Nani atamkamata wakati bosi wawakamataji ni mteule wa mwenyekiti wa NEC na mwenye bastola ni mjumbe! They are above the law japo haijatamkwa rasmi tu. Vijana hawa pia wamejaaliwa matusi ukiingia anga zao na ukawa si mwanamagamba au uwe mwnamagamba lakini CV yako ndogo utajuta! Who ever goes up must come down, it is just a matter of time!
Benno Malisa
Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM
BASTOLA ya kigogo wa makao makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mjini Dar es Salaam, imemjeruhi tumboni mwanafunzi wa Chuo cha Biashara Dodoma (CBE), Raia Mwema limeelezwa. Habari za uhakika zinaeleza kwamba mtu mmoja anayetajwa kuwa dereva wa kigogo huyo, alikwaruzana na mwanafunzi huyo Emmanuel James (30) eneo la Sinza, Mugabe, Dar es Salaam karibu na Hoteli ya City Style.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, wakati wa tukio hilo kigogo huyo hakuwapo kwenye gari ambalo aliacha bastola yake na dereva aliitumia kuwafyatulia risasi vijana waliomhoji sababu ya kuwamwagia maji machafu. Baada ya vijana hao kupiga kelele za kwa nini wamemwagiwa maji machafu, dereva huyo alipaki gari na kuanza kuwafokea vijana hao na walipojibizana naye alifyatua risasi mbili hewani na baadaye moja kumlenga tumboni Emmanuel James, kinaeleza chanzo cha habari.
Tukio hilo ambalo limetokea saa saba usiku wa Novemba 30, 2011, limeibua maswali mengi baada ya kuwapo taarifa za kutokamatwa kwa wahusika wala silaha iliyotumika katika tukio hilo.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa (kipolisi) Kinondoni, Camilius Wambura, hakuwa katika nafasi ya kuzungumzia tukio hilo kutokana na kuwa katika majukumu mengine ya Kitaifa. Juhudi za kumpata Emmanuel kujua hali yake na kuelezea kuhusiana na tukio hilo hazikuweza kufanikiwa wikii hii, huku wahusika wakielezwa kutamba kutochukuliwa hatua zozote.
Taarifa ya tukio hilo zimeripotiwa katika kituo cha polisi cha Urafiki Dar es Salaam, ambako imeelezwa kwamba hadi sasa wamekuwa wazito hata kuwahoji wahusika na kufanya uchunguzi zaidi kuhusu silaha iliyotumika.
Ingawa vijana wale walifanya kosa la lugha chafu iliyomkasirisha yule driver, lakini tukio la kutumia silaha kali kumjeruhi mtu haliwezi kuachwa hivi hivi, kosa ni kosa halijalishi nani kalitena.Nani atamkamata wakati bosi wawakamataji ni mteule wa mwenyekiti wa NEC na mwenye bastola ni mjumbe! They are above the law japo haijatamkwa rasmi tu. Vijana hawa pia wamejaaliwa matusi ukiingia anga zao na ukawa si mwanamagamba au uwe mwnamagamba lakini CV yako ndogo utajuta! Who ever goes up must come down, it is just a matter of time!
Ingawa vijana wale walifanya kosa la lugha chafu iliyomkasirisha yule driver, lakini tukio la kutumia silaha kali kumjeruhi mtu haliwezi kuachwa hivi hivi, kosa ni kosa halijalishi nani kalitena.
Hivi maelezo yako yanajustify dereva kutumia bastola na kujeruhi watu? Halafu unahoji eti dereva ana kosa gani? Wewe kumbe bure kabisa! Wanaokutegemea unawashauri nini?Mijitu mingine hovyo!!.
Kama kesi ipo mahakamani tusijadili mwenendo wa kesi, lakini tunaweza kujadili suala la bastola ya kigogo ilivyotumika kutoboa tumbo la mwanafunzi.