Rafiki yangu na dada yangu wananichanganya.

umekuwa mkali sana mbona?

Hebu pumzika basi unywe maji kwanza ghadhabu ishuke.

kwa vyovyote vile mna tabia zinazofanana

na ndo maana mkawa marafiki

sasa mungu ametafuta namna ya kukurudishia yote uliyowafanyia wengine.....

what goes around....comes around
 
Kha, unless huna cha kufanya ktk maisha !! Kwani walipoanzana wewe ulikuwepo au saidia kushika miguu ??
Huwezi kufanya lolote sana sana zidi kumwombea huyo ndg yako period !

Jaman nina rafiki yangu ambaye tumekuwa marafiki kwa muda mrefu sasa ila namjua ni tapeli na malaya sana na ameoa wake zaidi ya wawili bila ndoa na kuachana nao sasa cha kusikitisha zaidi amemrubuni dada yangu na anataka kumwoa na tayari ameshampa ujauzito.Nimeshindwa nimsaidieje dada yangu huyo.Nisaidieni mawazo.
 
pole sana,lakini chakukufanya wewe kukumbuka shuka kushakucha nikipi? au unataka kusema kama walipo anzana ulikua hujui na umekuja kujua wakati anamimba ndio akakwambia ya huyo jamaa? kumueleza kua huyo bwana sketi haimpiti nisawa
lakini je yuko tayari kukusikia achilizaa mbali kukuelewa?,je kama huyu bwana keshamwambia wenzie hao Salome,Rita,Semeni,Avintishi,Kusudiyao na Mtakavyo wate walikua wakorofi lakini kwa ndguyako amefika na muhusika ameamini 100% utaweza hata kunyanyuka kichambo chake? minaona kaa kimnya utizame yanavyoenda,yakimshinda atawachaa....
 
Jaman nina rafiki yangu ambaye tumekuwa marafiki kwa muda mrefu sasa ila namjua ni tapeli na malaya sana na ameoa wake zaidi ya wawili bila ndoa na kuachana nao sasa cha kusikitisha zaidi amemrubuni dada yangu na anataka kumwoa na tayari ameshampa ujauzito.Nimeshindwa nimsaidieje dada yangu huyo.Nisaidieni mawazo.
watu uwa wanabadilika
 
Waswahili husema shetani akizeeka huwa malaika. Inawezekana kabisa kuwa jamaa ndo ameamua kutulia na dadako, hivyo wape muda.
 
Usijiingize katikati ya Mapenzi ya Watu, utaja umbuka

Mwache Dada yako au afaidi au aumie Basi
 
Kwanza urafiki wa hivyo siupendi kabisa,huenda hakuwa friend wako ila alitumia chance hiyo tu ili apate njia yakumpata sist wako tu;huna jinsi kaa pembeni ucheki tu
 
Jaman nina rafiki yangu ambaye tumekuwa marafiki kwa muda mrefu sasa ila namjua ni tapeli na malaya sana na ameoa wake zaidi ya wawili bila ndoa na kuachana nao sasa cha kusikitisha zaidi amemrubuni dada yangu na anataka kumwoa na tayari ameshampa ujauzito.Nimeshindwa nimsaidieje dada yangu huyo.Nisaidieni mawazo.

Maliboro sijaelewa ilikuwaje ukawa na rafiki ambaye wewe mwenyewe unashuhudia kuwa ni tapeli na malaya halafu ulifikiri nini mpaka ukampeleka nyumbani kwenu akakutana na dada yako. Je inawezekana ule msemo wa "birds of the same feather fly together" unahusika kwako pia?

Tuache hilo kwanza. Mimi nakushauri uendelee na mambo yako kwani hawa dada zetu wana mfumo tofauti sana wa kufikiri na kufikia maamuzi. Wakishaingiwa na huu ulevi unaoitwa mapenzi vichwa vyao huwa vinabadilika kabisa na huwa wako tayari kujitoa kafara mfano wa wale wanaojilipua mabomu. Nakuhakikishia kuwa hata ungempa siri zote za utapeli na umalaya wa rafiki yako ikiwa ni pamoja na hilo la "kuoa bila ndoa" bado angeinua sketi tu na kupata hiyo mimba.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
this is really the case of 'birds of the same feather fly together'.... unajua fika kwamba rafiki yako ana tabia chafu na bado unamruhusu kuwa close na familia yako! umevuna ulichopanda, to say the least
 
Tatizo unaweza ukampa ushauri then ukaonekana wewe ni mbaya hivyo basi kuwa mpole sababu uwezi jua kwa dada yako atatulia kuliko unavyofikili maana kila shetani na mbuyui wake ni hayo tu.
 
mume wa dada yako ni shemeji yako so kuwa mpole tuu, dada huyooo anaolewaaa, mahariii ishatolewaaa

Hata mimi nashangaa mtu mwovu wa kiasi hiki eti ni rafiki yake..hawakukosea waingereza waliposema..'Tell me your friend and i will tell your behaviour' or 'birds of the same feathers flock together'!..
Mwambie dadaako Ukweli ili ajue CHOO alichokiingia kuwa ni cha KIUME!!..inaweza imsaidia baadaye!
 
wacha watifuane wakishindwana si basi utajuaje kama maisha ya dadako ndo yatanyokea kwa huyo tapeli kila shetani na mbuyu wake.
 
Back
Top Bottom