Mjukuu wa bibi Pili.
Member
- Dec 21, 2011
- 71
- 75
Mbunge wa jimbo la Tabora mjini Ismail Aden Rage amechukua vyombo vya muziki vilivyokuwa vikitumiwa na bendi ya sensema malunde ya mkoani humo hali iliyopelekea bendi hiyo kusitisha kufanya maonesho kwa wiki tatu sasa.
Wakizungumza na gazeti hili viongozi wa bendi hiyo kwa sharti la kutotajwa majina walisema hatua hiyo ya Rage imewasikitisha sana na ina lengo la kuivuruga na kuiua bendi yao.
Walisema mapema mwaka jana kabla ya uchaguzi mkuu uliohusisha wabunge,madiwani na rais,Rage aliufuata uongozi wa bendi ya Sensema Malunde akawaeleza kuwa atanunua na kuleta vyombo vya muziki vipya kwa ajili kufanya matamasha pamoja na kushiriki katika kampeni za uchaguzi za chama cha mapinduzi.
Aidha walieleza kuwa mbali na makubaliano hayo pia walikubaliana baada ya vyombo hivyo kuanza kutumika asilimia 80 ya mapato yatakwenda kwa mmiliki ambaye ni Rage na asilimia 20 itabaki kwa viongozi.
Walisema makubaliano mengine ni pamoja na kulipa mishahara ya wanamuziki na vyombo vya bendi vya zamani viwekwe ndani.
Wameongeza kuwa baada ya vyombo hivyo kuwasili,kazi ilianza mara moja ikiwemo upigaji katika kumbi mbalimbali za burudani katika mji wa Tabora na vitongoji vyake.
Aidha wamebainisha zaidi kuwa pamoja muziki kupigwa kwenye kumbi mbalimbali za burudani pia bendi hiyo ilikuwa ikifanya kampeni zake za ubunge.
Wanasema hali ilianza kuwa mbaya mwanzoni mwa mwaka huu,ambapo hadi kufikia mwezi machi mwaka huu wanamuziki walianza kusotea mishahara yao na ndiyo ukawa mwisho wa na mparaganyiko wa bendi.
Walisema Rage alichukua vyombo vyake vya muziki,na kuvifungia ndani na baadhi ya wanamuziki amewahamishia jijini Da-es-Salaam kutokana na tetesi kuwa anataka kuanzisha bendi yake huko.
Mwisho-