Dumelambegu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,052
- 257
Bila kubadili katiba, tutaendelea kushuhudia uteuzi madudu! Wenzetu wakenya post kama hizi lazima mtu aombe na afanyiwe usaili.
Kuna tetesi zimezagaa kwamba JK amemteua bwana Abdala Mtonga kuwa internal auditor general.
Kama ni kweli nadhani uteuzi wake utakuwa mzuri maana jamaa alikuwa afisa masuhuri wa ofisi ya CAG na pia alikua mkaguzi wa kanda hapo hapo. Ni mtu safi asiyetaka ujinga ujinga kwenye utendaji wa kazi. Tatizo lake ni muoga kufanya maamuzi. Labda anaweza kuleta utofauti kwenye hii ofisi mpya iliyounda
============
Si tetesi tena, ni habari kamili...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amemeteua Bw. Mohammed A. Mtonga (52) kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (Internal Auditor General).
Bw. Mtonga ni msomi mwenye Shahada ya Uzamili katika masuala ya Fedha (MSc in Corporate Finance) toka Chuo Kikuu cha Salford nchini uingereza.
Aidha Bw. Mtonga anayo Shahada ya Uhasibu ya CPA (T) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) na Stashada ya Juu ya Uhasibu (Advanced Diploma in Professional Accountancy) toka Chuo cha Jamii Nyegezi ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Mt. Augustine cha Mwanza.
Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mtonga amekuwa na utumishi wa miaka 32 katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Heasabu ambapo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali.
Nyadhifa alizowahi kushika Bw. Mtonga ni pamoja na Afisa Masuuli na Mkaguzi wa Hesabu wa Kanda. Pia amewahi kuwa Mkaguzi wa Hesabu Mkazi katika mkoa wa Lindi, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Makao Makuu ya Jeshi (Ngome).
Uteuzi huu umeanza toka tarehe 06 Aprili, 2011.
Mbona hawajasema alisoma lini, haswa hiyo Msc? Nafikiria uwezo wake wa kutafsiri hizo IFRS maana experience yake haionyeshi kama alikuwa ana-deal na IFRS - ama nakosea?
Mwislam Safi, ulamaa aneyejua kazi yake na misingi ya uislam, hongera JK kwa uteuzi huu.
Mwislam Safi, ulamaa aneyejua kazi yake na misingi ya uislam, hongera JK kwa uteuzi huu.
Mbona hamkuyasema hayo Mkapa alipokuwa Raisi, au kwa kuwa alikuwa Mkristo mwenzenu!? Mfumo Kristo Bwana! Mtu anakuwa na Chuki bila sababu kwa sababu rais Muislamu! Nchi hii yetu sote rais akiwa muislamu ataamua kadri ya uwezo wake na akiwa mkristo ataamua kwa kadri ya uwezo wake!:happy:
Mimi pia nahitaji hiyo sheria kwa kweli maana kama sielewi hivi, kwani Controller and Auditor General (CAG) pia anafanya audit kwa kuwa internal audit ni sehemu ya audit. Nahisi kama hatujuwi tunachofanya hapa sana sana tunazidi kumwongezea mzigo masikini mlipa kodi (nchi hii inaendeshwa kwa PAYE) pasipokuongeza efficiency yeyote kama tulivyofanya kwenye EWURA, SUMATRA na upuuzi mwingine unaofanana na huo.
Ni nani amesema kwamba tatizo letu ni kutokufanyika kwa audit? Hili si kweli kwani kila mwaka CAG anareport upotevu wa mabilioni na hakuna kinachofanyika, reports zake tunaishia kufungia vitumbua Kwamtogole.Tungekuwa serious kufanyia kazi reports na recommendations za CAG wala tusingehitaji ofisi mpya ya internal audit, huu ni upotevu wa pesa usio na sababu.
Nimeishoma hii thread kwa makini sana nilichokiona ni chuki walionayo Wakristo dhidi ya Waislam sijui kwa nini, mnasema Waislam awajasoma kazi yao kuuza kahawa, akitokea mwenye elimu akachaguliwa mnasema kachaguliwa kwa Uislam wake.
Kweli sasa naweza kuamini ni vigumu kutofautisha Chadema na Kanisa