Rais Abdulaye Wade wa Senegal akubali kushindwa!

Inauma sana dr slaa alishinda urais(2010) lkn walimchakachua,dr wa ukweli usife moyo 2015 urais wako ebu mwangalie mnyika 2005 walimchakachua lkn hakukata tamaa 2010 nadhani unajua,,,,maisha ni magumu kupindukia eh mungu dr uingie madarakan 2015 cement na mabati viwe 5000 tumechoka kupanga na kulala kwenye nyumba za tembe,ona sasa nondo 12mm sh elfu 20 kweli imbombo ngafu hadi huyu jamaa akitoka madarakani cement itakua 25,000/=
hawa jamaa hawana uchungu na nchi hata kidogo
 
kaumbuka.

Hii ndiyo shida ya kuwaweka wazee madarakani; wengi wao huwa wanataka kufikia kwenye viti vya ikulu. Wengi wao huwa hawaridhiki kuongoza kipindi kimoja kama Kibaki ama vipindi viwili kama Wade.
 
he was opposition, akapewa nchi kwa matumain kibaooooooo, bidae akataka kumrishisha mwanae nchi, wasenegal wakashtuka akaona agombee mwenyewe ,wakaenda round ya pili na kushindwaaaaaaaaa
 
Vijana tuamue
Vijana wa nchi gani? Kama unazungumzia Tanzania sawa kwasababu nchi nyingine wameisha amka miaka mingi iliyopita. Hapa TANU,bdae mwanae CCM wapo madarakani miaka 50 sasa!!! Ni rekodi barani Afrika!!
Nimeangalia nchi zote jirani,nchi za maziwa makuu,kusini mwa Afrika na Pembe ya Afrika hakuna chama kimetawala miaka yote hii. Sijui majirani wetu wanatuonaje!!!
 
images
images


Shirika la habari la serikali nchini Senegal limetangaza kuwa rais Abdoulaye Wade amekubali kushindwa na mpinzani wake Macky Sall katika dura ya pili ya uchaguzi wa Urais. Bwana Wade alimpigia simu mpizani wake Macky Sall, na kumuambia kuwa amekubali kushindwa.

Na maelfu ya wafuasi wa Macky Sall wamejitokeza katika barabara za mji wa Dakar wakisherehekea ushindi wa kiongozi wao. Miongoni mwa waliokuwa wakisherehekea ni Bi Seynabou Seck " Niimefurahi sana , Macky bado ni kijana na tena ni mtu mpole sana na ana heshima! Kwa hakika anastahili ushindi huu . Kila mtu alikuwa akimuombea ashinde".

Mshindi huyo wa duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa urais ameutaja ushindi wake kama muamko mpya kwa raia wa Senegal. Macky Sall alikuwa akizungumza mara tu baada ya mpinzani wake Abdoulaye Wade mwenye umri wa 85 kukubali kuwa ameshindwa katika duru hiyo ya pili.

Wade alikuwa anataka kuchaguliwa tena kama rais wa Senegal kwa muhula mwengine wa tatu baada ya kubadilisha katiba ya nchi hiyo. Mabadiliko hayo yalizua machafuko na vurugu kubwa nchini Senegal.

Machafuko hayo hayakushtua ulimwengu kwani tofauti na jirani zake Senegali imekuwa tulivu na hajawahi kuwa na mapinduzi ya kijeshi kama jirani zake. Lakini upinzani ulipinga hatua ya kiongozi wao mkongwe na kwenda mahakamani. Hata hivyo mahakama iliidhinisha hatua ya Wade ya kubadili katiba ili aweze kusimama tena kama rais.

Na baada ya dura ya kwanza kukosa kuwa na mshindi wa moja kwa moja kwani hakuna aliyepata zaidi ya asilimia 50, ikiwa ni lazima kuwe na duru ya pili ambapo viongozi wote wa upinzani walimuunga mkoni Macky Sall. Na sasa Macky Sall ambaye zamani alikuwa Waziri mkuu katika serikali ya Abdoulaye wade ameibuka mshindi.
 
Wadau, je? Kushindwa kwa rais aliyetaka kung'ang'ania madaraka Abdoulaye Wade wa Senegal kunatoa picha gani kwa CCM?
 
kwa wanaotaka CCM ianguke ni funzo kwa wasiotaka ianguke hakuna funzo lolote kila nchi ina aina na jinsi yake ya kuendesha uchaguzi na haiba ya watu wake.

Bado kuna vyama kongwe vinaendelea kuwepo licha ya misukosuko kama vile ZANU - PF, ANC na FRELIMO
 
Funzo lipo na kubwa zaidi kwa wanasiasa za majitaka. Pia viongozi na wananchi lazima wajifunze kuumngana ili kuangusha tawala dhalimu! Funzo lipo hata kwa vyombo vya sheria vinavyowabeba wanasiasa uchwara maana kule mahakama ya kisenegali ilihidhinisha Wade agombee muhula wa 3. Wade kaangukia pua! Sana sana baada kumuangusha jamaa inabidi waangalie vizuri sheria alizokiuka na kuifikisha nchi hapo ilipo.
 
Moderator umezidi kunionea. Kila nikipost kitu unakiunganisha na mwingine kulikoni au ubunifu kwako msamiati mgeni? Huu nao ni wizi wa kazi za watu. Hii ni Jamii forums siyo jamii fulani ya kubebana na kuoneana. Kuna haja ya kuheshimu michango ya watu. Kuna kipindi hufikiria kujiengua ili nione mtapata faida gani kumkosa nguli kama mimi.
 
Hawa wazungu waanze study ya France connection in west Africa. All these guys, very old, are members of influencial elite groups operating in France...in UK they hide behind British Legions. I am sorry for Wade but he is a member tooo.
 
Back
Top Bottom