Public Debate on Land Grabbing in Tanzania

Mwana wa Mungu unaonyesha "utumwa wa akili" kudai kwamba waje watuendeleze kuna tofauti gani na euro centric point of view kuwa walikuja Arfica kutu civilize?

Ama na weye sasa ni civilised?tuache haya mambo,no wonder mmeletewa dini badala ya kuwaendeleza imewapumbaza na kuwafanya watumwa wa wazungu,very sad!

Kwanini tusijikite kwenye licensing ambapo tuna import techologies and hows to?Thats what we should fight for na si eti waje kuichukua ardhi yetu waiendeleze kwa niaba yetu,unaota wewe ndot za mchana kweupe!sana sana utakuwa second class kwenye nchi yako kama unataka waje kuichukua ardhi yako ili "waiendeleze" na watu kama nyie mtaridhika maana mwana wa Mungu si unageuza upande wa pili wa shavu ukilambwa mbata upande mmoja?

Kaazi!
 
Wananchi walilia madini, maliasili

headline_bullet.jpg
Watoa masharti kwa mwekezaji


Rukwa%281%29.jpg

Ramani ya Tanzania ikionesha eneo la mkoa wa Rukwa kwa rangi nyekundu



EHHH NCHI IMEUZWA JAMANI EE MUNGU UTUOKOE NA HAYA MATATIZO YA NCHI KUUZWA AMEEN.
WAHUSIKA WAMEFUMBA MACHO.
 
Wakuu,
hata hivyo hii hapa-Yaani kampuni ya kimarekani inunue eneo halafu lifanyie utafiti?
Kwa upande mwingine nimecheka kuona kichwa kinasema "CCM yaanza kuuza nchi Tanzania"-Samahani lakini sioni ni jinsi gani CCM ikahusishwa na utoaji wa ardhi katika hiyo habari.

CCM ni wakala wa ardhi? Au Siasa tu?

Mkuu

Kaa huoni role ya CCM hapa nadhani unayo kazi ya ziada kuelewa kinachoendelea kwene hii thread.
 
Mwana wa Mungu unaonyesha "utumwa wa akili" kudai kwamba waje watuendeleze kuna tofauti gani na euro centric point of view kuwa walikuja Arfica kutu civilize?Ama na weye sasa ni civilised?tuache haya mambo,no wonder mmeletewa dini badala ya kuwaendeleza imewapumbaza na kuwafanya watumwa wa wazungu,very sad!
Kwanini tusijikite kwenye licensing ambapo tuna import techologies and hows to?Thats what we should fight for na si eti waje kuichukua ardhi yetu waiendeleze kwa niaba yetu,unaota wewe ndot za mchana kweupe!sana sana utakuwa second class kwenye nchi yako kama unataka waje kuichukua ardhi yako ili "waiendeleze" na watu kama nyie mtaridhika maana mwana wa Mungu si unageuza upande wa pili wa shavu ukilambwa mbata upande mmoja?
Kaazi!

Nakubaliana na maelezo yako nadhifu. Umeonesha mwanzo wa matatizo ya m-TZ, pale yanapoanzia, FIKRA DUNI. Anabweteka na kusubiri mwekezaji, mwezeshaji au mfadhili, kwa ALMOST EVERYTHING. Hii ndio talk of town kwene maofisi ya serikali mpaka huko mawilayani. Unaeza kujaribu kuangalia harakati za miradi mbalimbali ya maendeleo na kungalia mingapi haswa ni kazi ya nguvukazi yetu, mawazo yetu, fedha yetu, ukitafuta takwimu utashangaa..karibu kila kitu HATUWEZI.

Mawazo ya watu kaa huyu 'mwana wa mangi' ndio mawazo ya viongozi wetu na wengine wengi wa kiafrika. Wana mawazo ya kutaka kuwa mbwa milele. Mbwa daima anatafuta kuongozwa na kuambiwa nini afanye. Akiachwa peke yake anaweza kufa kwa njaa huyu. Kama tungekuwa na viongozi wenye fikra za kujitegemea kama paka, tungefika mbali sana.
 
Watanzania mungu atusamehe hatujui tulitendalo, mtu hujajua hata anakusudia kufanya nini na hiyo ardhi wewe unasema wananchi watapata ajira, hivi unafahamu asilimia kubwa ya maeneo ya vilivyokuwa viwanda vya umma vimebadilishiwa matumizi nje ya makubaliano ya awali na hakuna yeyote anayehoji?

Kiwanda cha ZZK (zana za kilimo kilichopo Iyunga mbeya sasa hivi ni godown la beer ya serengeti wakati hao wanaoitwa wawekezaji wakati wanapewa eneo hilo walisema wataendeleza utengenezaji wa zana za kilimo kwa ajili ya nyanda za juu kusini na nchi kwa ujumla. Mambo yanafanyika kwa uwazi bila kificho chochote.

Tatizo kubwa la nchi yetu ukiwa mzawa hupewi kipaumbele na kwamba sifa za uwekezaji ni lazima uwe mgeni dhana hii inatudhalilisha kama taifa. Kibaya zaidi nchi imejaa viongozi waongo ambao kwa maslahi na visenti wanavyopewa huwa hawahoji chochote mambo yanapokwenda nje ya mikataba iliyokubalika wakati wa kukabidhiana miradi mbalimbali.

Sio tatizo la nchi yetu, bali ni uongozi wa CCM na ubwege wa watanzania kuwaachia nchi CCM. Hivi CCM wanaharakia wapi, yaani JK anataka afanye yote yaonekane kwa miaka 10? tu BILA MSINGI WOWOTE IMARA. CCM hawajajenga msingi wowote IMARA.

CCM wameuza nyumba za serikali na viwanda kwa miaka michache tu ya Mkapa, watauza ardhi na madini yake kwa miaka michache tu ya Kikwete, pia "mabilioni ya Kikwete" yametumika kuuza sura ya Kikwete kwa walalahoi KISIASA kwa mwaka mmoja tu wa Uraisi wake. JK pia amejenga mashule ya Wazazi nchi nzima na Chuo kikuu Dom kwa miaka michache tu aliyopo madarakani. Yote haya ni kujitafutia sifa tu ambazo hazina tija, haraka haraka ya nini? Haiwezekanani ukajenga mashule nchi nzima na yakasimama yakiwa na walimu, majengo na vifaa kwa muda mchache kiasi hicho. Hata mwekezaji akajua papara zenu CCM na kwa nini asiwatapeli. Mkitaka kuleta maendeleo "kesho tu" sawa lakini kumbuka vichwa vyenu maji tu na hamna mlichoweza tokea Uhuru.

Kutoa ardhi kwa miaka 99 kwa nchi corrupt kama Tz ni ukichaa. Juzi tu Kikwete kakubali hatuna wataalam wa mikataba sasa hii ya miaka 99 nani atasimamia. Kwa serikali fisadi kama ya CCM si muda mrefu kuna waziri atasign mkataba wa kifisadi tena na kuwaongezea tena miaka 99 kufikia jumla miaka 198.
 
Miaka 99 ni zaidi ya miaka yote tuliyotawaliwa na wakoloni: Wajerumani na Waingereza kuanzia mwaka 1884 hadi 1961!!!
 
fikra za kiujamaa hazitatufikisha popote, tuingie kwenye full capitalism wajameni, nyerere alitumaliza na propaganda zake, ona hadi sasa bado tunahangaika na upupu aliotumwagia.

Capitalism ni nzuri tu hasa kama una serikali imara NA MAKINI lakini lazima iwe CAPITALISM YA KITANZANIA, kwa maana kua maslahi ya WATANZANIA lazima yalindwe. Kama hatuna serikali inayojali watu na basi hata iwe Ujamaa ama Capitalism, nk vyote havifai.

Investor toka aje anafaidika pia na mwenyeji awe anajikwamua kwa njia moja ama nyingine, sasa kama serikali haiwezi simamia hicho basi hamna haja ya investors.
 
"Nguvu iliyotumika kumwondoa mkoloni kwa kupigania huru ndio pia itumike kuutokomeza huu ukoloni mamboleo" bila hivyo hatutafika!
 
Kuna mtu anaweza kukiweka tena kile kisa cha Sultan Mangungo wa Msovero na Wajeremani na mikataba fweki ya ardhi ya miaka 99? Kunradhi kidogo, nadhani itasaidia kidogo kufundisha baadhi ya vichwa vigumu humu ndani.
 
pindabungeni%284%29.jpg

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda



Serikali imesisitiza kuwa haitakubalika na si busara kwa mtu yeyote kuuza kinyemela ardhi ya Tanzania kwa wageni kufuatia uanzishwaji wa Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jana.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge.
Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF), ambaye alitaka kujua kauli ya serikali kwa baadhi ya Watanzania watakaouza ardhi ya Tanzania kinyemela hasa baada ya milango ya soko la pamoja la EAC kufunguliwa jana.
Kadhalika, mbunge huyo alisema ipo hatari kwa waajiri wa sekta binafsi wakaanza kuwanyanyasa wafanyakazi wao kwa kisingizio cha kuleta wataalam wa kutoka nje.
Akijibu maswali hayo, Waziri Mkuu alisema haitakuwa busara na haitakubalika kufanya hivyo na mtu yeyote atakayeuza ardhi ya Tanzania kwa wageni isipokuwa kwa shughuli za uwekezaji, serikali itayafuta mauziano hayo.
Pinda alifafanua kuwa licha ya kuanzishwa kwa soko la pamoja, bado kuna maeneo mengi yataendelea kutawaliwa na sheria za nchi husika.
Aliwataka Watanzania kufahamu kuwa mtu yeyote mgeni ambaye hajatimiza masharti ya hapa nchini, hapaswi kuuziwa ardhi.
Alisema hata suala la ajira haliwezi kuwa la holela tu kama shamba la bibi na kuwataka waajiri wa sekta binafsi nchini kuenzi kwanza nyumbani kwa kutoa kipaumbele cha ajira kwa wazawa kwa kuwa wapo wataalam wa kutosha isipokuwa pale tu inapobidi.
Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania wasiende kwa hofu kuhusiana na soko hilo la pamoja kwa kuwa hawajui kilichoko mbele yao.



CHANZO: NIPASHE

Je serikali kweli itaweza kutekeleza inayoyasema?Au Maneno matupu ya Siasa? Vipi jamani kuhusu Kigamboni nasikia kauziwa Mzungu huko?
 
Kikwete ahaidi kusimamia Haki (Kutoka Kampeni ya Kikwete)


MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kuwa akichaguliwa Serikali yake itanunua mashamba makubwa ya ardhi isiyotumika ili kuigawa ardhi hiyo kwa wananchi wanaoihitaji.
Hata hivyo, Rais Kikwete amesisitiza kuwa suala hilo litakuwa la makubaliano kati ya Serikali na wenye mashamba hayo na kamwe Serikali haitataifisha mashamba hayo kutoka kwa wenyewe.
“Kamwe hatutataifisha mashamba ya watu. Tutazungumza mpaka tuelewane, “Rais Kikwete amesema leo, Jumatatu, Septemba 13, 2010, wakati aliposisima katika eneo la Kwashemshi kusalimia wananchi wakati wa mikutano yake ya Kampeni ya Uchaguzi Mkuu katika mkoa wa Tanga.
Mahitaji ya ardhi ya wananchi kujilimia mazao yao ya chakula na biashara yalikuwa moja ya vilio ambavyo Rais Kikwete amekumbana navyo katika mikutano mingi wakati wa ziara hiyo ya Kampeni leo.
Kila changamoto hiyo ilipoibuliwa na wananchi, Rais Kikwete ameambiwa kuwa baadhi ya mashamba makubwa, hasa ya mkonge yaliyotaifishwa, yametekelezwa na wenyewe wakati wananchi wanaendelea kuhangaika bila kuwa na ardhi ya kujilimia.
Wananchi katika eneo la Kwashemshi, kwa mfano, wametoa mfano wa mwekezaji mmoja ambaye wanadai kuwa tokea anunue shamba hilo la mkonge kwenye eneo hilo miaka 13 iliyopita, hajapata kuonekana tena.
Mgombea huyo wa CCM leo amefanya mikutano ya Kampeni na kusalimia wananchi katika maeneo ya Gombero, Maramba, Daluni, Mashewa, Matonge, Magoma, Makorora, Kwemazandu, Kerenge, Korogwe Mjini, Kwashemshi, Dindira na Bangalai, Bumbuli na Soni.
Mjini Korogwe, Rais Kikwete amerudia kuwahakikishia wananchi kuhusu azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata ardhi, akisisitiza kuwa Serikali yake inalijua tatizo la uhaba wa ardhi, na katika maeneo mengine ukosefu wa ardhi, na kuwa akichaguliwa tena kuongoza Tanzania atachukua hatua za kupunguza tatizo hilo.
“Hili la mashamba tuachie tuhangaike nalo. Hatutaweza kupata mashamba yote, lakini ni dhamira yetu kuzungumza na wenye mashamba makubwa ambayo hayatumiki na tuna matumaini kuwa matokeo ya mazungumzo hayo yatakuwa mazuri,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Tutachukua hatua za kuhakikisha tunawapatia wananchi wetu ardhi. Tutaifanya kazi hiyo kwa namna ambayo hatutatisha wawekezaji kwa sababu hawa ni watu muhimu kwetu. Tutakapokuwa tumeamua kupata ardhi basi tutazungumza na wenye ardhi ili waweze kutuuzia ardhi hiyo na tutawafidia kwa haki kabisa.”
Katika eneo la Magoma, wananchi wamemwambia Rais Kikwete kuwa kiasi cha wakazi 3,000 wa eneo hilo hawana ardhi ya kulima pamoja na kwamba shamba la mkonge katika eneo hilo limetekelezwa bila kuendelezwa.
Katika eneo la Matonge ambako wananchi wamemshukuru Rais Kikwete kwa kuwa Rais wa kwanza wa Tanzania kutembelea eneo hilo, pia ameelezwa tatizo la ukosefu wa ardhi ya wananchi kujilimia.
Rais Kikwete pia amewaambia wananchi katika maeneo mbali mbali ambako amesimama kuwa Serikali yake imedhamiria kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara nchini na kwa maeneo aliyopitia amesema kuwa barabara ya Soni-Bumbuli-Dindira-Kwashemshi-Korogwe itajengwa kwa kiwango cha lami.
 
Hilo fungu la kununua hayo mashamba ndo EPA ya uchaguzi wa 2015 au? I can't buy this nonsense
 
Rais Kikwete amesisitiza kuwa suala hilo litakuwa la makubaliano kati ya Serikali na wenye mashamba hayo na kamwe Serikali haitataifisha mashamba hayo kutoka kwa wenyewe.
"Kamwe hatutataifisha mashamba ya watu. Tutazungumza mpaka tuelewane"...

Naona Mh. Kikwete keshaongea na Mh. Mkapa kuhusiana na mali mbalimbali alizojipatia akiwa kama Rais. Maana si muda mrefu kule Kiwira nako ametoa ahadi inayofanana na hii hii kwa wananchi wa maeneo yale. Mara ghafla tunaona tena ahadi nyingine inayohusiana na kurudisha mali zilizochukuliwa kinyemela na viongozi wenzake... nahisi yatakuwa ni yale mashamba ya mamia ya hekari yaliyochukuliwa na Mh. Mkapa kule Lushoto kwa mbinu zilezile zilizotumika kuchukulia Kiwira!!

Kwa mtiririko huu, nahisi ahadi inayofatia itakuwa nyumba za serikali kwa pale Dar...!!
 
Hiyo ni ahadi hewa nyingine. Likija swala la kuhamisha walalahoi huwa hakuna majadiliano, hata kama mtu alipata eneo hilo kihalali. Lakini mtu akishaitwa muwekezaji, hata kama hakuna anachowekeza utaona serikali inavyofyata mkia.

Hivi ni serikali gani ambayo ina abudu wawekezaji na matajiri, na kuwaonea wananchi ambao ni walalahoi? Ngoma ya Kigamboni imetulia, inasubiri uchaguzi upite, baada ya hapo wakazi wote walio na vibanda vyao hilo eneo wataondolea kama wakimbizi.

Fanya comparison ya kauli hii ya leo na kauli aliyoitoa Kigamboni siku ya kampeni. Kigamboni wananchi walipolia kuhusu kuhamishwa alisema, nitawasemea ili haki yenu mpewe. Lakini huko kwa wawekezaji, anasema serikali itaongea nao mpaka waelewane. Mbona hakutaka kuwaahidi walalahoi wa Kigamboni kwamba serikali yake itakaa nao na kuelewana nao?

Kwashemshi na Kigambo wote wana tatizo linalofanana, serikali inatumia approach 2 tofauti kabisa. Kigamboni ardhi anapewa muwekezaji, so mlalahoi [sorry member wa JF mwenye jina hili] analazimishwa kuondoka, atake asitake, hicho alichowaambia Chiligati wakazi wa Kigamboni na kuwatisha wananchi kwamba hata wafanye nini, lazima mtahama tu. Muwekezaji akishapewa ardhi, ikifika mahali ardhi hiyo hiyo inahitajika, tunaanza kumbembeleza na akigoma hatuna la kumfanya. Lakini mlalahoi akigoma anaondolewa kwa nguvu. What a double standard!
 
Unajua wanafanya kama mchezo wa karata tatu.. binafsi ningependa kuwajua hawa wenye mashamba wasioyaendeleza ni kina nani? Maana wanaweza kuwa walibinafsishana wenye in 1990s kwa bei chee halafu leo wana flip kwa bei ya juu na wanatoka bado winners..
 
Back
Top Bottom