Raha ya nyumba ndogo

Ambassador

JF-Expert Member
Jun 2, 2008
933
75
Nimesikia mara kadhaa baadhi ya wanaume wakisema nyumba ndogo zinawaliwaza na kuwaondolea stress wanazozipata kwa wake zao. Mie nikitafakari nahisi kama nyumba ndogo zinaongeza stress maana utatakiwa kuingia gharama za kuihudumia, kubana muda wako ili kuwa nae na kujifunga mabomu pindi waifu atakapong'amua. Naomba wenye nyumba ndogo au uzoefu wa kuwa na nyumba ndogo watupe uzoefu wao. Waliowahi kupata bahati ya kuwa nyumba ndogo za watu nao tunaomba their side of the story. Bila kusahau waliowahi kupata adha toka kwa nyumba ndogo zao au rather nyumba ndogo za waume wao. Na wote mnaoguswa na hili, karibuni tuchangie.
 
Utakuwa na raha kuwa na nyumba ndogo tu kama utaitambulisha kwa nyumba kubwa.
 
ni mateso matupu ukiwa na stress nenda bar kakamue bia na maongezi na watu hasa kaa counter, nyumba ndogo ni kuongeza stress, kwa mwanzo utaona kama inasaidia, itakapo kugeukia utajuta kwa maamuzi uliyofanya hapo mwanzo.
 
nyumba ndogo chanzo cha matatizo uwezi kutatua tatizo kwa tatizo starehe unayo ona unapata ni ya mda tu nikama umepigwa sindano ya gazi baada ya mda inaisha stress zinabaki palele
 
Kuwa na nyumba ndogo ni kuongeza matatizo juu ya maproblems... one woman is too stressful, two women is double stressful, brokeness... three women is asking for a heart attack and a debt... four women ... mama weeeeee naomba nirudi kijijini
 
Jamani si muoe tu hata wake watano na wajuane,mbona Zuma kaonyesha njia kuwa hilo linawezekana yeye ana umri wa miaka 65 lakini wake zake hao wawili wa mwisho bado ni mahindi mabichiii mzee wa watu anajilia kwa ulaini .
 
Mkuu achana na biashara ya nyumba ndogo. Kama mkeo ameku-stress bora upambane nae mpaka dakika ya mwisho. Nyumba ndogo kwa risk ya kupata ukimwi ni kubwa, kwani kama atajua hujamuoa wewe unakwenda pale kujipoza tu lazima atakuwa nae na mtu pembeni anakusaidia. Kwa vyovyote utajidanganya kuwa uko peke yako na hutumii condom. Pia nyumba ndogo ni costing kuliko hata mkeo wa ndoa, small house msamiati kuwa leo sina pesa haupo provided umejirengesha ni zigo lako na mwisho wa siku ni wastage of time, resources and energy mwishowe ndio hiyo "NGOMA"
 
The same stress which you escape from your wife you will face the same with nyumba ndogo because both are women.

Better you underlying factors that in first place precipitated the crisis/stress
 
Nyumba ndogo ni noma kwa sababu unajenga kibanda, kuchomoa kazi.Ila kupiga nje si mbaya sana, kwani akikuboa unatimua fasta bila lawama yoyote kwa mwanadamu na Mungu anakusamehe.
 
Kwa kweli ni kero,niliwahi kuwa nyumba ndogo ya mtu bila kujijua kwa kiwango kikubwa aliniharibia future yangu tulipoachana watu hasa vijana (waoaji)walianza kuniogopa it was very bad.
 
Kwa kweli ni kero,niliwahi kuwa nyumba ndogo ya mtu bila kujijua kwa kiwango kikubwa aliniharibia future yangu tulipoachana watu hasa vijana (waoaji)walianza kuniogopa it was very bad.

kuna binti mmoja tulikuwa nae ofcn, nae alidanganyika na mume wa mtu kwamba atamwacha mkewe amuoe, yaani unashangaa huyu mtu ana akili za wapi, hakunaga mwanaume anaeacha mkewe na kuoa kimada, huko wanaendaga tu kwa tamaa zao lakini nyumbani wanarudi na adabu zao tele,kwanza mapenzi yenyewe mnayopewa huko ya chap chap mbaba arudi kwa mkewe....hebu fungukeni bwana hawa waume wanawachezea tu.
 
Kwa kweli ni kero,niliwahi kuwa nyumba ndogo ya mtu bila kujijua kwa kiwango kikubwa aliniharibia future yangu tulipoachana watu hasa vijana (waoaji)walianza kuniogopa it was very bad.

Hii yako ilikuwa imekaa vibaya zaidi. Ni bora angekwambia mapema kwamba wewe ni nyumba ndogo. Alikuwa Msabato? Maana Wasabato huwa hawavai pete za ndoa!
 
kuna binti mmoja tulikuwa nae ofcn, nae alidanganyika na mume wa mtu kwamba atamwacha mkewe amuoe, yaani unashangaa huyu mtu ana akili za wapi, hakunaga mwanaume anaeacha mkewe na kuoa kimada, huko wanaendaga tu kwa tamaa zao lakini nyumbani wanarudi na adabu zao tele,kwanza mapenzi yenyewe mnayopewa huko ya chap chap mbaba arudi kwa mkewe....hebu fungukeni bwana hawa waume wanawachezea tu.

Kuna dada mmoja namfahamu, mzuri na ana kipato chake. Amekuwa nyumba ndogo ya rafiki yangu kwa miaka kadhaa sasa! Halafu kila akipata mtu wa kumuoa, mwanaume anamkataza! Anamwahidi kwamba ipo siku atamwacha mkewe ili amwoe yeye! Yule dada huwa namhurumia sana!
 
Hii yako ilikuwa imekaa vibaya zaidi. Ni bora angekwambia mapema kwamba wewe ni nyumba ndogo. Alikuwa Msabato? Maana Wasabato huwa hawavai pete za ndoa!

laaziz! mbona nina frnd msabato na anavaa? ....
 
Back
Top Bottom