R chuga tujulisheni

sugi

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
1,392
292
wazee wa Arusha hebu tujulisheni,nimesikia kuwa madereva wamegoma asubuhi hii,mwenye details naomba atujulishe
 
migomo imezidi....tutafute njia nyingine za kufikisha malalamiko/kero/hoja/manung'uniko yetu kwa wahusika....! migomo inaathiri sana wasiohusika , kwa lugha nyingine MIGOMO NI UGAIDI kwani ugaidi huathiri kwa kiwango kikubwa zaidi wasiohusika kuliko wahusika
 
Kitendo cha madreva kugoma, ni atua nzuri inayoonyesha wametambua haki zao sasa kwa mujibu wa sheria za nchini zinavyotaka.

Madreva wamekuwa wakifanya kazi kwenye mazingira magumu kulingana na manyanyaso wanayopata kutoka kwa waajiri wao, wengi wanalipwa mishahara mibovu, mikataba ya kazi hawana, bima ya afya hawana, hata likizo hawapewi; sasa madreva baada ya kuligundua hilo hasa mara baada ya Elimu nzuri inayotolewa na Maafisa Kazi kutoka Wizara ya Kazi na Ajira juu ya sheria za kazi, na wao kutambua ni wapi wanapunjwa na kwa vile waajiri hawataki kubadilika basi matokeo yake ni Kugoma kwani ni Haki yao kisheria.
 
Back
Top Bottom