Queen Fifi : Mtangazaji bora kabisa wa kike wa wakati huu!

GadoTz

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
350
567
Kwenye show za radio, haswa vipindi vya kizazi kipya kumekuwa na pengo kwa watangazaji wa kike wenye uwezo na vipaji vya kipekee. Hii imekuwa kwa muda mrefu .

Mtangazaji wa radio asiye kuwa na mfano Salama Jabir baada ya kutoka kwenye radio, kukawa na pengo kubwa sana kwa upande wa mabinti. Baada ya Salama kuacha kutangaza radio akaibuka Dj Fetty kujaribu kukaba ilo gap ambaye kwa kweli alijitahidi sana na alitendea haki mic na kuwa mtangazaji mzuri sana.

Baada ya Fetty kukaa pembeni na kuacha utangazaji.

Nimeona kitu kutoka kwa mtangazaji mgeni yupo anatangaza East Africa radio kipindi cha The Cruise. Huyu binti yupo sawa sawa mno, ana kipaji nimekisia sijaona kwa watangazaji wote wa kike baada ya Salama J. Nimemmsikiliza mara mbili ila nimeona kipaji na package isiyo ya kawaida.

Japo sijajua history yake alianzia kutangaza wapi! Naamini ni hazina kubwa imekuja kwenye tasnia ya burudani kwa ujumla.
 
1474578567578.jpg
huyu ndiye Frida Amani
 
Namtafuta Dj Sinyorita yuko wapi?mwenye noyake anipm
Huyu nae tunda la earadio tena amshukuru sana sam misago kwa kumpa airtime ya kutosha kwenye the cruise na fnl.....wazee wa nyakunyaku wakamnyakua yeye na mamibby
 
Back
Top Bottom