Raia wanaposhinikizwa kupisha maendeleo....

nadhani hakuna anaependa kufanyiwa dhulma ,ila tatizo misingi ya kujitetea au kutetea haki zako ,coz vyombo vya sheria vya kutetea sheria za wananchi vyote viko pamoja na serikali na rushwa mbele ,ndio maana watu wanakuwa hawajui nn wafanye ,,kama kuta kuwa na mfumo kama ule wa waengereza kueka citizen advice bureau,, sehemu ya kutetea wananchi na haki zao,maybe ita saidia ,ila isiwe chini ya serikali iwe taasisi binafsi ,ambayo itakuwa na wanasharia walio kuwa wanajali haki za binaadamu

wahida inabidi tuendelee kujifunza namna ya kuzitambua haki zetu na jinsi ya kuzidai na kuzitetea badala ya kuviamini vya siasa...
 
Last edited by a moderator:
Hoja zako zimeshikamana vizuri kweli kweli.
Kama viongozi wanaochaguliwa direct na wananchi ndio wangekuwa wanasimamia maamuzi ya namna hii sidhani kama haya yangekuwa yanatokea, viongozi wanaofanya maamuzi ya kizembe namna hii ni administrative ambao ni wateule wa ama viongozi tuliowachagua sisi wenyewe au wateule wa wateule wa wateule wa wateule wa viongozi tuowachagua wenyewe kwenye mabox ya kura.

napendekeza kwamba, kwenye mchakato wa uaandaji wa katiba mpya tuhakikishe kwamba ama viongozi wanaoteuliwa na viongozi waliochaguliwa kwa sanduku la kura wasiwe na mamlaka ya kuteua viongozi, na pia tuongeze idadi ya viongozi wa kuchaguliwa kwa sanduku la kura au tuamue maamzi fulani fulani yafanyike baada ya kupigiwa kura badala ya kupigia kura viongozi pekee.

Sangarara kwa kuanza serikali za mitaa ziongozwe na mameya wa kuchaguliwa.........ma madiwani wawe waajiriw awa tumishi waote wa halmashauri zao badala ya Ikulu kupitia waziri wa serikali za mitaa au Pm kuwanyang'anya majukumu yao ya kudhibiti matumizi na nidhamu ya sehemu walizochaguliwa
 
Last edited by a moderator:
Hii ni nchi ya ajabu sana ambayo kila kukicha inakuja na mikakati ya kufukarisha raia wake kwa visingizio vya wapishe maendeleo kama vile raia siyo sehemu ya hayo maendeleo............................. Matokeo yake raia husukumwa nje ya maendeleo kwa maana ya huduma muhimu na kupunjwa fidia ya thamani khalisi ya mtaji aliouwekeza kwenye shughuli zake kama vile nyumba, shamba na maendeleo mengineyo........................ La ajabu kabisa huyo mwekezaji anayepishwa huwa halazimishwi na sera/sheria kuwafidia waathirika wake kwa hasara ya kunyimwa kivuno cha matarajio yajayo ya waathirika......athariza kimazingira, uchumi, afya n.k hujitokeza....zikiwemo hasara ya kukosa huduma muhimu ambazo sasa yabidi wazifuate mbali na gharama nyinginezo ambazo sasa zinakuwa zimebinafsishwa kwa huyu mwekezaji....................na kuwa faida ambayo mwekezaji hata anakuwa hajaipanda..... kwa hiyo huvuna asichopanda wala kustahili.....na mwaathirika huwa amesahaulika kabisa!!!!!!!!!!!!!!!! Ushauri Tunahitaji sera ambazo zitamtambua raia mwathirika kama sehemu ya huo uwekezaji mpya ili aendelee kuvuna na kumpunguzia makali ya kupisha maendeleo......kumtambua apewe hisa naye awe sehemu ya umiliki wa huo uwekezaji na kwahiyo hajapisha maendeleo bali naye amekuwa sehemu ya maendeleo kama kweli yapo! Tusipofanya hivyo kwa kuwapa hisa watu wetu kwenye mitaji ya maendeleo tajwa...ina maana baada ya miaka kama 20 hivi ijayo sehemu kubwa ya raia wetu watakuwa wakimbizi wa kiuchumi ndani ya nchi yao................ Kwa minajili ipi tuaafiki na khali hiyo?

Hii ni Laana: Mkuu Ruta, kwanza asante kuandika hii posti. Mungu akuzidishie na akubariki. Umejitolea kuandika haya mambo kwa niaba ya wanyonge, na wote waliodhulumiwa au wanaodhulumiwa mali na haki zao. Kumbuka kua watu hawa walijitolea muhanga na kumwaga damu kwa kupigania nchi mwaka 1978 na pia katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa. Leo, wanafikwa na msiba huu. Kweli hujafa hujaumbika. Nani aliejua jua wakati wa Draft (Lazima kuingia Jeshi kwenda mtukula), iko siku nchi hii itawahamisha kwa dhulma? Vipi kama walipoteza watoto zao katika kupigania nchi? Huu mtindo wa kuhamisha watu kihivi ni Laana. Huu ni wakati wa kuwa Patriotic. Na walio hamishwa na wanaohamishwa wote wapewe haki zao. Huu sio ubinaadam.

Mkuu, wazo la kua na sera za kumtambua raia muathirika ni muafaka sana. Ingekua vema zikatia maanani kua kuna dhulma za aina mbili inapokuja kwenye matumizi ya mali asili. 1. Kuitumia hovyo bila kujali watoto (Taifa la kesho) kwa mfano, mazingira, uchumi wa baadae ambao unatumika sasa hivi, etc . 2. Na Pili ni dhulma ya kutowapa malipo sawa wenye mali yao (wanainchi). kwa mfano mali asili zinauzwa bila utaratibu maalum ambao mfanyakazi wa serikali anaelewana na Muwakilishi wa kampuni wanakutana na kuelewana bei. Hii husababisha hata wawakilishi wa serikali kupunjwa saana tu. (kwa sababu hawajui mali inathamani gani).
 
Back
Top Bottom