public anouncement:RC arusha anena!

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
chadema waliomba(jana) lema apewe mdhamana lakini logistics zimekataa mpaka baada ya siku 14.chadema waliomba kibali cha mkutano kwa siku ya leo.lakini cdm wamekiuka hilo na kuamua kukesha eneo la nmc.kitendo hiki ni kinyume na taratibu za kimahakama.wakazi wa arusha walioko nmc wanapewa wito wa kuondoka au kutokwenda nmc.wananchi wanapewa wito wa kuendelea na shughuli zao na wasikubali kurubuniwa na watu kutoka nje ya mkoa.mahakama haifanyi kazi kwa kushinikizwa.kwa ufupi hii ndio taarifa kwa umma wa watu wa arusha iliyotolewa kupiti triple A fm arusha.
 
Mwezi wa tisa mwishoni nilikuwa Arusha...kimisingi wakazi wa Arusha ni balaa...kuna dalili ya vurugu kubwa kutokea Arusha...Inahitajika hekima katika hili..kumtoa Lema ni hekima kubwa zaidi maana ni mwakilishi wa wananchi na anatakiwa awepo bungeni kesho....
 
Tunategemea wakazi wa Unga Ltd ambao hawashiriki huo mkusanyiko hawatazuiliwa kuendelea na shughuli zao za kkawaida.
 
RC lazima aelewe kwamba CDM wanajua kwamba waliomba kibali cha aina gani, na wanaelewa walichoamua, hivyo akitaka kutumia nguvu kuliko busara kwa hili, atazua balaaa.
 
Wakeshe kwa amani bila kubugudhi wakazi maeneo ya jirani. Polisi watoe ulinzi kama kawaida, ikiwezekana kesho mchana apewe dhamana kwa masharti ya kwenda bungeni dodoma, ili ziara ya Prince Charles jijini Arusha siku ya j'5 iendelee bila usumbufu. Wakati mwingine ule ushauri wa 'funika kombe mwanaharamu apite' huwa una mantiki katika hali kama hii.
 
labda mchana watu wataongezeka lakini usiku huu na baridi hili nadhani watu watakaokesha ni wachache.
 
Mwezi wa tisa mwishoni nilikuwa Arusha...kimisingi wakazi wa Arusha ni balaa...kuna dalili ya vurugu kubwa kutokea Arusha...Inahitajika hekima katika hili..kumtoa Lema ni hekima kubwa zaidi maana ni mwakilishi wa wananchi na anatakiwa awepo
bungeni kesho....

mkuu unachosema nikweli watu wahuku mpaka wazee wamebadilika kabisa! juzi nilikuwa pale CRDB bank kuna jamaa alikuwa anaongea kwakuisifia CCM! watu walimbadilikia mpaka nikaogopa! watu wahuku nitofauti nasehemu zingine zote inchini!
 
Mi nadhani kama wangeeleza sababu ya msingi na ya kisheria iliyopelekea Mh Lema kunyimwa dhamana haya yote yasingetokea lakini kuna mazingira ya ukandamizaji wa haki,kwani kosa la Lema si la kupata dhamana?na pale mwanzo kwa nini walisema dahamana iko wazi leo kaifunga nani?laikini je Mh Tundu hajui kutafsiri sheria inayohusu dhamana kwa watuhumiwa?na ndio maana wameamua kulala viwanja vya NMC kwa sababu wameona wazi kuwa kuna ukandamizaji wa haki,kuna uonevu wa hali ya juu,na ki ukweli hili linaendeshwa na usalama wa taifa na maofisa wa polisi kwa ushirikiano na CCM.
Nasikitika kuona kwamba wamepoteza uwezo wa kutafakari na hawana uwezo tena wa kuitumia elimu zao,kwani mpaka sasa wanadhani watu wanaogopa jambo kwa kiasi kikubwa,wasidhani watu wameshasahau polisi walivyua watu Arusha,ingelikuwa hajui kufa wala hawakumbuki kama watu waliuawawa Arusha na au wangelikuwa hawajui ya kwamba wanaweza kukamatwa na kufunguliwa mashitaka basi usingeona mtu hapo NMC.Walipashwa kujifunza ya kwamba watu hawa wako tayari kwa lolote,na usije shangaa hali ikaanza hivyo na mwisho ikasambaa mikoa mingine,mzaha mzaha hutumbuka usaha,libya njoo,libya njoo utamu kolea
 
Wakeshe kwa amani bila kubugudhi wakazi maeneo ya jirani. Polisi watoe ulinzi kama kawaida, ikiwezekana kesho mchana apewe dhamana kwa masharti ya kwenda bungeni dodoma, ili ziara ya Prince Charles jijini Arusha siku ya j'5 iendelee bila usumbufu. Wakati mwingine ule ushauri wa 'funika kombe mwanaharamu apite' huwa una mantiki katika hali kama hii.

Kwahiyo unaona huyu prinzi anaumuhim sana hapa Tz?damn
 
jidananyeni nmc pako nyomi la kufa mtu..kuna mioto (vikome) imewashwa ili wenye baridi waote na bonge la mziki
 
Wao wana uwezo wa kuua raia anytime(kumbuka Tarehe 5 Januari Mwaka Huu), sasa leo walishindwa nini kupindisha kanuni na kumtoa Lema kuepusha haya yanayotokea? Dawa ya kiburi ni jeuri, kipindi hii watakula kiburi yao.
OCCUPY ARUSHA Hadi Upatikane "Utu wa Binadam".
Waraka Wa Lema ni Azimio Jipya La Arusha.
 
Magamba wote na msanii wenu JK mnaichezea amani ya nchi hii watanzania sasa si wa kuwachezea.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom