R.Mengi for President?

Status
Not open for further replies.
Nilivyomuona mimi mengi ni mfanya biashara per se mwenye sifa zote za ubepari. Narudia huo ni muono wangu. Sina shida na yeye kuwa bepari. Na ndio maana nikaona ni bora aendelee kwenye channel ya biashara. Nilivyompima nilimuona ana uwezo mkubwa wa kumanage biashara kuliko watu. Ndio maana nina wasiwasi iwapo ataweza kutumanage kama akiwa rais

Dunia tuliyoko tunahitaji viongozi wenye sifa zake.
Shida tuliyonayo ni ufisadi!
Na yeye alianza kupigana hivyo vita kabla mimi na wewe hatujawa na mwamko huo!
Huyu jamaa angetaka kukaa kimya bila kuukemea ufisadi tungekuwa wapi leo?
Nani asiyejua anaheshimiwa na angetaka kuitumia heshma anayopewa kwa kujikomba kwa viongozi sisi wananchi wa kawaida tungekuwa wapi leo?
Unazungumzia kuhusu mabepari!
Ni kiongozi gani tuliyenaye/tuliyekuwa nao ambao si mabepari?
Mkapa?
Chenge?
Lowassa?
Mwinyi?
nani?
Tumpe fair disscussion!
 
jmushi1 heshima yako kaka!
hivi leo hii wakisimamishwa mengi na dr slaa nani anaweza kupata kura yako?...ni mfano tu naomba jibu tafadhali
 
jmushi1 heshima yako kaka!
hivi leo hii wakisimamishwa mengi na dr slaa nani anaweza kupata kura yako?...ni mfano tu naomba jibu tafadhali

Either or!

Nia yangu ni kuwa licha ya kwamba R.Mengi hajatangaza hivyo..just kama ilivyo kwa Slaa..Basi tuwape wote a honest,respectfull and a fair discussion.
 
ngoja nikusaidie kitu kimoja, si kila unayemuona anasimama mbele za watu na kuongea na kupigiwa makofi ukahisi anaweza siasa auanaweza kuongoza.
mfano mzuri kwa rais wenu kikwete, alikuwa anajaza watu kwenye mikutano mpaka anakosa hewa anaanguka na kupoteza fahamu, lakini leo hii kila kona ya serikali yake ina uozo. so mi nahisi hata huyo mengi akipewa nafasi sidhani kama ataitumikia kama unavyohisi ukizingatia hajawahi kuwa hata katibu tarafa.
MFANO...marekani kuna wafanyabiashara wakubwa wanaokubalika wenye uwezo wa kusimama na kuongea wakasikika but kwa nini hawajihusishi na siasa?
sasa hapa ndo utapogundua kuwa siasa ni wito...so muache mzee mengi adili na kile anachokiweza
 
Watanzania wenzangu...
"KIFIKRA" naweza kusema bado tuko kwenye Ujamaa.

"KIVITENDO" tuko ama tunamalizia kuelekea kwenye ubepari!
Na hapa ndipo tunakuwa na "Transitition Period" ama kikwetu "Kipindi Cha Mpito"

Hapo katikati "Kwenye utambuzi wa kifikra na kivitendo" ndio tumekwama!
Hivyo basi Viongozi wetu nao hawasiti kuutumia udhaifu huo wa mkwamo wa katikati ili ku gain na ku claim political credits na hivyo kuendelea kututawala!

Viongozi wetu hawataki kuwaelimisha na kuwaandaa wananchi wake kuwa sasa tuko kwenye mbio kali za MARATHON za UBEPARI ili kuwawezesha kukabiliana MARATHON hizo kifikra na kivitendo!

Kutofanya hivyo kumepelekea wananchi kuwa na mawazo potofu na hivyo kubakia kwenye umasikini na kushindwa kufanya maamuzi ya busara pale inapokuja kwenye suala la kujichagulia viongozi bora!

Ni wazi kuwa nyakati hizi si kama zile za zamani ambapo siasa pekee zilitosha kumpeleka kiongozi ikulu!
Siasa kama za kina Mwalimu.

Dunia ya sasa ni yenye ushindani wa hali ya juu na hivyo tunahitaji Viongozi wenye kulielewa hilo!
Kipindi hiki cha Mpito tunahitaji Kiongozi/Viongozi wenye uwezo si tu wa kisiasa..Bali wa ki FIKRA na wa KIUTENDAJI BORA!

Kipindi cha nyuma enzi ujamaa ulipotukolea tulikuwa tukihitaji watu wenye vipaji vya kuongea na kutumobilize under those ideas!

Sasa hivi tumeshajua idea ni UBEPARI lakini KIFIKRA bado tunadhani ni UJAMAA!

Nyakati hizo ni historia ila mbongo zetu hazitaki ku acknowldege hilo na kwasababu hiyo viongozi wetu bado wanataka kuendelea kuutumia udhaifu huo na kutokuelewa huko ili kuendelea na ufisadi!

Mkapa wakati anaingia madarakani alijua hilo!
Akaamua kutomshika kipofu mkono wakati wa kula naye! Kwasababu alijua kwa kufanya hivyo..Basi yeye alikuwa hajaqualify kushika madaraka ya nchi!

Alijitahidi akaja na ule utaratibu wa white paper ili kusafisha mikono kama Pilato!

Isitoshe akatuona sisi ma mbumbumbu kwa kututangazia mali zake wakati anaingia madarakani ili tudhani kuwa na yeye ni swafi na hivyo hataiba mali zetu! Hili lilimsaidia kuiuza nchi yetu jumla huku tukiwa tumelala!

R.Mengi aliliona hilo na kuanzia hapo Mkapa akawa ni adui mkubwa kwake na kwa Taifa zima!

Hakutaka kuwaambia wananchi ukweli kuwa kuwa na mali si sababu tena ya kunyimwa uongozi kwenye mfumo huu wa kibepari!

Wote tunafahamu alilolifanya mara baada ya kuondoka madarakani na sasa hata ukitaka kujua mali zake unaweza fungwa!

Wananchi wenzangu wakati wa kuendelea na mjadala huu naomba tujiulize..
Je sifa za kugombea uraisi ni zipi hizo kwenye mfumo wetu huu?
Je ni kiongozi wa aina gani tunayemuhitaji?

Shurti tujiulize maswali mchanganyiko kabla hatujaamua kuwa Nchi hii tumpe nani!
 
Mengi anaogopwa na Kikwete sana na kunawasiwasi wa mbinu za kumzia asiingie kwenye siasa. Kikwete haamini kama vitu vyote vizuri mengi anavyofanya ni kwa roho nzuri tu na si kutafuta siasa lakini anaweza kuingia hatarini kwa kushukiwa.
 
ngoja nikusaidie kitu kimoja, si kila unayemuona anasimama mbele za watu na kuongea na kupigiwa makofi ukahisi anaweza siasa auanaweza kuongoza.
mfano mzuri kwa rais wenu kikwete, alikuwa anajaza watu kwenye mikutano mpaka anakosa hewa anaanguka na kupoteza fahamu, lakini leo hii kila kona ya serikali yake ina uozo. so mi nahisi hata huyo mengi akipewa nafasi sidhani kama ataitumikia kama unavyohisi ukizingatia hajawahi kuwa hata katibu tarafa.
MFANO...marekani kuna wafanyabiashara wakubwa wanaokubalika wenye uwezo wa kusimama na kuongea wakasikika but kwa nini hawajihusishi na siasa?
sasa hapa ndo utapogundua kuwa siasa ni wito...so muache mzee mengi adili na kile anachokiweza

Na kutokana na posting yangu iliyopita..Then unaweza kugundua kuwa kwanini wamarekani wanaweza kumchagua raisi kutegemeana na single issue ambayo ina waface kama vita ama uchumi!

Bush hakuwa maarafu..Lakini sifa ya kuwa tafu dhidi ya mwarabu ilmpa nafasi nzuri!

Pia sifa yake ya kuongoza kampuni zake pamoja na timu ya baseball vilikuwa mojawapo ya vigezo!
Clinton naye alkuwa maarufu kwasababu a uchumi!

Sisi tuna shida ya utawala makini kwenye kipindi hiki cha mpito na ufisadi uliobobea!

Umasikini, maradhi na ujinga bado ni adui anayepigiwa kelele za kisiasa peke yake!
Utendaji ni ufisadi!
Kutokana na hayo yote..Tunatakiwa tujifunze...Kuwa ni lazima tuwe tunachagua viongozi kutokana na matatizo tunayokabiliana nayo.

Kujijengea tabia ya kujiuliza na kupenda mabadilko positive..

Na hivyo kutufanya kuwa watu wenye kukumbuka watu wa aina fulani kutokana na aina ya challenge tunazokabiliana nazo!

Tunahitaji viongozi wanaoelewa kuwa ni nini kinaendelea na hivyo kuwa ni viongozi wenye kuweza kunegotiate on our behalf wakati wa mchakato mzima wa Soko Huria!

Viongozi wanaoenda kwenye negotiations huku wakiwa na kumbukumbu za wananchi wao!
Wasio penda rushwa wala ufisadi!

Watakaozisimamia rasilimali zetu na kusimama mbele za mzungu na kunegotiate with a firm resolve!

Hatutaki siasa peke yake!
 
siasa peke yake si kigezo, na biashara peke yake si kigezo, na hata vyote viwili si kigezo (refer DM) cha kuwa rais. Inakuwa vigumu sana kutenganisha wafanyabiashara wakubwa kama kina Mengi na ufisadi na mwenyewe analijua hilo ndio maana hataki kuingia kwenye siasa. Nadhani tunahitaji mtu firm kwenye siasa ambaye si fisadi kwa sasa kuwa rais pasipo asiye mwanasiasa Tanzania ni rahisi sana kungizwa mkenge na watendaji wake wakuu ambao wengi ni wanasiasa. Labda aanze kujenga serikali upyaaaaaaaaaa na kung'oa mizizi yote ya ufisadi (kama itawezekana).
 
Hivi kweli Watanzania wenzangu ni kiongozi gani aliyeko in touch na wananchi ambaye ameshawahi kusema maneno kama haya....?

"I have a dream that one day Tanzania will be free from corruption," alisema Mengi kwa Kiingereza akieleza namna anavyotamani kuiona Tanzania ikiwa taifa lisilo na rushwa siku moja.
 
Hivi kweli Watanzania wenzangu ni kiongozi gani aliyeko in touch na wananchi ambaye ameshawahi kusema maneno kama haya....?

Mbona hayo maneno hata miemi ninayasema almost everyday na nadhani hiyo ni dream ya kila mmoja wetu. Kama Mengi anafaa kuwatumikia wananchi (kama yuko msafi kiasi anachofikiriwa yupo) basi akagombee ubunge, ni nafasi nzuri ya kuwapigania wananchi kuliko hata urais.
 
Mama Mengi amewafanyia watanzania mengi!
Na pengine kuliko wabunge wengi tu! Si majimboni tu..Bali Tanzania nzima!
Na si Tanzania tu
Bali Afrika na Dunia mchango wake uko recognized!
Umesahau hiyo MLK award?
We unaona hao waliopita kati ya hao 8 ni wangapi viongozi na ni wangapi wafanyabiashara ambao wameshawahi kuipokea tuzo hiyo?
Kawawa ni nani?
Ni sifa gani zinazopeleka kupewa hiyo tuzo?
 
Huyu naye ni mfanyabiashara ama bepari?

Press Releases

Mzee Kawawa Receives MLK Award

January 23, 2007
Veteran politician Mzee Rashid Mfaume Kawawa, was on Tuesday January 23, 2007 conferred with the Martin Luther King Jr Drum Major for Justice Award, for his great contribution to Tanzania before and after this country's independence.

The MLK Award was presented to Mzee Kawawa by U.S. Ambassador Michael L. Retzer, after the Minister of State in the President’s Office (Political Affairs and Civil Societies Relations) Hon. Kingunge Ngambale-Mwiru made an introduction of the 2007 Drum Major for Justice Laureate.

A press release from the U.S. Embassy in Dar es Salaam says that Mzee Kawawa’s great contribution was the struggle for independence, as he was the key person who supported Nyerere in the liberation struggle.

Another remarkable achievement was his contribution towards recognizing and supporting peoples’ small groups like Women and Youth associations. He also supported the Tanganyika African National Congress (TANU) activities financially. TANU is the political party that came to win independence in 1961.

The Drum Major for Justice Award is named after Dr. Martin Luther King, Jr. Dr King was a vital figure of the modern era. His lectures and dialogues stirred the concern and sparked the conscience of a generation. The movements and marches he led brought significant changes in the fabric of American life through his courage and selfless devotion. This devotion gave direction to thirteen years of civil rights activities. His charismatic leadership inspired men and women, young and old, in the United States and around the world.

Mzee Kawawa becomes the eighth MLK Drum Major for Justice Laureate since the U.S. Embassy in Dar es Salaam first conferred the award to Justice Sinde Warioba in 1999. The late Mwalimu Julius K. Nyerere was the second laureate the following year posthumously, while there was no laureate in 2001.

In 2002, Hon Francis Nyalali received the award, followed by Professor Geoffrey Mmari and Mama Justa Mwaituka in 2003 and 2004, respectively. Ambassador Gertrude Mongella received the award in 2005, and last year it was conferred to Dr. Salim Ahmed Salim.

Mzee Kawawa believes in the freedom of religious benefits, the power of self reliance and the strength individuals can bring to achieve their development goals. In retirement, he still continues to follow Tanzania’s development, providing important advice where necessary.
 
jmushi1: Mengi anaweza akawa amefanya mazuri mengi kwa nchi yetu na tunahitaji kumthamini kwa yale aliyotenda, lakini kukimbilia kutaka kumpa urais si suluhisho. Bill Gates ni bepari na amesaidia sana nchi ya Marekani na dunia kwa ujumla, lakini humwoni anakimbilia kugombea, ditto for Rupert Murdoch au Donad Trump. Mi nadhani it is healthy to be discussing this lakini mimi ningemshauri huyu mzee abaki kuwa respeted elder and member of the society, he can do much more like this kuliko kama angekuwa rais.
Also kumbuka kwamba utajiri wake alioupata enzi za Mwinyi, and it was not a clear cut path, I do not judge him, but he does have a number of skeletons in his closet, so akitaka kugombea ajitayarishe for those skeletons come flying out.
 
Political situation yetu tuliyonayo hivi sasa ni nani msafi kuliko yeye?

Ni vigezo gani kuwa hawezi kutuongoza?

Je una amini kuwa hana kipaji cha uongozi?

Je hauamini kuwa amekuwa jemedari wetu msitari wa mbele kwenye vita dhidi ya umasikini na UFISADI?

Ni mambo gani yanayomkabili Mtanzania wa kawaida kwenye historia karibu yote ya Taifa?

Bill Gates naye ameshawahi kupata tuzo ya MLK?

Hivi umezisoma sababu zote zilizotumika kuwapa both R.Kawawa na R.Mengi tuzo maarufu ya MLK?
 
Susuviri kwa maoni yangu huyu ni mmojawapo wa watu ambao wanastahili huu mjadala na kwa maoni yangu rahisi kumnadi!
 
Pia kama kuna wale wenye hoja za kuwa ni kwanini R.Mengi hafai basi nao wanakaribishwa bila matusi wala kwenda nje ya hoja.
 
Political situation yetu tuliyonayo hivi sasa ni nani msafi kuliko yeye?

Ni vigezo gani kuwa hawezi kutuongoza?

Je una amini kuwa hana kipaji cha uongozi?

Je hauamini kuwa amekuwa jemedari wetu msitari wa mbele kwenye vita dhidi ya umasikini na UFISADI?

Ni mambo gani yanayomkabili Mtanzania wa kawaida kwenye historia karibu yote ya Taifa?

Bill Gates naye ameshawahi kupata tuzo ya MLK?

Hivi umezisoma sababu zote zilizotumika kuwapa both R.Kawawa na R.Mengi tuzo maarufu ya MLK?

Tuzo ya MLK:
Hii ni tuzo ambayo inatolewa na mara nyingi it has a poltical message from the US govt toward the given country eg in Tanzania. SAS alipopata MLK kulikuwa na timing fulani ukiangalia, ditto for Warioba. Tuzo aliyopewa Mengi ilikuwa ni clear emssage ya US govt na ilikuwa baada ya akina Mwanahalisi kumwagiwa tindikali. In fact ilikuwa ni focal point ya balozi na hata Mengi mwenyewe, yaani freedom of the press. but Mengi is only a recent champion of the fredom of the press maana siku za nyuma na hata leo vyombo vyake vya habari vimekuwa vikibeba CCM na kuwapigia debe akina Jk na wale ambao Mengi sees as useful to him.Kama mfanyabiasahra he is free to do so, but he has not shown good judgement.

Sifa za uongozi:
He is not the principled person kama anavyopenda siku hizi kuonekana, kwani hata This Day ilianzishwa as personal vendetta against Mkapa kutokana na ushindani wa kibiashara. Ni mtu ambaye keeps scores and hii si sifa nzuri kwa mtu ambaye anataka kuwa kiongozi. I think that temperament wise he is not suited for teh job, na pia we need new faces and fresh blood, siyo watu ambao wamekulia kwenye the old system like Mengi.
Just my 2 cents!
 
Unaona ngoma hiyo!?

Alisema mbali ya kuwezesha vyombo vyake vya habari kufanya habari za uchunguzi, balozi huyo alisema Mengi kama Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT), amewezesha hata waandishi walio nje ya vyombo vyake kuibua habari za ufisadi.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Dk. Salim Ahmed Salim, mzee Rashid Mfaume Kawawa, Jaji Joseph Warioba, Idd Simba, Joseph Butiku, Askofu Kakobe, Askofu Method Kilaini, Sheikh Othman Matata na Askofu Alex Malasusa. Mbali ya Mengi, Watanzania wengine waliokwisha kuzawadiwa tuzo hiyo na miaka yao kwenye mabano ni Rashid Kawawa (2007), Salim Ahmed Salim (2006), Gertrude Mongella (2005), Mama Justa Mwaituka (2004), Profesa Geofrey Mmari (2003), Jaji Francis Nyalali (2002), Jaji Joseph Warioba (2001) na Mwalimu Nyerere (2000).

Wana JF mnaona?
 
Na hawa viongozi nao wameshaulizwa mawazo yao?
Ama je kuna anayefikiri kuwa hawataweza kumu endorse?

Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Dk. Salim Ahmed Salim, mzee Rashid Mfaume Kawawa, Jaji Joseph Warioba, Idd Simba, Joseph Butiku, Askofu Kakobe, Askofu Method Kilaini, Sheikh Othman Matata na Askofu Alex Malasusa. Mbali ya Mengi, Watanzania wengine waliokwisha kuzawadiwa tuzo hiyo na miaka yao kwenye mabano ni Rashid Kawawa (2007), Salim Ahmed Salim (2006), Gertrude Mongella (2005), Mama Justa Mwaituka (2004), Profesa Geofrey Mmari (2003), Jaji Francis Nyalali (2002), Jaji Joseph Warioba (2001) na Mwalimu Nyerere (2000).

Haya....Kanyaga twende!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom