Rais akifurahia jambo na mcheza kikapu wa marekani...Mh. Rais ila watzi hatuna umeme, mzee!!

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
[h=1]DWIGHT HOWARD AKUTANA NA RAIS KIKWETE IKULU[/h]
Mchezaji maarufu wa mpira wa Kikapu duniani, Dwight Howard akimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya jezi wakati nyota huyo alipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es Salaam jana. Dwight Howard ni mchezaji nyota wa timu ya kikapu ya Orlando Magic ya nchini Marekani.
Nyota mchezo wa kikapu nchini Marekani Dwight Howard akimwangalia Simba aliyekaushwa kitaalamu na kupamba lango la ikulu jijini Dar es Salaam huku akifurahia jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati nyota huyo alipokwenda ikulu kumsalimia Rais na kutoa ahadi ya kutoa msaada ili kukuza vipaji vya mchezo huo nchini.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia), Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na nyota wa mchezo wa kikapu nchini Marekani Dwight Howard (Katikati) wakati nyota huyo alipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es Salaam jana.Nyota huyo anachezea klabu ya Orlando Magic.

Picha zote na Freddy Maro/Ikulu
 
sio mbaya amefanya kuficha siri na umasikini wa nchi kwa tabasamu kaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Haya ndo mambo anayoyapenda yeye.Haya yenu ya mgao wa umeme , kupanda bei ya mafuta , na ugumu wa maisha mtajijua wenyewe.hapa ni gambe tu
 
na yeye pia ni msanii,tusishangae jamani... haya ndiyo mambo anayoyapenda....View attachment 35899 JK.jpg View attachment 35901
 
ndio rais wetu huyo,kila mtu na blog kibao wanaongea negative kwa jamaa,ni dhahiri hakubaliki!!!!!!2015 sijui itakuwaje,,naomba mjadili mambo kama haya kwa kina ili watanzania waelewe kinachoendelea katika nchi yao...mmmmccccchhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!
 
Haya ndo mambo anayoyapenda yeye.Haya yenu ya mgao wa umeme , kupanda bei ya mafuta , na ugumu wa maisha mtajijua wenyewe.hapa ni gambe tu
...Huyo Kwanza anatamani kesho ndio iwe 2015 asepe. Ameoona joto ya jiwe ya hicho kiti. Wakati Nyerere anawaambia kuwa ikulu ni pagumu walidhani anatania? Sasa hivi mi naona ameshakata tamaa ya maisha kwa hiyo ameacha bora liende tu!
 
watu wa protocol nao sifuri kabisa, kwa umbile la jamaa ilipaswa hiyo picha ipigwe wakiwa wamekaa kwenye viti. Mke wa sarkozy rais wa ufaransa aliacha kuvaa high hilly ili angalau kimo chake kiwe kifupi asionekane kumzidi mumewe. Na sehemu zingine sarkozy anapofanya ziara watu wanaoruhusiwa kuwa karibu yake ni wenye vimo vifupivifupi.
 
Msanii ni msanii, of all the problems unapata muda wa kuchat na basketballer?..
 
Back
Top Bottom