Radio 5 yamchomolea Diamond show Arusha 08-12-2015

Unko T

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
200
266
Wajua tena sisi mwezi huu tunakwenda nyumbani kwa ajili ya kukutana na familia zetu.

Juzi Nilipokuwa Dar nilikuwa nasikia matangazo Radio 5 FM...91.3 Dar kuwa Diamond atakiwasha Geneva of Africa tarehe 08-12-2015. Na nikasikia interview ya Kitale na akapost Instagram.

Sasa jana nafika hapa home Boma Ng'ombe naweka 105.7 ������������ Sisikii kitu juu ya Diamond Platinumz.

Nikauliza kulikoni, naambiwa radio 5 haipigi tena matangazo ya Diamond Platinumz.

Sasa sijui na shoo imefutwa au bado ipo?

Nimetuma ujumbe mfupi kwa radio hiyo, sijajibiwa.

Ningekuwa nasikia radio nyingine ya Arusha nje ya Arusha ningeuliza maswali haya ila sina njia mbadala.

Wana-Jamvi naomba kujuzwa nini kimetokea kati ya ndugu Naseeb Abdul na Radio 5 FM
 
Mmiliki wa hiyo radio yuko chama gani? Asije akawa analeta mambo ya politics kwenye business...!
 
Ulivyoandika heading nikajua unatupa taarifa, kumbe wewe ndo unatafuta taarifa kwetu
 
Unatuletea redio za wenyeviti wa mitaa, kila mtu anayake??? Nacheki nana mtvbase hapa
 
Wausika na wenyeji wake ni TRIPLE A na wanamiliki radio yao (TRIPLE A FM ) kwahiyo kama kungekuwa na tatizo ungelisikia kwa wenyeji wake(triple A FM) na si sehemu nyingine, lakini ngoja nikupe nyongeza yeye kaitwa kufanya shoo kwahiyo swala la promo halimuhusu na ameshapewa kianzio japo wenyeji wanaweza kumuhusisha kwenye promo ya ktk media kutegemeana na makubaliano yao.
 
Nipe frequensi ya Triple A Moshi na Dar mkuu. Show ipo au haipo?
 
Back
Top Bottom