Mkuu wangu muuzaji mkubwa wa Tanzanite Toronto ni Mhindi Mtanzania ambaye ana duka pia mjini Arusha. Hivyo sielewi mapatano yake na serikali yetu isije kuwa serikali yetu imemtumia mtu huyu kuanzisha biashara hii huko Canada kwa faida ya taifa letu hii poa kabisa na mdio maana nikasisitiza sana serikali yetu iwatumie Diaspora..Ni athari za ukoloni mkuu, unajua India inasifika duniani kwa uuzaji wa vito vya Tanzanite na hawachimbi Tanzanite kule, sehemu nyingine utakuta matajiri wa Tanzanite dunia hii ni Toronto, inahuzunisha sana
Serikali ina uwezo kabisa wa ku-control haya madini, na hata kuwa wanunuzi wa haya madini na kutengeneza products.
Ten percent wapate wapi??
Nafikiri kuna haja ile sera ya majimbo ya CHADEMA kuwa applied , kama hawa jamaa watashika nchi.
Naamini mikoani kuna watu wenye akili zao ambao wanaweza ku-control madini kama wakipewa chance
Kinyume cha hapo na navyoifahamu Nchi yangu, kina Richmond ni wengi sana....