R.I.P. Dr. Remmy Ongara

......RIP Remmy Ongala, kweli kifo hakina huruma.......Bwana alitoa na ametwaa.
 
Bwana ametoa,bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!!

Mungu hahusiki jamani, hebu someni vizuri kitabu cha Ayub mtaelewa alisema maneno hayo bila ujuzi bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea kati ya Mungu na Shetani na isitoshe katika Ayub sura za 42 alitengua usemi huo na yale yote akidhani Mungu ndiye alikuwa akimtendea. Wachungaji walitudanganya, tukafikiri Mungu anahusika katika vifo vinavyotokea. Wengine wanasema "Tulimpenda marehemu lakini Mungu kampenda sana au Mungu anavuna alichopanda. Lakini unaweza kuangalia matokeo ya vifo kwa mfano. Unaaenda kutembeza umalaya unakumbana na virus vya ukimwi baada ya muda unakufa, Mungu ndiye aliyekutuma ufanye umalaya??? si alisema mzinzi hataurithi ufalme wa Mungu sasa atakutumaje. Jambo tunapaswa kujifunza ni kwamba Mungu karuhusu kifo cha mwanadamu lakini hasababishi kifo hicho, kuna tofauti kati ya kurusu na kusababisha. Ukitaka maelezo zaidi soma kitabu cha Mhubiri.

Hivyo usemi huo tunaendelea kuutumia kimakosa. Mimi namuomba Mungu aipe nguvu za familia ya mzee Remmy kukabiliana na msiba huu kwani ni kipindi kigumu kwao cha kumpoteza mpendwa wao. Na aiangalie familia hiyo ili iendelee kupata mahitaji yake ya kila siku. Amen.
 
RIP Dr Remmy, nilipenda sana wimbo wake mmoja aliokuwa anasema Watu wameiba wanajulikana,polisi wapo, mahakama zipo, inaundwa tume ya nini?
 
Du! si bado kama wiki mbili tu mwaka mpya uingie!!
Kweli life is not fair.
Nakumbuka kibao chake cha "SIKU YA KUFA"
rip Dr.
 
nimesikitika sana.. jana nilkuwa napiga nyimbo zake huyu jamaa...narudi nyumbani....kifo....na nyingine kibao..

sikujua kama nilikuwa naomboleza..........rip
 
RIP Dr. Remmy Ongalla

Wakuu hivi udocta (DR) wake ni kama u-Professa wa maji marefu, au ni kama wa Dr. Kikwete au ni PhD haswa wa xul au Dr. wa Kitabibu!
 
Poleni sana familia ya Dr Remmy... Soote tunaelekea huko, tofauti ya siku tu. ''Kila nafsi itaonja umauti''
 
nimesikitika sana......... hapa nimeweka kibao chake cha kipenda roho
 
Back
Top Bottom