TANZIA: Msanii wa Siri za Familia Mr. Benson Afariki Dunia

Jul 14, 2008
1,820
1,031
Msanii wa Maigizo Haji Jumbe ambaye amekuwa akiigiza kama Mr. Benson katika Tamthilia ya SIRI ZA FAMILIA inayotengenezwa na JASONS PRODUCTIONS na kurushwa na EATV kila Jumatatu hadi Alhamisi saa 12.30 jioni amefariki leo Jumatatu tarehe 24 October 2016 katika Hospitali ya Kinondoni. Marehemu amefariki ghafla akusumbuliwa na Tumbo.

Mazishi yatafanyika Jumanne Tarehe 25 October 2016 Saa 9 Alasiri Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Mr. Benson ameigiza kama Mume aliyesalitiwa na Mke wake. Aliamini kuwa ana mtoto mkubwa kumbe mke wake alimsaliti na rafiki yake.

INALILAHI WAHINALILAHI ROJIUN
 
Duuuuuh! Kweli tumwombe mungu kila wakati,huyu jamaa(haji jumbe) alikuwa ni wa kipekee sana! Bwana alitoa,bwana ametwaa! Jina lake libarikiwe! Mungu awafanyiwe wepesi ndgu na watoto(familia yake) aliyoiacha!!
 
Attachments

  • 14533492_202693796817510_3862995359567446016_n.jpg
    14533492_202693796817510_3862995359567446016_n.jpg
    27.2 KB · Views: 209
Duuuuuh! Kweli tumwombe mungu kila wakati,huyu jamaa(haji jumbe) alikuwa ni wa kipekee sana! Bwana alitoa,bwana ametwaa! Jina lake libarikiwe! Mungu awafanyiwe wepesi ndgu na watoto(familia yake) aliyoiacha!!
Mungu wangu jamani kumbe Ni huyu, Mungu Baba tusamehe makosa yetu
 
Innallillah wainna illah raji'un,

Daah nimeumizwa sana na kifo cha ghafla, ndugu zangu kifo kipo tunatembea nacho siku zote, siku tu ndio hatujui lini,

Tuhimizane mema na kukatazana mabaya ili huko tuendako tuwe na jambo la kujitetea.

Kifo ni mawaidha tosha kwa sie tuliobakia, ndugu yetu hakujua kama ataiacha dunia na vilivyomo kwa muda mchache tu,
Je mimi na wewe wajua mwisho wetu ukoje??

Tafakari, chukua hatua sasa.
 
Mungu aiweke roho ya marehemu pahali panapostahili... Amen.

Mkuu Superman Weka Picha Mkuu tumtambue hii kitu sijaicheki kitambo sana.. na This Monday mida ya mchana nimemuona Dayana akikatiza mitaa ya town na kicheni chake mguu wa Kulia slip na urefu wa kati ila on tv anamvuto zaidi... Pole sana Dayana kwa Kufiwa
 
Innallillah wainna illah raji'un,

Daah nimeumizwa sana na kifo cha ghafla, ndugu zangu kifo kipo tunatembea nacho siku zote, siku tu ndio hatujui lini,

Tuhimizane mema na kukatazana mabaya ili huko tuendako tuwe na jambo la kujitetea.

Kifo ni mawaidha tosha kwa sie tuliobakia, ndugu yetu hakujua kama ataiacha dunia na vilivyomo kwa muda mchache tu,
Je mimi na wewe wajua mwisho wetu ukoje??

Tafakari, chukua hatua sasa.
Ujumbe mzuri. Kifo ni muaidha bora kabisa
 
Back
Top Bottom