Pumba za mpunga

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,064
Nipo katika eneo ilinalolimwa mpunga sana na kuna mashine mpya za kichina mabazo sio zinakoboa mpunga ila zinamenya!!

Pumba zinazotokana na kumenywa kwa mpunga zimelundikana sana na nia yangu ni kutafuta ushauri kuhusu kuzigeuza kuwa kuni.

Je, kuna teknoljia ya kuweza ku press na kutengeneza kuni, nijuzeni ndugu zangu.
 
Waone SIDO nenda kwa maonyesho ya nane nane watakupa ushauri,pia jaribu tembelea UDSM-nadhani na wao wanaeeza wakawa na utaalam
 
Hongera sana kwa kuliona hilo. Kwenye punga kuna vitu vitatu:

1. Mchele
2. Pumba kama mapepe (rice husks)
3. Pumba laini (rice pollishing)

Pumba laini yaaani (rice polishing) ni chakula cha mifugo kizuri kuliko hata
pumba za mahindi.
Swali. UNATAKA UTUMIE ZIPI MKUU?

PUMBA ZA MAPEPE(RICE HUSKS)
unaweza kuchomea hata tofali za udongo.
uchaguzi ni wako.
ahsante.
 
ushauri ndo huo umepewa...... sina la ziada zaidi ya kukukazania usiiweke pending hiyo idea na fanya kijasiriamali
 
Mi nahitaji msaada ni wapi nitapata pumba za mpunga kwa dar es salaam, asanteni sana na ninasubiri majibu.
 
Nipo katika eneo ilinalolimwa mpunga sana na kuna mashine mpya za kichina mabazo sio zinakoboa mpunga ila zinamenya!!
Pumba zinazotokana na kumenywa kwa mpunga zimelundikana sana na nia yangu ni kutafuta ushauri kuhusu kuzigeuza kuwa kuni.
Je kuna teknoljia ya kuweza ku press na kutengeneza kuni,nijuzeni ndugu zangu.
hizo pumba zipo mkoa gani?wilaya or kijiji kipi,
Je kuna umeme?
machine zipo ,ila zinatumia umeme.na unaweza kupata mkaa/wood chips nzuri tu.
 
Back
Top Bottom