cha miaka 32 aliyokuwa akifanya kazi Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Je, ni kweli anakitu cha kujivunia? Wakati uteuzi huo unafanyika, hayo ni mambo yaliyofikiriwa? Isije ikawa ni miaka 32 yenye uzoefu butu kabisa na ni heri yule aliyefanya kazi kwa miaka 5 tu.
Je, yupo conversant kiasi gani na mifumo yetu ya IFRS na IPSAS ambayo inabidi itumike katika kaguzi zetu za umma kwa sasa?

Je, anajua nini wajibu wa Ofisi yake hiyo mpya? Je, ana malengo gani? Ili kuweza kufanya hayo yatimie? Je anajua ni wakaguzi wa ndani wa aina gani anaowahitaji? Je anajua ni aina gani za kaguzi zifanyike ili kuboresha usimamizi wa rasilimali za nchi yetu?

Nadhani, udhaifu mkubwa wa teuzi zetu ni ya kwamba haziwapi nafasi wateuliwa ku-lay down their vision on how they want to run the institutions ambazo wanateuliwa kuziongoza.

 
mwendelezo wa kuhakikisha waislamu wanapata madaraka ktk nchi tena nyazfa za juu!
 
ndugu naomba nikubaliane nawe japo tupishane kidogo. Profession ya uhasibu imegawanyika sana,kuna kazi ndogo ndogo kuanzia petty cash book management,journal entries n.k mpaka consolided financial statements. Ivi yote haviwezi kuangaliwa na mtu mmoja,hata ikiwa ivo ndo balaa maana uozo utafichuzwa na uyo uyo mmoja. Lakini kwa kuweka checks and balances inakuwa rahisi kumanage fedha. Ni kama kazi za kisheria,haiwezekani kuwe na jaji katika ngazi ya kata au mahakama ya wilaya,huko kuna mahakimu. Sasa na uhasibu uko ivo,ili kupunguza errors CAG anakuwa na wawakilishi kila ngazi ktk ofsi za serikali hasa level ya mkoa,hapa hawa ukagua hesabu za ndani kabisa,na huitwa Internal auditors, hawa wanasimamiwa na Chief Internal auditor,huyu ndo mkuu,ila hawa wote wanawajibika kwa Chief ambaye ni CAG,yan controller and Auditor General. Kwa ivo ivo kazi zaenda. Naomba kusema kuwa hamna kazi isiyogawanyika,huwa kuna Delegation of powers. Hata rais mwenyewe ana wawaziri,msikitini kuna sheikh,imam n.k kanisani kuna askofu mkuu,maaskofu na mapadre/wachungaji,n.k n.k . Nadhan nimejaribu kueleza kwa uwezo wangu. Mwisho tumwombee bwn Mtongo aweze kuwa na maamuzi. Auditing is all about drawing conclusion whether statements show a true and fair view. Ts making a decision. All the best bwn mtonga.


Mkuu hapo penye red naona unataka kuwa potosha great thinkers! Internal Audit sio sehemu ya CAG hata kidogo na wala Internal auditors hawaripoti kwa CAG kama unavyosema. Internal Audit ni sehemu ya taasisi husika ambayo ipo kama mojawapo ya Internal controls kwa maana hiyo nao pia ukaguliwa na CAG. Iwapo CAG ataridhika na kazi zao basi anaweza kuamini kazi zao na kupunguza "Sample" wakati wa ukaguzi wake. Internal Audit kwa practises wanatakiwa waripoti kwa Audit commitee!

Kwa leo ni hayo tu!
 
Back
Top Bottom