RAIA MWEMA: Vigogo wajipa ardhi kwa fujo nchi nzima

inabidi chadema waitishe maandamo kuitaka serikali itoye list hiyo hadharani na picha wamiliki, maana hawakawi kubadilishsa majina kama john samwel sita, ikawa samwel john au john samwel, sitta linaachwa, au mtu anaweka jina lamke kuepusha zogo.
 
Ethics za wanahabari zetu ziko wapi? Ukisoma unaona hii makala ni ya kichochezi.

Mwandishi anadrop names za Jakaya. Ridhiwani, Marmo bila kuweka vielelezo, sources, hata quotes za watendaji ili kutupa evidence sisi wasomaji. In this way, anybody with a big chunk of land, can be me or you we will stand to be accused.

Kitu kibaya zaidi, mwandishi was betting on ignorance of waTanzania wa kutoweza kuona mapungufu ya hii makala. And sadly great thinkers wa Jambo Forum fell into Mwandishi's trap. Hii makala is a prime example ya kutumia media kueneza chuki dhidi ya watu wengine. What else can you call this piece?
Since you seem to know what happened can you tell us what the newswriter left out? Because your retort still leaves us in the dark.
 
Ethics za wanahabari zetu ziko wapi? Ukisoma unaona hii makala ni ya kichochezi.

Mwandishi anadrop names za Jakaya. Ridhiwani, Marmo bila kuweka vielelezo, sources, hata quotes za watendaji ili kutupa evidence sisi wasomaji. In this way, anybody with a big chunk of land, can be me or you we will stand to be accused.

Kitu kibaya zaidi, mwandishi was betting on ignorance of waTanzania wa kutoweza kuona mapungufu ya hii makala. And sadly great thinkers wa Jambo Forum fell into Mwandishi's trap. Hii makala is a prime example ya kutumia media kueneza chuki dhidi ya watu wengine. What else can you call this piece?

selemani, nakuunga mkono 100%. Hapa kuna uchochezi zaidi kuliko kupashana habari. Tukio hili lilishalipotiwa hapa jf mda mrefu. Nashauri mwenye taarifa kamili afafanue kuliko kututajia majina tu ya vigogo.
 
Vigogo wajipa ardhi kwa fujo nchi nzima

* Yumo Ridhwan Kikwete, Marmo, Gavana Ndulu, Dk Kimei
* Maelfu waachwa 'kwenye mataa'
* Orodha yabanduliwa ghafla

Kashfa ya sanya sanya ya viwanja katika maeneo muhimu muhimu nchini imezidi kushamiri ikiwahusisha waliokuwa mawaziri pamoja na familia zao, akiwemo pia motto wa Rais Kikwete, Ridhwan Kikwete, Raia Mwema limebaini.

Uchunguzi wa Raia Mwema katika baadhi ya maeneo nchini, ikiwemo mikoa ya ya kanda ya Kaskazini, Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani, unaonyesha kwamba vigogo hao wamekuwa wakijitwalia maeneo kwa kasi ya ajabu; huku wenyeji wa maeneo hayo wakinyimwa.

Kwa mujibu wa habari hizo, baadhi ya maeneo vigogo hao wamekuwa wakinunuwa kwa fedha taslimu na baadhi ya maeneo wamekuwa wakijitokeza na kugawiwa na watendaji wa halmashauri na manispaa za maeneo husika, huku maelfu ya wananchi wa maeneo husika wakinyimwa pamoja na kuwa wa mwanzo kuomba na kulipia gharama za fomu ambazo hutumika kupimia viwanja.

Mfano wa hivi karibuni ni mkoani Arusha ambako siku chache baada ya uchaguzi mkuuu, vigogo kadhaa waligawiwa viwanja katika mazingira tata huku maelfu ya wananchi wa mkoa huo walioomba akijikuta wakiwa hawamo katika orodha ya watu waliopata viwanja iliyobandikwa kwenye ubao wa matangazo na kubanduliwa baada ya wananchi kuanza kulalamika.

Sakata hilo la aina yake limetokea katika halmashauri ya Arusha Vijijini mkoani Arusha, ambako Idara ya Ardhi ya Halmashauri hiyo ilikusanya mamilioni ya fedha kutoka kwa wananchi, wakiwemo ‘makabwela’, kwa ajili ya kupimiwa viwanja katika eneo la Burka ambavyo hata hivyo vimegawiwa kwa vigogo.

Mbali na Ridhwan, vigogo wengine waliogawiwa viwanja vya Burka huko Arusha Vijijini ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Philip Marmo, na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Aggrey Mwanri…………………………..

Habari zaidi katika RAIA MWEMA ya leo.

Hivi Ridhiwani ni mtoto wa kigogo au naye ni kigogo?
 
Changamoto kwa Mh. Godbless Lema kuhakikisha kila mwenye haki kupewa haki yake. Halmashauri tunayo ngoma italia tu.

Mhusika ni Mh. Ole Medee nayo yuko busy na vyeo mfano Bunge la SADC sidhani kama atakuwa na muda wa kuangalia matatizo ya wananchi ndani ya Jimbo lake
 
Baada ya Uchaguzi, Vigogo wajipa ardhi kwa fujo nchi nzima

Yumo Ridhiwan Kikwete, Marmo, Mwanri, Kabwe wa Mwanza !
Maelfu ya waliolipia waachwa 'kwenye mataa'



..........................................................................[snip]

Akizungumzia malalamiko hayo na mengine, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, alisema taarifa alizonazo ni kwamba viwanja vya Arusha viligawanywa kwa kufuata taratibu, lakini alikataa kuzungumzia kuhusishwa kwa vigogo.​

Huyu mtu mbona kila wizara anayokwenda ni matatizo makubwa? Au anapelekwa makusudi ili afanikishe ufisadi.
 
Naamini mmeshaona hiyo ni safari ya kuelekea ubepari... mara ya kwanza tuliona uchumi umepanda kwa 6% lakini maskini amekua maskini kwa zaidi ya 10% msimu uliopita, msimu huu tuaona tumekuwa 15% umaskini wa mtanzania wa kawaida 50%.... hili lilitokea Kenya pia, sera zetu mbovu na wasimamizi ndo kabisa!
 
[/LEFT]

Huyu mtu mbona kila wizara anayokwenda ni matatizo makubwa? Au anapelekwa makusudi ili afanikishe ufisadi.

Nasikia anajivunia ujasiri wa kukataa mkataba wa IPTL, akajifanya msafi kuliko sufi, lakini sasa nasikia ni bingwa wa kuchukua mzigo kwa wateja ndiyo maana miradi mingi ya viwanja inakwama huku mabilioni ya wavuja jasho yakiendelea kuteketezwa kwa surveys.
 
FOMU ILIKUA SH 10000 WATU WALIOCHUKUA FOMU 12700 VIWANJA 700 KILA SQUARE METER SH 8500.WALIOPATA MAWAZIRI MAKATIBU WATOTO WA VIGOGO MADIWANI WA CCM.HATA WAKATI WA KUJAZA FOMU SIFA MOJAWAPO UWE MKEREKETWA WA CCM!wana jf tuchukue hatua gani?MIMI NA WEWE 20 x40 sq meter sh 9M tutaweza huku yule mgiriki kafidiwa kwa kodi zetu???
Duh, ama kweli huo ni wizi kabisa. Yaani Arusha vijijini kiwanja sq 1 ni Tsh.8500?? hawakutaka wananchi wa kawaida wamiliki hiyo ardi kwa kweli.

Nikifanya comparison, kigamboni kuna viwanja vimeuzwa kwa Tsh.3500-4000 kwa sq.metre. je, ardhi ya huko ni ghali kuliko hiyo ya DSM???

Haya ndio sawa na yale yale ya minara ya BOT kwamba ardi ya dar es salaam ina trhamani kubwa kuliko ya Tokyo na New York.


Huu ni wizi kwa kweli.Halmashauri ya Arusha imewaibia wananchi.
 
Manispaa ya Arusha imeniibia hata mimi buku kumi yangu na kiwanja sikupata tupinge wizi huu wa sisi makabwela:A S angry:
 
Back
Top Bottom