Punda hataki aitwe punda

Mabel

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,273
678
Siku moja PUNDA alikutana na Simba faragha kutoa malalamiko yake kuhusiana na wanyama wengine juu yake, mazungumzo yalikuwa hivi:

Punda: Wenzangu wanadai eti mimi sio MWEREVU ndio maana wananiita PUNDA!
Simba: Sasa wewe hutaki jina hilo na unataka nini?

Punda: Nataka uwakataze wasiniite tena jina hilo kwani mimi ni MWEREVU sana!
Simba: Sawa mimi nitawakataza ila kabla nataka nikupe kamtihani kadogo ili nihakikishe kweli wewe ni MWEREVU au la, uko tayari?

Punda: Ndiyo!
Simba: Sasa nenda nyumbani kwangu ukaniangalie kama nipo halafu urudi kunipa jibu

Basi PUNDA akatimua mbio kuelekea nyumbani kwa mfalume wa pori kumangalia kama yupo nyumbani kwake na punde akarudi

Simba: Umenikuta nipo nyumbani kwangu?
Punda: Aisee bwana sijakukuta, haupo!

Simba: Wewe ni punda na utaendelea kuitwa PUNDA daima, potea hapa!

Basi PUNDA akaondoka kwa unyonge
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom