R.Mengi for President?

Status
Not open for further replies.
Hujanijibu kuhusu NICO!
Hivi Mkapa angekuwa na roho kama ya Mengi si tungekuwa mbali sana?
NICO ni mkombozi wa rasilimali zetu kuwekwa mikononi mwetu!
Vipi Kiwira?
Richmond?
Niendelee?

Kwa nini umlinganishe Mengi na Mkapa au Lowassa? Kwa nini usijadili mazuri ya Mengi on their own merits bila ya kukimbilia kufanya comparative analysis na vigogo wengine? Mengi is a different breed altogether compared to the later two as he's a capitalist par excellence and not a career politician as the other two are (or have been.) NICO is a business venture and it would be both inappropriate and unfair to expect hard-baked politicians like Mkapa and Low-ass-man to be any of its pioneers.
 
Heshima kwenu wakuu,kwanza nakubali Mengi ni mfanya biashara mkubwa aliye fanikiwa hapa Tz,lakini siungi mkono kwa yeye kuwa Pres hapa Bongo, kwa sababu kwanza ana ukabila mfano mzuri nenda kaangalie pale IPP mahali ambapo yeye ni Mkurugenzi Mtendaji,lakini pamoja na kuwa na mafanikio ktk biashara zake mara kwa mara amekua na migogoro na wafanyakazi wake kuhusu mishahara sasa hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yananifanya nisimkubali
 
Mimi nimeanzisha mjadala tu.
Yeye mwenyewe hajawahi kusema kuwa atagombea urais!
Ni wazo tu ambalo nataka tilijadili and maybe tum convince kama tukikubaliana ili tu muendorse!
Cha muhimu tumpe fair,honest and respecting discussion kwasababu hata yeye ameturespect na kutufanyia mengi wananchi na huku hata yeye akiwa si kiongozi!
Sasa tukiondoa tofauti zetu na kumpa uongozi kwanini asifanye makubwa zaidi kama akipewa ushirikiano?

Kuhusu yeye kuwa CCM hilo siwezi kumsemea.

Kuhusu supporting data nitajitahidi,ila ujue kuwa almost everybody knows what he has done to the community nationwide!

Ok, kwa hiyo huna dataz sio, nimekupata wenye nazo wataziweka hapa. Mzee Mengi kwa kweli anaheshimika, anaogopa kuingia kwenye siasa ili aendelee kuheshinika.

Hivi pamoja na misaada ya chakula anayotoa, kutoa sadaka misikitini na makanisani na mashuleni au mahospitali kama ambavyo hata mimi ninafanya ni kigezo cha kugombea urais? Mengi angeweza pia kujenga barabara hata ile inayoingia pale ipp kuwa ya kiwango cha lami!
 
His long experience and success in doing business in Africa has taken him to participate in a large number of national and international business as well as taking an active interest in private sector development. To this effect, he has been a long-time advocate of promoting good governance in Africa as well as enhancing technical and managerial skills in the private sector, as key mechanisms for improving the business environment and attracting foreign direct investment to the continent. However, as a leading media tycoon, he has also called on the African press not to follow the international media's inclination to portray only the negative aspects and constraints of doing business in Africa, since these only reinforce certain stereotypes, overshadow the business opportunities that exist in the continent and has a detrimental effect on potential foreign investors.
As a leading member of the business community Reginald Mengi has served as Chairman of Tanzania's National Board of Business Accountants and Auditors, of Tanzania's Chapter of the International Chamber of Commerce (ICC), and of the Tanzanian Chapter of the Commonwealth Press Union (PCU). He has also participated in several organised under the (NEPAD), met with various and Latin American leaders and is a member of the Board of Management of the African Commonwealth Business Council (CBC).

Personal life.....??!
 
Mama huyu jamaa anawapandishia mawaziri wazembe bila kujali!

Huyu ni rafiki wa fisadi kwa maoni yako?

Na kuhusu NICO no hajaianzisha mwenyewe..Kama vile ambavyo atahitaji msaada kwenye kuongoza![/QUOTE]

Je kuwapandishia mawaziri inatosha kuwa na sifa za uraisi, hata Lowassa alikuwa akiwapandishia mawairi bila kujali!

Mengi anaweza kuwa katika mafisadi kwa kuendelea kwake kukaa sisiemu na kutoa michango ili chama hicho kiendelee kuwa madarakani kupitia ITV, alitoa mchango mkubwa sana 2000 na pia 2005. Chama cha Mafisadi kinawalinda sana wafanyabiashara, je yeye tutamtoaje katika hilo kundi linalolindwa na mafisadi?

Na kuhusu NICO, unaweza kuwataja hao walionzisha nae (Major share holders)?
 
His long experience and success in doing business in Africa has taken him to participate in a large number of national and international business as well as taking an active interest in private sector development. To this effect, he has been a long-time advocate of promoting good governance in Africa as well as enhancing technical and managerial skills in the private sector, as key mechanisms for improving the business environment and attracting foreign direct investment to the continent. However, as a leading media tycoon, he has also called on the African press not to follow the international media's inclination to portray only the negative aspects and constraints of doing business in Africa, since these only reinforce certain stereotypes, overshadow the business opportunities that exist in the continent and has a detrimental effect on potential foreign investors.
As a leading member of the business community Reginald Mengi has served as Chairman of Tanzania's National Board of Business Accountants and Auditors, of Tanzania's Chapter of the International Chamber of Commerce (ICC), and of the Tanzanian Chapter of the Commonwealth Press Union (PCU). He has also participated in several organised under the (NEPAD), met with various and Latin American leaders and is a member of the Board of Management of the African Commonwealth Business Council (CBC).

Personal life.....??!

Je hizi ndizo sifa anazotakiwa kuwa nazo mgombea wa urais? na je Tanzania hakuna aliyeweza kuvunja record ya haya uliyowaweka hapo juu ?
 
Marekani yampa tuzo Mengi

blank.gif
blank.gif

1-mengi.jpg
blank.gif
Reginald Mengi​
h.sep4.gif

na Martin Malera

MWENYEKITI wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amepokea rasmi tuzo inayoheshimika ya Martin Luther King.
Mengi ambaye anakuwa Mtanzania wa nane kutwaa tuzo hiyo alikabidhiwa tuzo yake nq Balozi wa Marekani hapa nchini, Mark Green.
Taarifa rasmi ya iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na ubalozi wa Marekani hapa nchini inaeleza kwamba, Mengi alitwaa tuzo hiyo kutokana na kutoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya rushwa akitumia vyombo vya habari anavyomiliki.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mengi alisema tangu alipoanzisha magazeti mawili ya This Day na Kulikoni yanayoandika habari za uchunguzi kuhjusu masuala mbalimbali yanayohusu rushwa wamekuwa wakipokea vitisho vya aina tofauti.
Alisema ingawa vitisho hivyo vilikwenda sambamba na kupoteza maisha kwa baadhi ya wafanyakazi, hawajawahi kutishika na akawataka waandishi wa habari kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi nchini.
Sambamba na hilo, Mengi alisema kutokana na mchango mkubwa wa vyombo vya habari kufichua habari za ufisadi na kwa ushirikiano anaouonyesha Rais Jakaya Kikwete, anaamini siku moja Tanzania itaondokana na tatizo la rushwa.
"I have a dream that one day Tanzania will be free from corruption," alisema Mengi kwa Kiingereza akieleza namna anavyotamani kuiona Tanzania ikiwa taifa lisilo na rushwa siku moja.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, Mengi alisema kazi ya kuanzisha vyombo hivyo maalumu kwa ajili ya kuibua ufisadi ilikuwa ngumu kiasi cha kujijengea maadui mbalimbali waliochukizwa na harakati za magazaeti hayo kuibua maovu katika jamii.
"Lakini tulibaki imara, tukaendelea na kazi bila kuogopa vitisho na tunaamini jamii itaelewa jukumu letu kama kioo chao ambacho watakitunza badala ya kukivunja kwa sababu ya kuibua maovu," alisema Mengi.
Mengi alisema athari za rushwa ni kubwa na mbaya, bila kujali ukubwa wake, kwani inaondoa haki, uhuru na kuleta ubaguzi, mambo ambayo Martin Luther King, mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu wa Marekani aliyepoteza maisha akipigania haki za watu weusi nchini humo, alikuwa akipambana nayo.
"Kwa namna ya pekee kabisa, napenda kuishukuru Serikali ya Marekani kwa kunipa tuzo hii kubwa na ya hshima duniani. Hii imenipa nguvu na hamasa ya kupambana na ufisadi na maovu mengine katika jamii.
"Hata hivyo tuzo hii si yangu, bali ni kwa ajili ya waandishi wa habari wanaoibua taarifa za ufisadi," alisema Mengi.
Mengi pia alisema tuzo hiyo anaitoa kwa Rais mstaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Rais Jakaya Kikwete, ambao alisema katika utawala wao wameonyesha dhamira ya kweli ya kupambana na rushwa.
Akizungumza nje ya ukumbi huo, Mengi alitoa changamoto kwa wamiliki wengine wa vyombo vya habari kuacha tabia ya kuingilia kazi za waandishi kwa kuwachagulia habari za kuandika na kuwawezesha waweze kufanya kazi za habari za uchunguzi kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Balozi Green alisema vyombo vya habari duniani kote ni njia pekee ya kupambana na vitendo vya ufisadi na ndiyo maana katika baadhi ya nchi hakuna uhuru kamili wa vyombo vya habari.
"Hapa Tanzania nafurahi kusema kuwa kuna uhuru mkubwa wa vyombo vya habari na Serikali ya Marekani itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wanaoandika habari za uchunguzi," alisema Balozi Green.
Akimzungumzia Mengi, Balozi Green alisema hakuna shujaa aliyeacha vyombo vyake vya habari kuwa huru kufanya kazi za uchunguzi kama Mengi.
"Kutokana na ushujaa wake, mwaka huu hatukusita kabisa kutoa tuzo hiyo ya heshima ya Martin Luther King kwa Mengi, kwa kuwezesha vyombo vyake vya habari kufanya kazi nzuri ya habari za uchunguzi kuhusiana na rushwa…," alisema Balozi Green.
Alisema mbali ya kuwezesha vyombo vyake vya habari kufanya habari za uchunguzi, balozi huyo alisema Mengi kama Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT), amewezesha hata waandishi walio nje ya vyombo vyake kuibua habari za ufisadi.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Dk. Salim Ahmed Salim, mzee Rashid Mfaume Kawawa, Jaji Joseph Warioba, Idd Simba, Joseph Butiku, Askofu Kakobe, Askofu Method Kilaini, Sheikh Othman Matata na Askofu Alex Malasusa. Mbali ya Mengi, Watanzania wengine waliokwisha kuzawadiwa tuzo hiyo na miaka yao kwenye mabano ni Rashid Kawawa (2007), Salim Ahmed Salim (2006), Gertrude Mongella (2005), Mama Justa Mwaituka (2004), Profesa Geofrey Mmari (2003), Jaji Francis Nyalali (2002), Jaji Joseph Warioba (2001) na Mwalimu Nyerere (2000).
 
Wenye macho na waone!
Mimi sitaki wenye chuki wachangie mada!
Hoja!
 
Je hiyo tuzo inamfanya awe eligible kugombea urais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania?
 
His long experience and success in doing business in Africa has taken him to participate in a large number of national and international business as well as taking an active interest in private sector development. To this effect, he has been a long-time advocate of promoting good governance in Africa as well as enhancing technical and managerial skills in the private sector, as key mechanisms for improving the business environment and attracting foreign direct investment to the continent. However, as a leading media tycoon, he has also called on the African press not to follow the international media's inclination to portray only the negative aspects and constraints of doing business in Africa, since these only reinforce certain stereotypes, overshadow the business opportunities that exist in the continent and has a detrimental effect on potential foreign investors.
As a leading member of the business community Reginald Mengi has served as Chairman of Tanzania's National Board of Business Accountants and Auditors, of Tanzania's Chapter of the International Chamber of Commerce (ICC), and of the Tanzanian Chapter of the Commonwealth Press Union (PCU). He has also participated in several organised under the (NEPAD), met with various and Latin American leaders and is a member of the Board of Management of the African Commonwealth Business Council (CBC).

Personal life.....??!

Usituletee copy-and-paste work! Wacha kabisa hiyoo! Mtu mwenye kumiliki almost all major media outlets in the country na isitoshe mapesa in billions hatashindwa kueneza mazuri na sifa zake dunia nzima. Mengi kufungua kliniki ya wajawazito sehemu fulani au kutoa laki mbili-tatu kwa chama cha Walemavu siyo big-deal kwa mtu mwenye uwezo wa kipesa kama yeye. Ila sema unique and unlimited access aliyo naya kwenye printing press na TV stations ndizo zinakufanya mtu kama jmushi1 kupumbazika kwa vile hutangaza "mazuri" tu anayoyafanya (kusaidia laki mbili hapa, laki tano pale) kwenye vyombo vyake vya habari. Kwa mtu mwenye uwezo kama wake ningetegema angejeng refferal hospitali kubwa na ya kisasa kama anavyofanya Dikembe Mutombo kwao Kongo au University kubwa kushinda UDSM siyo kujitafutia sifa kwa kujitangaza kwenye magazeti na luninga zake kila anapogawa laki 3 kwa madrasa fulani Zanzibar au shule ya vidudu Pemba.
 
Je hiyo tuzo inamfanya awe eligible kugombea urais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania?

Kama wewe hujui maana ya rushwa ni ufisadi then sina haja ya kuendelea kubishana!
Yes anafaa kuwa raisi kwasababu hizo!
Sababu unazozitoa wewe ni barabara ya IPP?
 
Usituletee copy-and-paste work! Wacha kabisa hiyoo! Mtu mwenye kumiliki almost all major media outlets in the country na isitoshe mapesa in billions hatashindwa kueneza mazuri na sifa zake dunia nzima. Mengi kufungua kliniki ya wajawazito sehemu fulani au kutoa laki mbili-tatu kwa chama cha Walemavu siyo big-deal kwa mtu mwenye uwezo wa kipesa kama yeye. Ila sema unique and unlimited access aliyo naya kwenye printing press na TV stations ndizo zinakufanya mtu kama jmushi1 kupumbazika kwa vile hutangaza "mazuri" tu anayoyafanya (kusaidia laki mbili hapa, laki tano pale) kwenye vyombo vyake vya habari. Kwa mtu mwenye uwezo kama wake ningetegema angejeng refferal hospitali kubwa na ya kisasa au University kubwa kushinda UDSM siyo kujitafutia sifa kwa kujitangaza kwenye magazeti na luninga zake kila anapogawa laki 3 kwa madrasa fulani Zanzibar au shule ya vidudu Pemba.

Nilete nini sasa?
Sema kama si valid niondoe!
Nasema kama mkiishiwa na hoja kipeni kitu msilete usiku!
Kwani umeisoma hiyo habari hapo juu ama unaanza kuona wasiwasi kuwa hoja unazidiwa?
Kwani huoni kuwa alikuwa akifanya jambo la hatari kuukemea ufisadi hadharani?
 
Kama wewe hujui maana ya rushwa ni ufisadi then sina haja ya kendelea kubishana!
Yes anafaa kuwa raisi kwasababu hizo!
Sababu unazozitoa wewe ni barabara ya IPP?

Sijabisha ila nimekuuliza maswali kadhaa ambayo hujajibu hata moja! waweza kusema tu huna jibu, nikaacha kuuliza na wewe ukaendelea kujenga hoja.
 
Talkin about copy n paste!
Waka mslete usiku hapa kila mtu ni Mtanzania!
Yani kuna watu wana chuki za nguvu hadi inaogopesha!
Sasa kama hali ni hii tutakuwa na umoja kama Watanzania ama tusahahu?!
 
Sijabisha ila nimekuuliza maswali kadhaa ambayo hujajibu hata moja! waweza kusema tu huna jibu, nikaacha kuuliza na wewe ukaendelea kujenga hoja.
Ndio sina jibu!
Na nimeshasikia maoni yako!
Ila kama hupendi kuchangia una demokrasia ya kujiamulia zaidi ya just kubishana!
 
Ndio sina jibu!
Na nimeshasikia maoni yako!
Ila kama hupendi kuchangia una demokrasia ya kujiamulia zaidi ya just kubishana![/QUOTE

kwi kwi kwi, kumbe huo ndio ubishi eeh, good to let me know.
 
Naomba nikushauri mushi: usitumie nguvu sana kuendeleza huu mjadala. Watu wanamfahamu sana mengi. Mimi namfahamu kidogop kwa sababu nimewahi kufanya kazi katika moja ya makampuni yake na kwa kweli nilikuwa karibu yake kidogo. Kwa nilivyomuona, nadhani ni bora aendelee tu na biashara, hiyo nafasi uliyomkadiria ni ya juu sana kwake. Asante
 
Unakaribishwa Mpita Njia.
Naomba unieleze kuwa ni kivipi nafasi niliyomkadiria ni ya juu ili na mimi niweze kujua namna ya kujibu.
Pia naamini kuwa kuna watu wanaomfahamu R.Mengi personally na mimi siko hapa kumpigia debe bali kusisitizia umuhimu wa kumjadili base on character na si vinginevyo!
 
Nilivyomuona mimi mengi ni mfanya biashara per se mwenye sifa zote za ubepari. Narudia huo ni muono wangu. Sina shida na yeye kuwa bepari. Na ndio maana nikaona ni bora aendelee kwenye channel ya biashara. Nilivyompima nilimuona ana uwezo mkubwa wa kumanage biashara kuliko watu. Ndio maana nina wasiwasi iwapo ataweza kutumanage kama akiwa rais
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom