Raia wa kigeni mbaroni wakiuza watu Dar

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


na Happiness Katabazi


RAIA wa Nepal, Ashok Kumar Khadka, na wenzake, anayetuhumiwa kufanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana, Mwanasheria wa Idara ya Uhamiaji, Patrick Ngoyomela, alidai kuwa mbali na mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani, washtakiwa wengine ambao ni raia wa India na Nepal ni Hasnein Kamrudin Osman, Kamal Gautama, Adhikar Did Natu, Rama Prakash Paudel, Atmaram Ghimire, Sibnath Bag, Mohamed Ridzwan Khan.

Wakiwa mahakamani hapo, wakili wa Idara ya Uhamiaji Ngoyomela alishindwa kuwasomea mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao kwa sababu walikuwa hawafahamu lugha ya Kiingereza, hivyo endapo angewasomea mashtaka hayo wasingeelewa.


Ngoyomela alimuomba hakimu huyo aahirishe kesi hiyo hadi hapo atakapopatikana mkalimani wa kutafsiri lugha ya watuhumiwa hao.


Ombi hilo lilikubaliwa na hakimu huyo ambaye aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 27, aliamuru washtakiwa hao wapelekwe gerezani.



 
Wahindi wanachukua Madini Yetu, Biashara Zetu na sasa Wanasafirisha able bodied people...
 
Hebu tujuze vema sasa hao viumbe wakisafirishwa kwa madhuni yepi hasa?
 
Back
Top Bottom