Public Debate on Land Grabbing in Tanzania

kama hakuna sheria iliyovunjwa sioni kama kuna problem
Ni kweli hakuna problem lakin ulimsikia Mbunge wa Mpanda Mjini akisema bungeni wakati anachangia hoja ya Ofisi ya Wazir Mkuu kwamba hataki kuwa sehemu ya ufisadi huu kwa kuwapa wazungu ardhi kwa malipo ya Tshs 200 kwa eka kama kodi ya ardhi na Tshs 500 kwa eka kama ada kwa halmashauri ya wilaya hivi hakuna watanzania wenye uhitaji wa ardhi na ww unasema no problem tena aliendelea kusema wanamilikishwa kwa miaka 99 kazi kwako NO PROBLEM
 
Ni kweli hakuna problem lakin ulimsikia Mbunge wa Mpanda Mjini akisema bungeni wakati anachangia hoja ya Ofisi ya Wazir Mkuu kwamba hataki kuwa sehemu ya ufisadi huu kwa kuwapa wazungu ardhi kwa malipo ya Tshs 200 kwa eka kama kodi ya ardhi na Tshs 500 kwa eka kama ada kwa halmashauri ya wilaya hivi hakuna watanzania wenye uhitaji wa ardhi na ww unasema no problem tena aliendelea kusema wanamilikishwa kwa miaka 99 kazi kwako NO PROBLEM
Hivi, ni bara la Afrika peke yake lililo na ardhi isiyotumika? Marekani kuna ardhi isiyotumika na baadhi ya wakulima hulipwa kila mwaka wasilime ili kusaidia bei za mazao ya kilimo ya Marekani. Kwa nini basi hao wawekezaji wasitafute ardhi Marekani au Canada, au South America? Sababu ni rahisi. Africa is the most exploited continent and there are no policies to safeguard our land. So foreigners see it as an easy money making destination. Na sisi tulivyo mbumbumbu tunaona kugawa ardhi yetu for nothing ndio uwekezaji wenyewe.
 
Wahindi nao wanapambana kuwauzia ndugu zao mashamba. Kuna wabangladesh wamenunua mashamba huko pemba mnazi na walipelekwa na wabongo na wahindi hapo hapo kisutu. Kuna wengine 8 wanajiandaa kuja ila wanatuma hela kwa hao ndugu zao ili wajifunze kiswahili. Wao walikuwa wananiulizia hili eneo la pemba mnazi likoje? Tahadhari tu.
 
Ancestors wa Watanzania watalia na nyie na vizazi vyenu vyote kwa kuuza na watoa aridhi ya vizazi vyao kwa wageni,endeleeni siku ikifika itakuwa kulia na kusaga meno.Migodi shughuri yake bado aijaishi tayari mmedakia Ardhi jamani mbona maisha ya Mtanzania mmeyageuza mchezo wa kuigiza.

Maisha kamwe si jumba la maigizo japo wenye mamlaka wanataka tuamini maisha ni maigizo.Na kama kweli maisha ni maigizo basi omba scine iishe kwa audience kufurahi mchezo huo ulioigizwa,vinginevyo patakuwa hapatoshi na sijui kipi bora kuishi siku haupo mbele ya uso wa wana dunia unaacha familia yenye furaha kuwa ni Watanzania au kuishi siku haupo duniani familia yako ikaishi ughaibuni na kutafutwa kuja kuludisha mali mliowauzia wageni.
 
-
Bila kfanya kama Egypt au Tunisia tutashitukia watanzania ni tenants katika nchi yetu ya kuzaliwa!
 
Kwa kifupi TZ hamna fedha, hamna ujuzi kama nchi kiasi cha kuweza kujiamulia mambo yenu ya uchimi wenyewe na hata bajeti zenu zinategemea wafadhili ili mutekeleze miradi yenu ya maendeleo.

Sasa naelewa kwa nini umefikia hitimisho hilo.

Tanzania tuna fedha nyingi mno, huwezi amini tatizo ni distribution of resources, lack of prioprities na wizi wa rasilimali zetu unaofanywa na baadhi ya viongozi

Ujuzi tunao mwingi sana vijana wamesomeshwa wakeelewa walichosomea tatizo nchi haitaki kuwatumia, au ikiwatumia haiwalipi wanavyostahili na ndio maana wanaenda kutafuta ajira nchi za nje, na taifa linaishia kupata hasara.

Mambo ya kushindwa kuamua mambo yetu wenyewe inatokana na ukweli kuwa viongozi wetu wengi wana mtazamo kama wako wa kutegemea wafadhili na kama unategemea wafadhili basi lazima wao ndo watakuwa na sauti.
 
Back
Top Bottom