Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,804
- 1,871
- Thread starter
- #61
Wewe binti Ngoda hizi data zako walakini kabisa:
Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza Tanzania nzima kwa kuwa na shule za Sekondari nyingi kuliko mikoa yote ya Tanzania. Una sekondari 288 wakati hata Dar es salaam ina sekondari 252 tu (Chanzo: www.moe.go.tz/NectaResuls). Wakazi wa kilimanjaro ni 1441000 ukilinganisha na Dar es salaam ambao ni takriban 2,809,000 (Chanzo: Tanzania: Regions, Major Cities & Urban Localities - Statistics & Maps on City Population).
Hizi shule ni za kata ama ni zipi? halafu la muhimu ni idadi ya shule au iadadi ya wanafunzi? je hujuwi kuwa kutokana na shida za usafiri wazazi wengi watoto wao wanasoma mikoani hasa huo mkoa wa kilimanjaro?
Pato la kodi la mkoa wa Kilimanjaro (Rombo, Hai, Mwanga, Same, Mosho mjini na Moshi vijijini) ni 14,236.4 Milioni (Tzsh) wakati lile la Dar es salaam ni 441,000.5 Milioni (Tzsh) (Chanzo: Tanzania Revenue Authority - Kigoma). Kigoma na Kilimanjaro wapi na wapi?
Kabla sijaandika zaidi naomba huyu waziri kivuli wa fedha wa CHADEMA akisaidiana na wapambe wake hapa JF wanieleze ni vipi watazigawanya hizo14,236.4 milioni Tzsh katika huduma za matibabu (hospitali, zahanati na elimu ya afya), Polisi, utawala mkoa na wilayani, pembejeo, na Elimu(mishahara ya walimu, ukarabati na stationaries).
Ni nani aliyekwambiakuwa pato la mkoa hutumika kwa maendeleo ya mkoa? ULISHAWAHI KUSIKIA MKOA UPI UKIPITISHA BAJETI YAKE ? Je hujui kuwa hilo pato la mkoa wa Dar es Salaam linajumuisha wakaazi wa mko wa Kilimanjaro pia?
Mkishindwa kufanya hivyo maana yake ELIMU BURE KWA WATANZANIA WOTE NI PROPAGANDA YA UONGO. Vinginevyo mlitaka kutumia pesa ya walipa kodi wa mikoa mingine kuendeleza mkoa wenu maana kiuchumi haiwezekani Kilimanjaro yenye wakazi 1441000 iwe na shule kupita Dar es salaam yenye wakazi 2,809,000.
Sasa wewe mwenyewe umekiri kuwa mkoa wa Kilimanjaro umeendelea kwa kuwa na shule nyingio kuliko Darisalama yako. Hiyo peas ingepelekwa wapi tena? Msuya alipojenga kule kwao Mwanga(Kilimanjaro hiyohiyo) alikuwa Chadema? Kikwete anavyojenga Bagamoyo yuko Chadema?
CAMARADERIE acha Jazba. Kwanza hizo data za kodi ni za Kilimanjaro- ila nilipokopi chanzo nilikuwa nimepele kambele ukurasa. pato la Kigoma ni dogo zaidi.
Shule za kata, walimu hulipwa mishahara na nani? Tafadhali jibu swali hili ni muhimu sana katka kuendeleza mjadala
Bajeti ya taifa hutokana na kodi zikusanywazo mikoani na sio kuwa zinatoka mbinguni. Hivyo unapopiga bajeti yako (japo ni centralised) lakini ili kuwa mhalisia ni vyema uangalie kuwa umeingiza ngapi na umetumia ngapi. Ni lazima ujue na lazima uzingatie sana kuwa hizi pesa zinatoka kwanza mikoani kwenda makao makuu. Hivyo kama wewe ni mchumi mzuri ni vyema kuelewa kuwa ulipopewa pesa toka makao makuu umepata zaidi ya ulichoingiza au chini ya ulichoingiza. Pili, matumizi yako ni zaidi ya ulichoingiza au ni chini ya ulichoingiza. Hivyo ndivyo uchumi unavyokwenda.
Samahani hoja yako ya mwisho sijaielewa mantiki yake hivyo sitaijibu.