Quality Plaza yaungua?

kiraia

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
1,716
999
Kuna habari zimetangazwa na Redio one kuwa Jengo la Quality Plaza (nyerere Road) linaungua, kwa wale waloko eneo la tukio tunaomba mtuhabarishe.

Mod Naomba uihamishe hii baada ya 2 hours
 
Manji anachoma moto apate pesa za kuwapa CCM kwa ajili ya uchaguzi. Tehetehetehetehetehetehe
 
likiungua likaisha hapo fresh tuu.............walio karibu waombe walio karibu wasisogelee tukaanza kuhesabu marehemu
 
Ukiona hivyo wajanja wa mji wameshachukuwa chao mapema, sasa wanapoteza ushahidi,habari ndiyo hii wakale wapi? Isitoshe jengo lina bima watalipwa maana ndo maisha ya ki-tz ukikichoka unakitia moto, then unalipwa kingine ila lazima utoe %
 
Kuna habari zimetangazwa na Redio one kuwa Jengo la Quality Plaza (nyerere Road) linaungua, kwa wale waloko eneo la tukio tunaomba mtuhabarishe.

Mod Naomba uihamishe hii baada ya 2 hours

Kuna tawi la CRDB pale! Mie mteja wa hiyo benkiiiiii!
 
Ni kweli linaungua VIKOSI VYA ZIMA MOTO VINAANGAIKA KUZIMA, ZIPATI PICHA ZILE BANK,
 
kama kawa magazeti yataandika kuwa magari ya fire yalifika bila kuwa na maji
 
Kuna ofisi ya rafiki yangu Mkuki na Nyota Publishers mule ndani pia just next door from crdb.
What a lose.
OMG
 
Mmmmh ni moto wa kawaida au ndo ule wa kupoteza ushahidi? Poleni wazalendo wa kweli mliokumbwa na janga hili
 
Jengo si la Manji tena, sehemu kubwa ni la PSPF- Shirika la serikali, na waliomo mle ndani ya jengo ni wafanyabiashara mbalimbali wazalendo wazuri tu watazania. Inasikitisha kushabikia kuungua moto kwa jengo. Ni muhimu kutofautisha umiliki kwa maana ya kuwa na haki na mali fulani na Mali yenyewe.

Mimi niko radhi tuibiwe kama tunavyoibiwa kila kukicha kwenye migodi na makampuni kama ya bia, mabenki nk, ilmradi fedha hio isitoke nje ya mipaka ya tanzania. Wewe iba lakini pesa ibaki Tz kwa maana ya kujenga majengo kama hayo ya Quality Plaza na mengine. Maana hata Manji akifa au akikimbia nchi bado tunakuwa nayo. Ndio maana nafikiri si sahihi hata kidogo kwa mlioshabikia mali kuungua! Ni mali yetu haiondesheki ile ni yetu. Atakapochukuwa nchi jemadari, atasawazisha mapato yote yatokanayo na mali (assets) kama hizi. Lakini kama watakuwa wamekimbiza huko Jersey sio rahisi!

Hivi mnajua ni Bongo tu unaweza ukaingia kwenye Bureau de Change, ukatoa Dola hata 50,000 ukauza na wala usiulizwe tena wewe ni Mtz, na ukienda na vijisenti vyko ni Bongo tu unaweza kununua any amount of dola bila kuulizwa chochote, na bila kupewakaratasi lolote! Ndio hivyo! Ndiyo maana nchi inaliwa. Tujipe pole kwa kuunguliwa mali yetu pale Nyerere Road. Tutumaini jeshi letu la uokozi wa moto limenusuru mali na maisha!
 
Mbona matukio ya kuungua majengo ya meshamiri sana kipindi hiki? Utasikia 'tumeunda tume ya uchunguzi ili kujua chanzo cha moto' na mwisho wa siku hakuna report ya kueleweka na hakuna njia mbadala inayopatikana kukabiliana na haya majanga ya moto.
 
Back
Top Bottom