Rage, Sophia Simba wapanda kizimbani

Mutukwao

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
211
25
Kesi ya igunga ambayo inafanyika hapa igunga imefikia patamu jana pale waziri sophia simba na aden rage walipotoa ushaidi wao jana.hivi leo asubuhi ccm wamekataa kuendelea na kesi kwa kile kinachoonekana hawana imana na jaji anayeendesha kesi hiyo.baada kwenda kujadiliana kidogo kati ya jaji na wakili wa ccm hatimaye kesi inaendelea kama kawa.
 
Kesi itaendelea j3 but th blowing wind is about unroot th ccm trees!
 
Kafumu asipo nyang'anywa ubunge kwa yale mabastola ya Rage, Mahindi ya BM, Daraja la Magufuli nk nitajua kweli haki haipatikani mahakamani.
 
SiSieMu watashinda tu. Tumeshachoka na udhalimu wao kilichobaki ni kuwatoa tu.
 
IJUMAA, MEI 18, 2012 | NA ABDALLAH AMIRI, NZEGA

* Ni katika kesi ya uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga
* Rage aeleza bastola yake ilivyoonekana jukwaani
* Chakula alichokula Sophia Simba Igunga champonza
* Adai aliandaliwa na ndugu yake, ashindwa kumtaja jina


MBUNGE wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wamepanda kizimbani.
Rage na Sophia Simba walipanda kizimbani jana wilayani hapa ili kutoa ushahidi wa kesi ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi Mbunge wa Igunga, Dk. Peter Kafumu (CCM).

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ilifunguliwa na mlalamikaji Joseph Kashindye dhidi ya Dk. Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Igunga. Kesi hiyo iliendelea kusikilizwa jana mjini hapa katika Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora.

Rage ambaye ni shahidi wa 15 kwa upande wa wajibu madai, alikiri kushiriki kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, ambapo alipangiwa na chama chake kufanya uratibu katika Tarafa ya Igulubi wilayani Igunga.

Akiwa mahakamani hapo, Mbunge huyo wa Tabora Mjini, alitoa maelezo yake huku akiwa ameketi katika kiti kilichokuwa kizimbani hapo.

Baada ya kutoa maelezo hayo, wakili wa mlalamikaji, alianza kumuuliza maswali shahidi huyo juu ya umiliki wa bastola yake na kwa nini alikuwa nayo katika mikutano mbalimbali ya kampeni jimboni humo.

Wakati akijibu maswali hayo, Rage alikiri kumiliki bastola hiyo pamoja na kushiriki nayo katika shughuli nzima za kampeni wakati huo.

Hata hivyo, alisema upepo ulimponza hasa pale ulipopeperusha shati lake na kusababisha bastola yake kuonekana hadharani na kupigwa picha na waandishi wa habari waliokuwa mkutanoni hapo.

"Pamoja na kufanya mikutano mbalimbali hasa wakati nilipokuwa ninapanda kwenye jukwaa la kampeni, upepo mkali ulifunua shati langu na kusababisha bastola kuonekana hadharani na ndipo waandishi wa habari walianza kuniangalia na hatimaye walinipiga picha.

"Picha ile ilionekana katika Gazeti la Mwananchi la kesho yake,'' alisema Rage.

Alisema kuwa, baada ya kutokea tukio hilo, bastola hiyo ilichukuliwa na Jeshi la Polisi kwa maagizo ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kisha akahojiwa na jeshi hilo.

Alisema pia kwamba, pamoja na kuhojiwa pia alipigwa faini ya Sh 100,000 na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi.

Katika utetezi wake huo, Rage alitumia zaidi ya saa tatu mfululizo, ambapo alisema suala la yeye kuwa na bastola lilimalizika baada ya Kamati ya Maadili kumpiga faini kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

Wakati huo huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, ambaye alikuwa shahidi wa 16 kwa upande wa mjibu madai, alitoa ushahidi wake ambapo alikiri kula chakula na wanachama wa CCM katika Hospitali ya Nkinga, Kata ya Inkiga.

Waziri Simba, alisema alishiriki kula chakula hicho baada ya kupata mwaliko kutoka kwa ndugu yake ambaye, yupo katika hospitali hiyo ingawa alipoulizwa jina la ndugu yake huyo alishindwa kulitaja.

Licha ya kula chakula hicho, Simba alisema alikula yeye pamoja na watu zaidi ya 50, hali ambayo iliwafanya mawakili wa mlalamikaji waendelee kumuuliza maswali, likiwemo la kudaiwa kuwahamasisha wasimchague Kashindye kwani hana mke na ni masikini, madai ambayo aliyakanusha vikali.

Kesi hiyo ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Dk Kafumu, inasikilizwa na Jaji Mery Shangali na inaendelea leo.

Wakati ikiendelea, tayari mashahidi 22 upande wa mlalamikaji tayari wameshatoa ushahidi.


 
Unajua ushahidi wa uongo huwa unasumbua sana upande ule unaotunga uongo. Fuatilia yale yaliyosemwa na Rage & Sophia Simba (Mwananchi leo) uone walivyoongea uongo mkavu kabisa.
 
Tuone kama walifanya fair game, Sophia hawajui hata hao ndugu zake aliyekuwa anakula nao wali

Rage, anasema Upepo ndio uliokuwa unaoionyesha hiyo Pistol yake; na sio yeye na Ubabe wake

CCM na nguvu za dola; sasa Mahakamani wanabadilisha story na watashinda hiyo kesi pamoja na Mbunge wao kusema Uongo kuwa Mpinzani wake amejitoa kugombea Ubunge
 
Kama kuwa na bastola ni sahihi kwa nini alipigwa faini hiyo laki moja? shullingi laki moja ilikuwa ni faini ya nini? hivyo ni moja kwa moja Rage alifanya makosa au ilikiwa kosa kupanda na bastola jukwaani, pili hivi hiyo impunity ya Rage inatoka wapi?
 
our judiciary system is politicized dont expect anything valuable out of this case!!
 
Huyu si yule mama muimba maneno ya mipasho, sina hakika lakini kwa kauli zake anaweza kuwa alisema haya maneno machafu kabisa..nyani haoni kundule yeye toka u-PS mpaka uwaziri haoni kuwa maisha ni safari na uwepo wa masikini ndiyo sababu ya kuwepo matajiri pia?

Hana aibu huyu mama..mbona ye hatujauliza mafanikio yake aliyapataje? Kashifa za utajiri na umasikini ni matusi makubwakwa watanzania maan 99% ni masikini hoehae.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom