Raha ya kupanda Dala Dala(Tupe kituko ulichowahi kuona au kusikia kwenye dala dala

big-diamond

JF-Expert Member
May 23, 2009
421
551
Nimegundua kwamba watu wanapokwenda kazini asubui huwa wana hasira ya kazi na wanaporudi majumbani huwa wana stress za kazi na kuanza kukumbuka uvundo uliotokea siku nzima!sasa usiombe ukapanda gari ambalo kuna konda mkorofi,!!

Mmama: Konda ondoa gari kuna joto,
Konda: Usituzingue wewe, kama vipi shuka upande fridge!:A S 465:
 
Konda: kamanyola
mama: shusha
konda: akushushe nani?! kwani nilikupandisha mimi? si ulipanda mwenyewe, njoo mlangoni ushuke mwenyewe.
 
Abiria: Kuna kiti au unasema panda tu?
Konda: Hao wengine wamekalia ndoo?

Abiria: Ebu tupunguzieni sauti ya redio
Konda: Sheria za nchi tu zinatushinda, tusikilize na zako, hebu tupunguzie misheria

Mama: Bwana ondoa gari joto sana
Konda: Usituzingue wewe shuka upande friji
 
Konda: Anti, kuna siti pale nyuma, ingia
Anti: Siwezi kukaa siti za nyuma
Konda: Kwenda zako wewe, kwani za nyuma ziko nje ya gari?
 
Ukipanda daladala hasa Coaster na ukose siti, uwe umesimama peke yako......
 
Walevi usiku wanazingua sana kwenye daladala...

Labda wenye experience za kupanda daladala usiku,watujuze... Kuna vituko vingi kwenye daladala...
 
Nimegundua kwamba watu wanapokwenda kazini asubui huwa wana hasira ya kazi na wanaporudi majumbani huwa wana stress za kazi na kuanza kukumbuka uvundo uliotokea siku nzima!sasa usiombe ukapanda gari ambalo kuna konda mkorofi,!!

Mmama: Konda ondoa gari kuna joto,
Konda: Usituzingue wewe, kama vipi shuka upande fridge!:A S 465:

Mi wananikera abiria wenye simu za kichina kwenye daladala na mara nyingi wanaweka sauti hadi mwisho,kero tupu,gari zima kelele!
 
Walevi usiku wanazingua sana kwenye daladala...

Labda wenye experience za kupanda daladala usiku,watujuze... Kuna vituko vingi kwenye daladala...
hivi ni visa vinvyosababisha huduma ya daladala za arusha kuishia saa 2 au 3 usiku
konda:mzee fungua nauli
mlevi:maayu(sitaki)
konda:mzee mlipie mke wako basi
mlevi:chukua hiyo mama watoto,nimeichoka!!
 
hivi ni visa vinvyosababisha huduma ya daladala za arusha kuishia saa 2 au 3 usiku
konda:mzee fungua nauli
mlevi:maayu(sitaki)
konda:mzee mlipie mke wako basi
mlevi:chukua hiyo mama watoto,nimeichoka!!
Ili tokea tumepanda kipanya pale mwenge kwenda buguruni.pale mwenge walipanda Wanajeshi 3 kufika sheli wakapanda wanajeshi wengine 2! Kuona hivyo konda akaanza kulalamika,wale Wanajeshi wakaona konda hakutumia lugha nzuri(konda alimwambia dreva kwa sauti ya chini kuna mawe matano kumbe walisikia!) wakaapa hawashuki na lazima dreva awapeleke! Sisi abiria kimyaaa! Kuona hakieleweki konda na dreva wakasema hawajachukua nauli ya mtu hawaendi tena buguruni! Wakaenda baa ya jiranh pale sheli wakaagiza supu kabisaaa! Wanajeshi nao wakaapa watalala humo hadi warudi wawakomeshe! Mie nikakamata mchuma mwingine nikaondoka zangu!!
 
Abiria: Kuna kiti au unasema panda tu?
Konda: Hao wengine wamekalia ndoo?

Abiria: Ebu tupunguzieni sauti ya redio
Konda: Sheria za nchi tu zinatushinda, tusikilize na zako, hebu tupunguzie misheria

Mama: Bwana ondoa gari joto sana
Konda: Usituzingue wewe shuka upande friji
Siku moja nimepanda daladala Gongo la Mboto kwenda Posta,hiyo daladala lilikuwa na konda mbabe sana alikuwa anahakikisha hapandi mwanafunzi! Siku hiyo kuna wanafunzi 3 wa Azania wakapanda kwa taabu sana na matusi wakaporomoshewa kibabe! Tulipofika Baridi mnazi mmoja wale madenti wakashuka kumbe siku hiyo walimpania yule konda hivyo kila mmoja alikuwa ameficha waya kwenye shati alafu wamechomekea! Ghafla walivyoshuka tu konda akaanza kupigwa waya! Konda alipigwa waya hadi akachanganyikiwa damu tupu! Dreva nae kuingilia waya ukatembea vibaya mno! Wale vijana wakakimbilia kariakoo na safari yetu ikafia hapo maana konda damu na dreva damu!! Hii ni mwaka 99!!
 
Hahahah!sasa usiombe ukakaa siti moja na mlevi af akaanza kukulalia ile kiusingizi!
 
Back
Top Bottom