Radi Iliua Timu nzima ya Mpira wa Miguu nchini Kongo!!! Oct, 1998

Osaka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
1,762
551
Wasalaam wana JF!
Bara la Africa linasifika kwa matumizi ya nguvu za giza katika michezo mbalimbali hasa hasa ktk mashindano ya mpira wa miguu ( soccer).
Timu nyingi za Africa ya Magharibi kwa miaka mingi zimekuwa zikitumia uchawi (fetishism) ktk kabumbu, uchawi huo unajulikana kama kama: juju au muti . Huku kwetu tunaita ndumba au omuti.

Katika moja ya matukio ya kushangaza ikiaminiwa kuwa kuna mkono wa mtu (the black magic) ktk mchezo wa soccer, ni pale timu moja ya mpira wa miguu ikiwa na wachezaji wote 11 walipokung’utwa na radi wakati timu pinzani ikibaki salama bila ya mchezaji hata mmoja kudhurika! Tukio hili lilitokea nchini Kongo miaka ya nyuma kidogo (28 Oct, 1998).
Source: http://www.independent.co.uk/news/lightning-kills-an-entire-football-team-1181336.html


Hata kwetu hapa bongo tumeshuhudia baadhi ya timu zetu za soccer , wachezaji wake wakiruka ukuta bila kutumia milango maalumu ya viwanja vya mpira katika hisia kuwa timu pinzani itakuwa imefanya ‘vitu’ vyake mapema ktk milango hiyo.
 
Mi ndio naisikia. Nimeigoogle nimeikuta ni kweli...Aisee, sisi waafrica ni noumer!
Nadhani hata wazungu waliachwa midomo wazi na tukio hilo la kipekee!!
 
Mi ndio naisikia. Nimeigoogle nimeikuta ni kweli...Aisee, sisi waafrica ni noumer!
Nadhani hata wazungu waliachwa midomo wazi na tukio hilo la kipekee!!

Hii ndio sanaa ya watu wa Afrika.
 
Hii sanaa si ije hapa kwetu ichakaze baraza zima la mawaziri ili tuanze upya?
 
Back
Top Bottom