Radio 104.1fm inatumika vibaya?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
Ndugu zangu wana JF, usiku wa kuamkia leo (kuanzia saa tatu hivi) nilipata nafasi nyingine ya kusikiliza kipindi fulani kutoka radio inayomilikiwa na taasisi ya dini ya Kiislamu hapa Tanzania.

Mada ilikuwa 'Waislamu na historia ya Tanzania'. Msemaji, ambaye mtangazaji
alikuwa akimwita shehe, alikuwa akijibu maswali yaliyokuwa yanaulizwa na mtangazaji huo.

Swali mojawapo liliuliza kama Mwalimu Julius Nyerere ni mwasisi wa Chama Cha TANU au ni Baba wa Taifa la Tanzania. Shehe huyo alijibu kwamba Mwalimu Nyerere hakuwa mwasisi wa TANU au TAA wala Baba wa Taifa. Badala yake
waasisi/waanzilishi wa Chama Cha TANU na TAA walikuwa Waislamu (aliwataja kwa majina), ambao hawajawahi kuenziwa hadi leo kwa vile ni Waislamu na hivyo hawajulikani kabisa.

Alidai historia ya Tanzania imepotoshwa makusudi kwa sababu ya udini. Yeye alijaribu kuelezea historia ambayo alisema ni sahihi kwa kuwataja hao waasisi wa TAA/TANU na taifa la Tanzania.

Swali jingine aliloulizwa shehe lilikuwa ni kwa nini baadhi ya viongozi wastaafu hawakuhudhuria kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 48 ya Uhuru wa
Tanganyika Jumatano iliyopita. Alijibu kuwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alihudhuria na mara alipoonekana Uwanja wa Uhuru, watu wengi sana walimshangilia kwa kukumbuka neema aliyoleta Tanzania enzi za utawala wake.

Alisema Rais Mstaafu Benjamini Mkapa aliogopa kuhudhuria kwa sababu
watu wangemzomea kama fisadi (kwa mujibu wa gazeti alilonukuu) ila alisema habari zingine zinaeleza alikuwa na udhu. Na kwa Rashidi Kawawa, alisema
alikuwa nje ya nchi kwa matibabu.

Swali jingine lilihusu mwafaka wa CCM na CUF. Shehe huo alidai wanaopinga mwafaka kati ya CCM na CUF siyo wengine bali ni Wakristo. Alisema Waislamu hawawezi kupinga kitu kizuri kama hicho. Ili kuthibitisha hoja yake, alinukuu maoni ya Waziri Mkuu Fredrick Sumaye (ambaye ni Mkristo), aliyotoa kwenye Kongamano la Mwalimu Nyerere Foundation hivi karibuni kuwa yeye (Sumaye) hana imani na makubaliano ya kuunda Serikali ya mseto yanayofanywa na Serikali za Kiafrika.

Alinukuu gazeti mojawapo lililoandika kuwa Sumaye "hakubaliani na baadhi ya Serikali za Kiafrika zinazong'ang'ania madarakani na badala yake kuvitaka vyama vya upinzani kuunda Serikali ya mseto." Nilivyoelewa, Sumaye alitaka kuwepo uwazi zaidi katika kufikia mwafaka na siyo katika mazingira ambayo chama tawala kinatumia nguvu za dola kung'ang'ania madarakani (kama ilivyotokea Kenya na Zimbabwe). Ila Sheshe alitoa 'judgement' ya jumla tu kuwa wanaopinga mwafaka ni mafisadi (ambao ni Wakristo).

Shehe alidai Waislamu wanaunga mkono Serikali ya mseto na hawawezi kupinga juhudi zinazofanywa kuondoa tofauti za kisiasa. Alihoji, "Kwa nini Sumaye hataki CCM na CUF wazungumze kwa amani na kuafikiana? Je, anataka wandelee kuvutana na kwa maslahi ya nani?"

Katika baadhi ya magazeti aliyokuwa akinukuu habari zake ni yale yanayomilikiwa na taasisi za dini ya Kiislamu, hasa yalipokuwa yakishabikia hoja alizokuwa akizitoa.

Binafsi napenda sana uhuru wa kutoa mawazo/maoni ila nasikitika sana kwamba kwa viongozi wa dini wanaoheshimika na watu wote kutoa mawazo kama ya shehe huyo ni kujidhalilisha kabisa na kuonyesha upeo mdogo wa kufikiri au kupotosha habari kwa maslahi binafsi.

Ningependa sana viongozi wa dini zote waoneshe 'maturity' na busara wanapozungumzia mambo yanayoweza kuleta ubaguzi wa kidini nchini. Nilijiuliza: mahubiri ya namna hiyo yanalenga nini hasa kwa vijana wa Kiislamu au hata tu vijana (na watu) wa dini nyingine wanapoyasikiliza na kuyashika?

Ndugu wana JF, naomba mchangie kwa hili. Nia ni kujaribu kuona kama kwa jinsi mambo yanvyoenda tutaweza kwa baadaye kuishi kwa amani tena kama viongozi wetu wa dini wanaanza mchakato mchafu wa kupotosha mambo kama huyo shehe. Binafsi sioni kama mahubiri kama haya yanatujenga!
 
I cant waste my time to listen poor arguments from MASHEHE.
 
Makubwa...
nahisi kama kuna kupandikiza chuki fulani ya kidini vile.....
Waislamu ni watu safi, ila wapo wasio na mapenzi mema na taifa hili.
Miongoni mwao ni huyo muandaaji wa kipindi na huyo mgeni wake ambaye ni shehe
 
kibaya kwako kizuri kwa mwenzako.

Kuna Tume ya habari Tanzania, kama unaona walikuwa wanavunja sheria za nchi basi wape taarifa washughulikiwe.
 
nimewahi kusikiliza hii radio mara kadhaa, lipo jambo moja ambalo nahisi ni kua inakosa wanahabari wasomi kama zilivyo radio zingine, wanashindwa kupambanua mambo katika mwanga uliobora, naamini lipo tatizo hapa.
 
Back
Top Bottom