Propaganda za uongo: Elimu bure, CHADEMA ikishinda

Mkuu mada yako ni nzuri,
Ila jaribu kuangalia Nyerere kipindi kile aliweza kwa kutumia rasilimali zipi?
Na pia kipindi hiki raslimali hizo zipo, zimepungua au zimeongezeka?
Kutoa elimu bure, itategemea na utashi na uzalendo wa kweli wa serikali,
Kwa mfano hivi sasa fedha nyingi zinapotea kutokana na ufisadi, misamaha ya kodi na mambo kama hayo,
Ikiwa mianya hiyo itazibwa kuna uwezekanno mkubwa kupata elimu na matibabu bure,
Gharama za uendeshaji wa serikali ni kubwa, na hii ni sehemu moja wapo ya mianya ya mataumizi mabaya ya fedha za Umma.
Inanitia shaka kwa nini umeamua kulinganisha Dar na Kilimanjaro? kwa nini usizungumzie Tanzania at large?
Kigezo kisiwe ngome ya CDM, bali ukweli wa jambo!
Kwa uelewa wangu kipato kinachopatikana mkoa wa Kilimanjaro na mikoa mingine kinapelekwa Serikali kuu,
Linganisha Pato la Taifa leo hii na wakati ule, pia idadi ya watu! Linganisha uwekezaji na tunachovuna kupita huo uwekezaji kama ni sawa na mataifa mengine ktk nyanja husika!

Hakuna kisichowezekana, ni uzembe wetu na serikali inayotuongoza ya kutokuwa na Uzalendo wa kweli kuwatumikia wananchi wake!
Ni kiasi kikubwa sana cha pato la serikali linaishia mikononi mwa wachache, najua unajua hili.
Inawezekana tukitia nia!
AMKA
 
Huhitaji kwenda shule kuelewa hiyo hoja ya elimu bure!! Elimu bure inawezekana, fanya homework yako vizuri tutakuelewa kama utatuletea facts siyo kuturudisha nyuma wakati tuko karne ya 21.

Huhitaji shule! Hivi wewe uko makini?

Unajua itaigharimu kiasi gani Mkoa wa Kilimanjaro kutoa Elimu bure kwa shule 288. Kweli Waafrika uchumi hawaujui. Tafadhali jisahihishe. Kama mlikurupuka tu bila kutumia shule kupiga kampeni ya ELIMU BURE, basi kweli CHADEMA NI CHAMA CHA PROPAGANDA.
 
Maneno mengi yanini. Wewe toa makadirio yako ya kodi na unipigie hesabu ya matumizi katika sekta zote mkoani na utoe balance. Usikosoe tu jaribu kuja na majibu mliyonayo kwa data unazozielewa wewe.
vipi lini madeni wa wazee wa africa mashariki yatalipwa?
au zile suti tano ziuzwe ipatikane hela?????
 
Zawadi,
Unapouliza swali ni vizuri uwe na back up ya mfumo unaotawala mpango wa matumizi ya maendeleo nchini. Sasa unapotaka kuona Mkoa wa Kilimanjaro ukiweza kujitosheleza wakati maendeleo ya nchi bado yako centralized kupitia serikali kuu, unajaribu kujenga hoja gani haswa?. Ingekuwa vizuri sana kama ungeuliza swali bila kuwapangia Chadema watosheleze Elimu bure kutokana na kitu unachofikiria wewe. Usitake kulazimisha majibu unayoyategemea wewe..

Hili sii swali bali umejijengea majibu akilini mwako na kuona haiwezekani kwa sababu hujui mikakati ilitowekwa isipokuwa ile unayofikiria wewe...Kwa hiyo badilisha usemi wako, Uliza - Chadema waliahidi Elimu bure kwa wote wangeweza vipi kufanikisha azma hiyo?..Hata mimi ningependa sana kusikia Chadema walitarajia kufanya nini ili kuhakikisha Elimu bure inapatikana.

Halafu Nyerere hakushindwa kutokana na Elimu bure..Labda nikukumbushe tu kwamba Nyerere alitumia kiasi kidogo sana cha bajeti ya serikiali ktk ELIMU ukilinganisha na leo hii, isipokuwa kila fedha yake ilikuwa accounted for wakati leo hii bajeti ya Elimu inatumikia zaidi vikao, misafara na matumizi ya wizara pamoja na kulipa mishahara hewa zaidi kuliko ujenzi wa elimu yenyewe.
 
Mwalimu NYerere alitoa elimu bure, matokeo yake baada ya miaka 20 nchi ilitembelea magoti. CHADEMA (Mh Slaa) japo ya kujua hilo bado ilisisitiza kutoa Elimu bure kwa watanzania wote ili ishinde uchaguzi 2010, lakini ikaanguka. Hii ni kutokana na ueleo mkubwa wa watanzania na kuelewa kuwa hizo ni PROPAGANDA ZA UONGO.

Wiki iliyopita nilipoandika Thread "CHADEMA NI CHAMA CHA PROPAGANDA" wengi walidai nilete ushahidi au vyanzo vya taarifa hizo. Sikufanya hivyo kwa kuogopa Mod kuifuta habari hiyo. Leo nimeamua kuandika ushahidi wa Propaganda hizo za uongo tukianzia kwenye kipengele cha ELIMU BURE KWA WATANZANIA WOTE.

Ili twende hatua kwa hatua naona vyema tuanzie na mkoa wa Kilimanjaro ambako ndio Ngome ya CHADEMA ilikojikita. Naomba waziri kivuli wa fedha wa CHADEMA aeleze kinaga ubaga ni vipi kwa kutumia kodi ya mkoa wa Kilimanjaro itamudu kutoa elimu bure kwa wananchi wa mkoa huo kabla hatujazungumzia Tanzania nzima.

Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza Tanzania nzima kwa kuwa na shule za Sekondari nyingi kuliko mikoa yote ya Tanzania. Una sekondari 288 wakati hata Dar es salaam ina sekondari 252 tu (Chanzo: www.moe.go.tz/NectaResuls). Wakazi wa kilimanjaro ni 1441000 ukilinganisha na Dar es salaam ambao ni takriban 2,809,000 (Chanzo: Tanzania: Regions, Major Cities & Urban Localities - Statistics & Maps on City Population). Pato la kodi la mkoa wa Kilimanjaro (Rombo, Hai, Mwanga, Same, Mosho mjini na Moshi vijijini) ni 14,236.4 Milioni (Tzsh) wakati lile la Dar es salaam ni 441,000.5 Milioni (Tzsh) (Chanzo: Tanzania Revenue Authority - Kigoma).

Kabla sijaandika zaidi naomba huyu waziri kivuli wa fedha wa CHADEMA akisaidiana na wapambe wake hapa JF wanieleze ni vipi watazigawanya hizo 14,236.4 milioni Tzsh katika huduma za matibabu (hospitali, zahanati na elimu ya afya), Polisi, utawala mkoa na wilayani, pembejeo, na Elimu (mishahara ya walimu, ukarabati na stationaries).

Mkishindwa kufanya hivyo maana yake ELIMU BURE KWA WATANZANIA WOTE NI PROPAGANDA YA UONGO. Vinginevyo mlitaka kutumia pesa ya walipa kodi wa mikoa mingine kuendeleza mkoa wenu maana kiuchumi haiwezekani Kilimanjaro yenye wakazi 1441000 iwe na shule kupita Dar es salaam yenye wakazi 2,809,000.

Nasubiri majibu yenu kabla sijaendelea na sekta nyingine.

Elimu ya bure primary to University inawezekana, acha propaganda pesa inayoptea kwa misamaha/kukwepe kodi pekee inatosha kugharamia elimu bure wacha mapato yayopotea kwa mikataba feki ya madini,gas,mafuta etc.
 
mwanzoni nilimchukia Obama ila kwa sasa nampenda kuliko Bush just because hardened islamists wanaipatapata sana kwa sasa

Ala? thinking he is gone win? isn't? then you are deceived

Everything thing in this earth will eventually die and decay and so is obama

Justice fighters will be at paradise, injustice fighters will be at hell

the choice is yours, those who got to paradise are the winners
 
magawanyo wa rasilimali za nchi hii hutegemei pale zinapotoka, mapato ya Dar es salaam au kwenye migodi yanawafaidisha hata wamakonde wa Newala na wamakua wa Masasi. Sasa jiulize, mapato ya serikali yanakwenda wapi? si ndani ya mifuko ya mafisidi waliorundikana serikalini na kwenye chama cha Magamba?

Nyerere alisema inchi corrupt haikusanyi kodi, Tanzania ni nchi corrupt, kodi haikusanywi hata kile kidogo kinaishia kugharamia kuiba kura kwenye hata vichaguzi vidogo, sahau Kagoda, Meremeta, EPA n.k Nchi ina viongozi wa ajabu sana (CCM) wawekezaji wanapewa tax relief ya miaka mitano ikiiisha anauza anaingia mwingine naye anapewa miaka mitano mpaka miaka 50 mingine ya uhuru(itakuwa 100) kodi haikusanywi.

Madini hayatusaidii chochote,tumeshindwa hata kujifunza kwa wenzetu wa Botwsana, Zambia nk. hebu jiulize wewe Ngonda, TZ sasa inaweza jifananisha na Rwanda waliochinjana miaka 15 tu iliyopita? posho za vikao na nguo za bure za kijani zisikufanye upoteze utu wako.
Ulianza vizuri lakini umemaliza vibaya. Ninachowaomba mimi ni bajeti yenu kivuli inayoambatana na ukusanyaji kodi (kwa muona wa CHADEMA) na matumizi ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu bure.

Pengine niwe wazi hapa- Kuwa cha BURE KABISA HAKIPO, SWALI ni nani atalipa. Nilivyowaelewa katika kampeni yenu 2010 ni kuwa mtatumia fedha za kodi ya wananchi kutoa elimu bure. Ninachowaomba ni kuiona bajeti hiyo hapa JF ili nielewa kama inawezekana au ni Propaganda za uongo za kuingilia IKULU.
 
Tanzania haikutembea magoti kwa sababu Nyerere alitoa elimu bure. Tanzania tulianza kutembea magoti baada ya vita vya Idi Amin. Be factual.

Mkuu Jasusi hawa wamezaliwa juzi na wanaweweseka na Chadema hatag historia hawajui .Hawajui lini Mwalimu alisema tufunge mikanda na kwa sababu gani .
 
Mimi nashangaa sana watu wanavyoona CDM jinsi ilivyokuwa waongo wakasahau ahadi za JK zilivyokuwa za uongo na zisizotekelezeka. Mimi naamini kabisa kama JK amekasirika kupita kiasi ukimpa mikanda ya kipindi cha kampeni yake ni LAZIMA atacheka sana na hasira kwisha kabisa kwa jinsi atavyojishangaa ujasiri wa uongo kiasi kile aliukoupatai! Hata leo zikifanyika kampeni natumani hawezi kudanganya kama awamu iliyopita.

kWA HIYO uONGO WA jk NDIO UHALALISHE UONGO WA Mh Slaa? Yaani potovu 2 ni sawa na halali moja au......
 
Ala? thinking he is gone win? isn't? then you are deceived

Everything thing in this earth will eventually die and decay and so is obama

Justice fighters will be at paradise, injustice fighters will be at hell

the choice is yours, those who got to paradise are the winners
atakuja moto zaidi yake for sure nilimpenda sana JOHN McCAIN kuliko obama kwa wakati ule.
i lv israel
palestina gona be screwed at UNO.huwezi ipa uhuru mikusanyiko ya magaidi kuwa nchi
 
atakuja moto zaidi yake for sure nilimpenda sana JOHN McCAIN kuliko obama kwa wakati ule.
i lv israel
palestina gona be screwed at UNO.huwezi ipa uhuru mikusanyiko ya magaidi kuwa nchi

Well you deceived and blind

Justice will overaul injustice

Wether you love isra HELL or what

Kama hawafanyi justice watapigwa vibaya sana na MUUMBA (and my trust to MUUMBA is beyong reasonable)
 
Mkuu umenena
Topical mbona unanishangaza? How old are you? Hujui IDD AMIN alichofanya Kagera. Yaani wewe ningekutukana vibaya hujui ndugu zangu na babu zangu waliokufa huko Minziro walikuwa wangapi yaani wewe zuzu. Akili zako kama za JK ambaye haijui Dowans, Hajui kwa nini Tanzania ni Maskini. Na wewe upo upo.
 
Tanzania haikutembea magoti kwa sababu Nyerere alitoa elimu bure. Tanzania tulianza kutembea magoti baada ya vita vya Idi Amin. Be factual.
Usipoteze mda kujibizana na mpumbavu, maana waelewa tunaona wewe ndo mpumbavu sasa, na hata mimi hapa nimekwisha onekana mpumbavu kuingilia thread ya mpumbavu
 
Wewe binti Ngoda hizi data zako walakini kabisa:

Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza Tanzania nzima kwa kuwa na shule za Sekondari nyingi kuliko mikoa yote ya Tanzania. Una sekondari 288 wakati hata Dar es salaam ina sekondari 252 tu (Chanzo: www.moe.go.tz/NectaResuls). Wakazi wa kilimanjaro ni 1441000 ukilinganisha na Dar es salaam ambao ni takriban 2,809,000 (Chanzo: Tanzania: Regions, Major Cities & Urban Localities - Statistics & Maps on City Population).

Hizi shule ni za kata ama ni zipi? halafu la muhimu ni idadi ya shule au iadadi ya wanafunzi? je hujuwi kuwa kutokana na shida za usafiri wazazi wengi watoto wao wanasoma mikoani hasa huo mkoa wa kilimanjaro?

Pato la kodi la mkoa wa Kilimanjaro (Rombo, Hai, Mwanga, Same, Mosho mjini na Moshi vijijini) ni 14,236.4 Milioni (Tzsh) wakati lile la Dar es salaam ni 441,000.5 Milioni (Tzsh) (Chanzo:
Tanzania Revenue Authority - Kigoma). Kigoma na Kilimanjaro wapi na wapi?

Kabla sijaandika zaidi naomba huyu waziri kivuli wa fedha wa CHADEMA akisaidiana na wapambe wake hapa JF wanieleze ni vipi watazigawanya hizo14,236.4 milioni Tzsh katika huduma za matibabu (hospitali, zahanati na elimu ya afya), Polisi, utawala mkoa na wilayani, pembejeo, na Elimu(mishahara ya walimu, ukarabati na stationaries).

Ni nani aliyekwambiakuwa pato la mkoa hutumika kwa maendeleo ya mkoa? ULISHAWAHI KUSIKIA MKOA UPI UKIPITISHA BAJETI YAKE ? Je hujui kuwa hilo pato la mkoa wa Dar es Salaam linajumuisha wakaazi wa mko wa Kilimanjaro pia?

Mkishindwa kufanya hivyo maana yake ELIMU BURE KWA WATANZANIA WOTE NI PROPAGANDA YA UONGO. Vinginevyo mlitaka kutumia pesa ya walipa kodi wa mikoa mingine kuendeleza mkoa wenu maana kiuchumi haiwezekani Kilimanjaro yenye wakazi 1441000 iwe na shule kupita Dar es salaam yenye wakazi 2,809,000.

Sasa wewe mwenyewe umekiri kuwa mkoa wa Kilimanjaro umeendelea kwa kuwa na shule nyingio kuliko Darisalama yako. Hiyo peas ingepelekwa wapi tena? Msuya alipojenga kule kwao Mwanga(Kilimanjaro hiyohiyo) alikuwa Chadema? Kikwete anavyojenga Bagamoyo yuko Chadema?
 
Really? kwanini alienda vitani?
inaelekea wewe hata speech za baba wa taifa huwa husikilizi; sababu za nchi nguingia vitani mwalimu alizieleza kinaga ubaga nenda kanunue mkanda usikilize;

kuhusu hoja yako ya kutoa elimu bure hapa nchini hilo linawezekekana kabisa ikiwa tu utajiuliza mambo yafuatayo:

1. ni kiasi gani kinapatikana kwa kuwalipisha wananchi ada ya shule? kwa maneno mengine ada ya shule inachangia asilimia ngapi ya gharama nzima ya kuwahudumia wanafunzi kwa mwaka?

2. kama chama tawala kinaweza kugawa mabango ya kampeni bure kwa kila nyumba yaliyogharamiwa kwa fedha nyingi, na tena mengine yamewekwa mpaka katika nyumba za tembe kule vijijini kabisa; je kinashindwaje kutoa elimu bure kwa wapiga kura hao? kwa maneno mengine mbona wananchi hawakuambiwa wachangie mabango ya kampeni?

3. tunaposema bure maana yake nini? je ni bure kweli kama ilivyo ofa ya bia? je na kodi wanazolipa wananchi? au ndio zinaishia EPA? nini maana ya serikali? kwa nini tumeiweka serikali madarakani? serkali tumeiweka madarakai ili ikusanye kodi kwa wananchi pamoja na kusimamia rasilimali za nchi yetu ili zitunufaishe sote. moja ya manufaa ni elimu, kwa hiyo serikali ikusanye kodi ijenge shule ili walipa kodi wake wapate elimu bora pamoja na huduma nyingine kutokana na kodi zao (otherwise haina haja ya kuwa na serikali), sio unawalipisha tena ADA baada ya kuwakamua kwenye kodi.

4. haya tunaichangia hiyo elimu; lakini imeboreshwa kwa kiasi gani? Kiwango cha elimu kikoje nchini hivi sasa ukilinganisha na enzi ya mwalimu? kwa maneno mengine kuchangia elimu sio factor ambayo inaweza kusababisha kutolewa kwa elimu bora, zaidi ya kuwakatisha masomo baadhi ya walala hoi ambao wana vipaji lakini wanaishia kuuza mayai kwa sababu tu hawana uwezo wa kuchangia elimu.


kutokana na tafiti mbalimbali inaonesha kuwa malipo ya ada kwenye elimu kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vikuu kwa wanafunzi wote huchangia tshs bilioni 34 kwa mwaka, wakati gharama za mikopo kwa vyuo vikuu tu (achilia mbali gharama ya shule ya msingi na sekondari ambayo serikali inagharamia), ni zaidi ya bilioni 300 kwa mwaka, yaani maana yake kinachochangiwa na wazazi kwenye gharama za elimu ni sawa na kuchukua maji ya kifuu halafu uyamwage baharini, its nothing! hii ni kuwatwika mzigo mkubwa wazazi amabo hauna manufaa yoyote kwa sababu tu serikali iliyopo madarakani imeshindwa kusimamia rasimali za nchi vizuri.

nini kifanyike ili elimu itolewe bure?
1. kuondoa misamaha ya kodi isiyokuwa na tija; tunaambiwa kuwa misamaha ya kodi nchini ni aslimia 4-5 ya pato la taifa, wakati wenzetu wa nchi jirani haizidi asilimia 1. wataalamu wa uchumi wananena kuwa nchi yetu inapoteza tsh 700 bilioni kwa mwaka kutokana na misamaha ya kodi isiyokuwa na tija! kiasi hiki ni kikubwa sana kuliko kile cha bilion 34 ambacho tunawakamua walipa kodi wetu kwa ajili ya kuchangia elimu. kwa hiyo tupunguze misamaha isiyo na tija na pesa inayopatikana itumika kuboresha huduma za jamii ikiwemo kutoa elimu bure.


2. Serikali isimamie vizuri rasilimali zetu ambazo ni adhimu sana katika bara la afrika na duniani kwa ujumla, tatizo la serkali yetu badala ya kutumia akili na technlogia ya kisasa ili tuweze kuchuma rasilimali zetu kwa maendeleo yetu wanyewe, yenyewe inazigawa rasilimali zetu kama pipi tu kwa wageni kupitia mikataba mibovu halafu sisi wenyewe tunakwenda nje kutembeza bakuli! hii haitatusaidia tutaendelea kupata elimu duni hata kama tutaichangia kiasi gani, mpaka hapo ugonjwa huu wa kuto kuzijali na kuzisimamia rasilimali zetu utakapotutoka!

3. serikali ibane matumizi yasiyo ya lazima kama vile posho zisizo na tija kwa mfano waziri analipwa responsibility allowance mpaka laki mbili kwa siku? waziri huyohuyo bado ni mbunge atalipwa tena 70,000 kwa siku atakapohudhuria vikao vya bunge, bado hujaingiza pediem yake, posho ya mavazi nje ya nchi, hujapiga hesabu mashangingi mangapi wanayotumia viongozi wetuwa serikali pamoja wabunge.

katika kubana matumizi pia tusisahau kupunguza misururu mirefu ya misafara nje ya nchi; nilikuwa nasoma makala moja, kwenye kikao kimoja nje ya nchi, Uganda walienda na watu 5, Kenya watu 7, Burundi watu 5, Rwanda watu 6 lakini Tanzania walikwemda watu 25! hii maana yake nini kama sio kuchumia tumbo?

tukumbuke kuwa nchi hii ni masiki; siku zote tunalalamika kuwa sungura mdogo! kama kweli sungura mdogo mbona viongozi wetu wanaishi kana kwamba hatugawani sungura? yaani matumizi ya serkali utafikiri tunafuga na kugawana tembo! je hoja ya sungura mdogo ni ya kweli? mbona viongozi wetu hawaioneshi kwa vitendo hoja hiyo?


4. serikali sasa iseme ufisadi basi! mabilioni ya fedha yaliyopotea kwenye EPA, RICHMOND na mwanawe Dowans, issue ya RADA pamoja na mengine mengi ikiwemo mikataba mibovu ya madini, yange tosha kabisa kuimarisha uchumi wetu na kutoa huduma bora za jamii ikiwemo elimu bure.


TAFADHALI NILIYEJIBU HAPA MIMI NI MTANZANIA TU WA KAWAIDA SINA ITIKADI YA CHAMA CHOCHOTE NA NAKUOMBA TUJIBIZANE KWA HOJA NA SIO MIPASHO WALA MATUSI MIMI SITA JIBU
 
Bila elimu ya bure basi nchi tunatengeneza mabomu yanayotembea yaliyokata tamaa. we unafikiri a loser anachochote cha kupoteza kama vurugu ikianza! Jamani watu wasome waweze kufikiri japo kidogo. Madrasa na jando havitoshi jamani kama elimu ndugu zangu. Tatizo hawa viongozi wengi wamesoma bure kabisa ila hawataki wengine wasome bure. Kenya primary, secondary school, A level from this year watakuwa wanasoma bure, wananini wanatuzidi hawa!
 
Ulianza vizuri lakini umemaliza vibaya. Ninachowaomba mimi ni bajeti yenu kivuli inayoambatana na ukusanyaji kodi (kwa muona wa CHADEMA) na matumizi ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu bure.

Pengine niwe wazi hapa- Kuwa cha BURE KABISA HAKIPO, SWALI ni nani atalipa. Nilivyowaelewa katika kampeni yenu 2010 ni kuwa mtatumia fedha za kodi ya wananchi kutoa elimu bure. Ninachowaomba ni kuiona bajeti hiyo hapa JF ili nielewa kama inawezekana au ni Propaganda za uongo za kuingilia IKULU.

Zawadi siku nyingune usiwe unakuja na thread za kishabiki jipange naona umeanzisha mada umeshindwa kuitetea. shame on you
 
Back
Top Bottom