Rai: Zitto ameleta songombingo; wabunge CCM sasa wana posho na kujivua gamba kuvutia wananchi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Wabunge CCM, posho na kujivua gamba
Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ameleta songombingo kipindi hiki cha Bunge la Bajeti. Hili naweza kuliita ni sakata la aina yake hasa katika kipindi hiki ambapo kuna mwamko mkubwa katika siasa za vyama vingi hapa nchini Tanzania.

Suala la posho pamoja na malipo mbalimbali yanayoonekana kuwa ni makubwa wanayopewa wabunge lilipata kumletea shida na dharau kubwa aliyekuwa Mbunge wa Karatu na sasa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa katika Bunge la 2005-2010 pale alipoonekana kupingana na malipo hayo.

Ni katika kipindi hiki ambapo Chadema kama chama kikuu cha upinzani na chama kinachounda kambi rasmi ya upinzani Bungeni, kinapoonekan kupinga sana matumizi makubwa ya Serikali, huku hali za wananchi pamoja na huduma mbalmbali za kijamii zikiwa mbaya na kutopewa nafasi ya kutosha katika bajet ya mwaka.

Kwa mujibu wa bajeti ya Serikali iliyosomwa wiki iliyopita, posho iliyotengwa inakadiriwa kufika Sh bilioni 987. Mbali na hapo na wabunge katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti watakuwa wakijinyakulia posho ya S150,000 kila siku nje ya mishahara yao kwa kipindi kisichopungua cha miezi mitatu, yaani Juni, Julai na Agosti. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, Bunge linamaliza mkutano wa bajeti Agosti 31 mwaka huu.

Nimeliita sakata hili la aina yake, kwani ni jaribio kubwa kwa wabunge wa CCM na chama tawala hasa kipindi hiki ambacho mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete ameasisi dhana ya kile kilichoitwa "kujivua gamba".

Mojawapo ya sababu za kujivvua gamba zilizolezewa ni chama kupoteza mvuto mbele ya Watanzania hivyo kupoteza kura nyingi na viti vya wabunge katika uchaguzi wa mwaka mwaka 2010.

Napata shida sana ya kuielewa dhana ya kujivua gamba na mustakabali wa ufufuo huo wa CCM iliyopoteza mvuto mbele ya umma na Watanzania na yale ambayo yanendelea kufanyika ndani ya CCM na Serikali yao.

Hii ni karata muhimu ambayo Chadema wanatumia katika kipindi hiki na ni kipimo hasa cha kujua utashi wa waheshimiwa wetu pale mjengoni Dododma!
Sitakosea iwapo nitayalinganisha malipo ya posho wanayopewa Wabunge kwa kuhudhuria vikao ambavyo wanapaswa kuwepo na ufisadi mwingine unaoendelea katika taasisi mbalimbali za umma.

Waakati wanapochaguliwa, wabunge wanajivika joho la watu wenye hekima kila mahali wao tu ndiyo wanaoshauri na kutoa maelekezo, hii imekuwa ni tabia maarufu sana kwa wanasiasa wetu lakini linapokuja suala la maslahi yao, hekima zao zinatoweka.

Ni lazima sisi kama wanadamu tuweze kujitofautisha na wanyama kwa sababu tuna utashi na uwezo wa kufikiri. Haiwezi kuingia akilini kweli, leo tuna wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaodai fedha zao miaka nenda rudi, na walimu wetu, wauguzi na madaktari wanaojitolea kufanya kazi katika mazingira magumu lakini hawalipwi posho.

Kwa CCM inayodai kwamba inataka kujivua gamba, huu ni wakati wa kutafakari upya dhana hii ya kulipana posho. Kamwe CCM haiwezi kuvutia wananchi kwa kutaka watu watatu waondolewe chamani! Hakika matatizo ya CCM kamwe hayawezi kuwa watu hao watatu.

Nasema hivi kwani yanayoendelea bungeni katika sakata hili la posho yanaonekana na kusikiwa na Watanzania wengi. Hakuna Mtanzania aliye sawa atakayeweza kuvutiwa na tamaa zinazoonyeshwa na wabunge wa CCM wanaong'ang'ania posho hiyo.

 
kwa sasa magamba yameshindwa kuvulika, duh! kweli chama cha magamba kina kazi sana!
 
Back
Top Bottom