Rafiki kipenzi kutembea na X wako-imekaaje hii?

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Wadau nina rafiki yangu mkubwa sana ambaye nimejua kuwa kwa sasa anatoka na aliyekuwa girlfriend wangu ingawaje wenyewe wanafanya siri sana.,hii imekaaje?.,inamaanisha kuwa hata enzi zile mapenzi yalipokuwa motomoto jamaa alikuwa akimtamani kama vile fisi anavyosubiri kwa hamu simba amalize kula nyama ili aibuke na mifupa?
 
Sasa dogo mbona unasumbua akili yako, huyo wewe umeisha wachana naye vipi ukae unakereka..au ulijidai mwamba kumbe bado unapenda.


Mimi sijali rafiki yangu akachukue x wangu kama nao, ubaya mimi sina ma X mana sichezi na wajinga :biggrin:
 
Sasa dogo mbona unasumbua akili yako, huyo wewe umeisha wachana naye vipi ukae unakereka..au ulijidai mwamba kumbe bado unapenda.


Mimi sijali rafiki yangu akachukue x wangu kama nao, ubaya mimi sina ma X mana sichezi na wajinga :biggrin:

Dinnah yuko wapi aisee lol:biggrin::biggrin:
 
Yote yanawezekana,pengine alikuwa anamtamani tangu ukiwa nae au ulipomuacha wakawa na ukaribu,akaona thamani yake....wanasema ukisema wa nini wenzio wanauliza watampata lini... songa mbele,heshimu maamuzi yao na kubali hali halisi.
 
kwani we uliweka pingamizi la mahakama ...? nawe c unaye mpenzi kwa sasa...? acha kumfuatilia usiwe na kisebusebu.
 
Yote yanawezekana,pengine alikuwa anamtamani tangu ukiwa nae au ulipomuacha wakawa na ukaribu,akaona thamani yake....wanasema ukisema wa nini wenzio wanauliza watampata lini... songa mbele,heshimu maamuzi yao na kubali hali halisi.

hahahhah..Ule msemo wa ukimuona wa nini, wenzio wanasema " nitampata lini"... una ukweli!
 
Niliwahi soma hii:
I don't feel jelous when I seem my BF with another gal, my mom taught me about leaving my old toys to the less fortunate kids

Achana nao, omba Mungu usigeuke miserable halafu wakawa na couple ya mfano, utajuuuuuta kumuacha!
 
Alikuwa,that means PAST.Achana nae,kama mlimwagana,inauma nini?..Mi nahic kwa gals ndo huuma sana,na boys hutumia kutoa maumivu kwa kutoka na rafik yake ambae mzur kushinda yeye,na ukute analitambua.ata kama ana bwana mwingine.Ila wewe man,find atakae mfunika haitakuuma..Songa mbele.Kutoka na rafik yako kawaida sana.Hakuna bind yoyote btn you 2.
 
Kila mtu na akili yake, wewe labda usingeweza kutembea na X wake lakini yeye kaweza, wasikushughulishe kula kikushuke na kama walivyokufanya hujui basi na wewe ndio kua zuzu kabisa wape nafasi wasije kujigonga na visiki kwa kuku hofia weye.
 
waache na mahusiano yao, ila uwe macho tu na huyo rafiki yako, anaweze kukuzunguka kwenye mambo makubwa ukashangaa
 
Ndivyo binadamu tulivyo. Ww ukiwaza 'ntamwacha lini?' wenzio wanafikiria 'tutampata lini?' kuwa mwangalifu kijana hao jamaa wasije tena kukuchukulia ulienae kwa sasa!
 
Haina shida dogo, as long as huyo mshikaji hakuwa sababu ya wewe kuacha mzigo wako , get over it songa mbele.
 
kuuma lazima iume,lakini si wako tena.unaweza shangaa jamaa akaja kuoa kabisa,its part of life.we songa mbele kamanda
 
hahahah mkuu uliacha kwa majaribio????? ukiamua umeamua si kuanza kuangalia nyuma ulikotoka pakoje au panaendaje
 
acha wivu wa kijinga, asa ulitaka akaki tu bila rafiki kwanza naomba umshukuru huyo rafiki yako
 
Hapa ishu sio kuendelea kumtamani huyo mwanamke,tulishaachana na life goes on, an interesting thing here ni kwamba jamaa ni zaidi ya rafiki kwangu,urafiki wetu ni wa tangu utotoni na hata wazazi wetu ni wameshakuwa ndugu kabisa,hata nilipokuwa naenda kumtembelea huyo demu nilikuwa nafikia nyumbani kwa jamaa, sijui hata yeye mwenyewe anafikiria nini kwa sasa maana si mnajua hawara hana talaka?
 
Najaribu kufikiria kuwa si ina maana lazima atafeel insecurity fulani maana kila akiniona anajua kuwa nimeshamrukia mkewe na naweza kuendelea kumrukia anytime.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom