Akili Kichwani
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 1,508
- 216
Mungu hahusiki jamani, hebu someni vizuri kitabu cha Ayub mtaelewa alisema maneno hayo bila ujuzi bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea kati ya Mungu na Shetani na isitoshe katika Ayub sura za 42 alitengua usemi huo na yale yote akidhani Mungu ndiye alikuwa akimtendea. Wachungaji walitudanganya, tukafikiri Mungu anahusika katika vifo vinavyotokea. Wengine wanasema "Tulimpenda marehemu lakini Mungu kampenda sana au Mungu anavuna alichopanda. Lakini unaweza kuangalia matokeo ya vifo kwa mfano. Unaaenda kutembeza umalaya unakumbana na virus vya ukimwi baada ya muda unakufa, Mungu ndiye aliyekutuma ufanye umalaya??? si alisema mzinzi hataurithi ufalme wa Mungu sasa atakutumaje. Jambo tunapaswa kujifunza ni kwamba Mungu karuhusu kifo cha mwanadamu lakini hasababishi kifo hicho, kuna tofauti kati ya kurusu na kusababisha. Ukitaka maelezo zaidi soma kitabu cha Mhubiri.
Hivyo usemi huo tunaendelea kuutumia kimakosa. Mimi namuomba Mungu aipe nguvu za familia ya mzee Remmy kukabiliana na msiba huu kwani ni kipindi kigumu kwao cha kumpoteza mpendwa wao. Na aiangalie familia hiyo ili iendelee kupata mahitaji yake ya kila siku. Amen.
ndugu muacici, nina neno kidogo na ile comment ya kitabu cha ayubu. tafadhari zingatia kuwa kitabu cha ayubu si cha historia au mambo ya nyakati (matukio/chronicles).......... ni kitabu cha utenzi kinachokusudia kuibua asili, sifa na tabia ya Mungu.......... simulizi la shetani kama ulivyolinukuu liko katika prologe ya hicho kitabu (3-42:6). ........ na kibwagizo chake kiko kwenye epilogue yake (42:7 hadi mwisho)............ ila maudhui ya kitabu chenyewe yako sura za 3-42:6 na yameandikwa katika mtindo wa utenzi unawahusu ayubu na marafiki zake watatu (elifaaz, zofari na bildad) mwishonimwishoni anaibuka kijana mmoja mdogo lakini mwenye hekkima kubwa (elihu) kushinda hata ya ayubu na rafiki zake wote. anaongea mambo yanayokaribia kufanana na ya Mungu mwenyewe na hatimaye anasababisha ayubu akiri alipopotoka na kutubu.......... tafadhari soma taratibu na Mungu akusaidie kuelewa nasema nini na kama utapata tatizo, nitafurahi kukusaidia........... unaweza kutumia PM........... ubarikiwe..........
RIP Dr Remmy..............