Quality Centre kuna wizi wa sumu

mbongopopo

JF-Expert Member
Jan 24, 2008
1,611
759
wadau nimesikia hapa Dar kuna matatizo sana yanakuwa makubwa, kuna watu ukienda kunywa vinywaji hasa hii ilitokea Quality Centre ni kwamba unawekewa sumu katika kinywaji

namba moja mume makini mkiwa mnaletewa vinywaji popote ulipo hakikisha haijafunguliwa kabla ya kuja mezani kwako

sasa ndugu ya rafiki yangu aenisumulia kuwa kuwa jamaa yake alienda kunywa na marafiki, wanaletewa vinywaji na mara kuna watu hawawafahamu walikuja kaa karibu nao pia, ila anauakika hakunyanyuka kuacha kinywaji na ni kinywaji alichokunya aliondoka kama mtu aliyelewa sanaaaaaa akijisikia tumbo linauma, huko mbeleni alitoka kwenye gari nakuanguka na kuzimia kupelekwa hospitali ikawa ni sumu, wakaiwahi kumutibu na kumpa matibabu sasa imagine usipowahiwa ukidhani ni kuchoka au malaria etc

sasa alianza kujisikia kalewa kupita kwa drink isiyo na pombe kali moja tu aliyokunywa, akaibiwa kila kitu ndani ya pochi as alikuwa kama mtu aliyelewa na kutokujijua cha hatari sasa kumbe aliwekewa sumu bora ingekuwa kitu cha haraka waibe waondoke

naombeni muwashauri ndugu zenu na marafiki wawe makini kila mahala waendepo

nashukuru mie hata nikinyanyuka kwenda msalani nikirudi labda awe ndugu yangu nitaweka imani ila mwingine yeyote naiacha na kununua ingine

hii kitu ni hatari sana sasa
 
INgawa nimepata shida kuielewa thread lakini hatimaye nimeielewa.
Hili si tatizo la Qality centre au mahali fulani, ni aina ya uhalifu unaibukia dar, popote pale wanapopata nafasi hawa wahalifu wanatekeleza kazi yao
 
Du hii investment mpya mshaianzishia zengwe kweli bongo noma..

ni bora watu wajue maana wengi wanaona ni sehemu mpya wanaenda wakidhani kumekucha, tabu kubwa pia ni lazima wafanyakazi wa hizo sehemu wanajua kinachoendelea wao wanachosubiri ni kukatiwa pesa share yao na kula mbele
 
INgawa nimepata shida kuielewa thread lakini hatimaye nimeielewa.
Hili si tatizo la Qality centre au mahali fulani, ni aina ya uhalifu unaibukia dar, popote pale wanapopata nafasi hawa wahalifu wanatekeleza kazi yao

mie nimejaribu kuonya kuwa kama pale inatokea basi wezi hawa au style ya kuibiwa hivi ipo sehemu nyingi, wanaoleta kinywaji mezani kwako ni ma wahudumu sasa inakuwaje pombe yako ina sumu na muhudumu kakufungulia hapo ulipo au kujifanya kafungua wakati ilishafunguliwa b4 haujaletewa.

sasa mfano nilionao ni wa hapo tu QC sina kwingine ila nimeandika kusema kuwa watu muwe makini maana inaweza tokea popote.

Nasema imetokea QC na ndio maana nimiandika hapo. NI QC sumu alipowekewa mtu usinibadilishie maneno hapa ni QC kama kuna kwingine haya semeni

TABU WABONGO MKIONA SEHEMU MPYA MNADHANI NI DHAHABU ISIKOSOLEWE PHWUUUU
 
INgawa nimepata shida kuielewa thread lakini hatimaye nimeielewa.
Hili si tatizo la Qality centre au mahali fulani, ni aina ya uhalifu unaibukia dar, popote pale wanapopata nafasi hawa wahalifu wanatekeleza kazi yao

Huo ndio ukweli. Ni lazima tuwe waangalifu, sio Quality Center peke yake. Uhalifu unakua kadri hela ya bongo tambarale inavyozidi kuota mbawa
 
Muandika thread embu uwe una weka vituo na ku phrase vizuri sentesi zako. Back to the point-hiyo kitu inaitwa Dorolee. Huwa wanawekewa watu wanaokunywa ovyo na kujisahau na kuacha chupa au glass zao mezani bila uangalizi wakienda toilet au kucheza mziki. Baadhi ya Wahudumu wa bars pia huwa wanahusika Inapatikana zaidi maeneo ya unywaji ya Wilaya ya Kinondoni,wilaya ya Ilala kidogo hasa Ilala Kariakoo na Buguruni. Wilaya ya Temeke hasa maeneo ya Temeke na Tandika. Take care!
 
Nilivyosoma heading nikastuka.
Wizi wa sumu!! yaani wezi wanaiba sumu!!
Kumbe ni wizi wa kutumia sumu!! Asante sana mdau post imetusaidia walevi.
 
Hii kitu miaka ya hapo nyuma ilikuwa inafanyika sana kwa mabasi ya safari ndefu. Nadhani watu walistukia sasa imehamia kwenye mabaa.
Ni kweli tunapaswa kuwa waangalifu sana na vinywaji vyetu. Usimwamini mtu yeyeto ambaye humjui.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom