Elections 2010 Propaganda za CCM kumpa chati Dr. Slaa

No slaa anapote hivyo kisiasa kama mrema

Akianza kuokota makopo ndo mtakubali

Wakati wa watanzania kuingia kwenye dimbwi la kudanganywa na mafisadi umeisha Hakuna kopo litakalookotwa na DR Slaa ni mbele kwa mbele mpaka IKULU ha ha ha
 
Akili ya binadamu inaweza kugawanywa katika makundi manne:

1. Akili za chini. Wenye nazo hujadili nani kala nini, kavaa nini nk,
2. Akili za kawaida. Wenye nazo utawatambua kwa kujadili matukio; nani kafunga goli, nani kampiga ngumi nani, nk
3. Akili za juu. Wenye nazo hujadili mawzo (ideas), kisha huwashirikisha wenzao mawazo yao na namna watakavyoyatumia kuleta tija (maendeleo) ktk jamii. Watu hawa ni wachache na tunawahitaji,
4. Akili za juu sana (extra-ordinary intelligent). Hawa huwa na IDEAS lakini hata wakiwashirikisha watu wachache sana huelewa, wengi hudhani ni uzushi. Ni baada ya miaka mingi watu hawa huonekana kuwa LA, KUMBE, walikuwa sawa....too late. Nadhani wamo kina Isaac Newton, Galileo Galileo, Yesu wa Nazaret, JK Nyerere, nk.

Sasa, sisi na jamii yetu tuko wapi?Kama jamii kubwa ipo No. 1, au 2, basi lazima CCM itumie mbinu hiyo.....,

Ukiyatazama magazeti nayo yamegawanyika ktk makundi hayo...je TV?
 
mozze umeeleza vizuri, unajua CCM kama ni kubugi step ni kwa hili labda wangelileta wiki ya mwisho ya kampeni ambapo watu wasingekuwa na muda wa kulichambua. Lakini inavyoonekana watu wanajiuliza inakuwaje mme atambue leo kaachwa baada ya kampeni kuanza?

Target ya CCM ni kumfanya Slaa achukiwe na jamii imuone hafai kuwa kiongozi, CCM haikuangalia upande mwingine wa shilingi wale watakao mwonea huruma ni wangapi je ni wengi kuzidi watakaomuona hafai? vipi wale watakaopuuza.

Kitu kingine ambacho CCM haikukiangalia ni publicity na sympathy kama nilivyoongea hapo juu, leo hata ambao walikuwa hawanahaja ya kumjua Slaa wanafanya hivyo, baada ya kuyajua mabaya wanayoyasoma kwenye Habari Leo watataka wajue sababu za yeye kuandikwa hivyo kwani yeye ni nani.

Mwisho watakuja kugundua kumbe ni mpambanaji toka bungeni anayepambana na mabaya ya serikali hapo ndipo uamuzi wao utakuja baada ya kuyahusisha matatizo waliyonayo na serikali inayomwandika vibaya anaye watetea na uamuzi nafikiri utakuwa wazi kabisa.

Mwisho huyo aliyekuwa mme anajidhalilisha bure, CCM watakuja kumtupa kama mpira wa wakubwa, amuulize Angelina wa Mrema alivyojichora. CCM hawana urafiki na mtu hata huyo RA ni rafiki yao leo kesho atakuja ambiwa si raia.

Halafu mambo ya ndoa hayamalizwi na mahakama kuu yatakiwa yaanzie mahakama za kifamilia kama zipo then za mwanzo baada ya kutolewa uamuzi ndipo upeleke madai. Mahakama kuu itaomba vielelezo vya mahakama za chini ikiwemo ya familia walifikia wapi itabase kwenye hizo hukumu.

Yeye alichotakiwa ni kwenda kwenye mahakama ya mwanzo na kudai mke kuwa bado anampenda lakini kudai fidia kabla ya kukanusha kama unampenda au la sidhani kama atafanikiwa, na sijui kwa nini mwanasheria wake hakumshauri hivyo.
 
ccm unajua wanaishi karne iliyopita
ccm wanafikiri magazeti ni muhimu sana kama zamani
ccm wanafikiri hii mitandao ya simu iko mjini tu
kwa taarifa yao.....mwaka huu hadudanganyiki
na tutapiga simu mpaka vijijini kuongea na ndugu zetu
kwamba huu ni uzushi tu.....

Hii ni inaonyesha kabisa kuwa slaa nitishio kubwa kwa ccm . Maana wanaona kabisa akiinyakua hii nchi kwa uadilifu wake na sera zake za kufichua zaidi maovu yaviongozi wa serikali ambao wako ccm.

Wanatafutiza uchafu wakumchafua ni wachache wanao weza kubebwa na tuhuma hizo nakuacha kumchagua slaa eti kapora mke!k kuna kiongozi yoyote msafi katika hilo. Heri ya slaa kama kapola kahalalisha . Je hao wanochochea hizo tuhuma wanaumiza wanaume wangapi kwa kuwachukulia wake zao kwa kutumia madaraka waliyo nayo?

CCM tafuteni hoja za kuwarubuni watu naahadi hewa zenu.
Mwacheni slaa atuongozee hii nchi, ili aweze safisha huu uchafu wa ccm majungu matupu.

Ccm wanatoleana kashfa wao kwa wao tumewazoea. Wakipishana kidogo tu na mmoja wao ndani ya chama chao wanamtafutia urai a wa nje au wanamzuria lolote la kumchafua.



Na huyo mume wake wazamani vipi? Anamatatizo sana anatafuta mtaji kwa kuuza mke. Fidia wewe baba yake? Mbona ulimtupa slaa kamuokota kamsaidia na wanao kawafadhili wewe ndiye umlipe slaa kwa kukulelea wanao.

Slaa kweli ni mtu wa watu anahuruma sana kabeba mke na watoto wake na anawalea.

Hii inadhihilisha kuwa slaa anauwezo wakuwaonea huruma watoto wakitanzaia ambao wanaishi maisha yasiyo na uhakika wa kupata hata uji bila sukari katika nchi yenye utajiri mwingi kama hii. Wakati viongozi wanajenga maghorofa kila kukicha.



Huyu mume ni fisadi anataka kujitajirisha kwa kumuuza mkewe ni sawa na wale wauaji
wa albino.

Tena ufisadi wake mbaya sana huyu, si mtu mzuri. Jamii ikae naye mabli .

Watanzaia amkeni njama za ccm na watu wake ni za kifisadi katika kona zote ufisadi wa pesa, ufisadi wa maisha ya watu kwani huyo mwanamke ni huru ana miaka juu ya kumi nanae anaamua nini cha kufanya ccm mnafisadi uhuru wa huyu dada.

Tafuteni uongo wa majukwaani kuwarubuni wananchi kwa ahadi hewaa!

Slaa ilikuwa nisiende kupiga kura nakuahidi mimi na nyumba yangu tutakupigia kura unatisha mambo yako yako juu unawaendesha ccm hawalali. Sera zako ziko juu.

Kweli tendwa katangaza leo vijana wa ccm wanaongoza kwa kuleta fujo katika kampain za vyama vya upinzani. Nahuu ni uhuni ccm sasa imekuwa tatizo katika jamii kwa kuwa na wahuni wengi zaidi kuliko watu walio serious.
 
Akili ya binadamu inaweza kugawanywa katika makundi manne:

1. Akili za chini. Wenye nazo hujadili nani kala nini, kavaa nini nk,
2. Akili za kawaida. Wenye nazo utawatambua kwa kujadili matukio; nani kafunga goli, nani kampiga ngumi nani, nk
3. Akili za juu. Wenye nazo hujadili mawzo (ideas), kisha huwashirikisha wenzao mawazo yao na namna watakavyoyatumia kuleta tija (maendeleo) ktk jamii. Watu hawa ni wachache na tunawahitaji,
4. Akili za juu sana (extra-ordinary intelligent). Hawa huwa na IDEAS lakini hata wakiwashirikisha watu wachache sana huelewa, wengi hudhani ni uzushi. Ni baada ya miaka mingi watu hawa huonekana kuwa LA, KUMBE, walikuwa sawa....too late. Nadhani wamo kina Isaac Newton, Galileo Galileo, Yesu wa Nazaret, JK, Nyerere, nk.

Sasa, sisi na jamii yetu tuko wapi?Kama jamii kubwa ipo No. 1, au 2, basi lazima CCM itumie mbinu hiyo.....,

Ukiyatazama magazeti nayo yamegawanyika ktk makundi hayo...je TV?





Kumbe Jakaya Kikwete (JK) ni kichwa,mnamkubali!
 
Watanzania kwa sasa wamefunguka kifikra kwanza dkt slaa amekuwa mwaminifu sana kwa kutangaza maisha yake binafsi ya kweli , kikwete asimame azungumzie kweli yake anawamama wa barabarani wangapi tena alivyomtaalam wengine anaongozana nao kwenye kampeni wengine anafanya nao kazi ikulu wengine ni madc .
kwa wakristu Yesu alibaini unafiki wa wanadamu walipompelekea mwanamke mzinzi bila mwanaume aliyekuwa akizini nae yeye akawakomesha akawaambia aliyemsafi na anyanyue mkono ampige jiwe mwanamke huyo wote walitoweka akabaki peke yake na mwanamke huyo akamwambia aondoke leo nawaambia CCM na waandishi walioshadidia hoja hiyo aliyemsafi aendelee kumshambulia slaa
 
Nextime fupisha kidogo, lakini every ting iliyoandika ni true true kabisa.

CCM, it's Too late.
 
Nadhani tukiangalia mapungufu,hakuna wa kusimama.Inawezekana mtu akawa mlevi sana lakini hard worker au anaperform zaidi kuliko asiye mlevi.Cha msingi tuangalie ni kiongozi gani ambaye atasimamia maslahi ya Watanzania.
Mambo ya binafsi wakagombane nayo huko kwao,sie tunahitaji sera na jinsi watakavyotekeleza.
 
Kumbe Jakaya Kikwete (JK) ni kichwa,mnamkubali!
mtiwadawa heshimu quotes za watu hauna ruhusa kubadili quotation ya mtu unachotakiwa ni ku quote na kutoa comment yako basi lakini si kubadili maana. Ujue humu kuna watu wazima na heshima zao hatuchezi mdako wa kitoto. Kwa kutumia hii post naku ripoti moja kwa moja kwa MODS. We can anaweza naye kuku-ripoti ili tabia kama hii isirudiwe.

Angalia unavyo distort maana

4. Akili za juu sana (extra-ordinary intelligent). Hawa huwa na IDEAS lakini hata wakiwashirikisha watu wachache sana huelewa, wengi hudhani ni uzushi. Ni baada ya miaka mingi watu hawa huonekana kuwa LA, KUMBE, walikuwa sawa....too late. Nadhani wamo kina Isaac Newton, Galileo Galileo, Yesu wa Nazaret, JK Nyerere, nk.
mtiwadawa kabadilisha badala ya kuacha ilivyo JK Nyerere yeye kaweka mkato ili isomeke JK, Nyerere kama watu wawili tofauti.
4. Akili za juu sana (extra-ordinary intelligent). Hawa huwa na IDEAS lakini hata wakiwashirikisha watu wachache sana huelewa, wengi hudhani ni uzushi. Ni baada ya miaka mingi watu hawa huonekana kuwa LA, KUMBE, walikuwa sawa....too late. Nadhani wamo kina Isaac Newton, Galileo Galileo, Yesu wa Nazaret,JK, Nyerere, nk.
Uhuni na utoto huu hauvumiliki, ujue hizi comment zinaweza kutumika kama ushahidi mahakamani ndiyo maana JF huwa inatunza kumbukumbu.
 
Mbona hii kesi ni rahisi sana. Sitaki maana yake sitaki, Nataka maana yake nataka. Kama haya maneno yamesemwa kweli na mwanadada huyu, nanukuu “NAKUACHIA kibanda chako, nakwenda kwenye nyumba yangu.” basi ni kwamba yalikuwa yamemshinda. Uzuri kamuaga. Kwa hiyo huyu bwana kubwatuka kwake ovyo amejifunga mwenyewe na kumpa Judge kazi rahisi.
 
Pongezi kwa kazi nzuri Mozze.

Nadhani mwaka huu ccm wanakosa pa kukimbilia. Hata hivyo bado kazi ya kuwaelimisha watu tunayo kubwa.
 
Kuna kitu ambacho Wapinzania wanaweza kukifanya na ambacho kinataka ubunifu, ni kuangalia namna gani wanaweza wakatumia power ya media ambayo watawala wame-imonopolize kwa kufanya negative campaign kwa Wapinzani i-turn out kuwa positive campaign kwa wapinzani na negative campaign kwa watawala.

Wenzetu wanasema . . . turning the negative to positive.

Hebu team ya campaign kaeni chini, umizeni vichwa na angalieni nini mtafanya . . . mfano mdogo . . .

Kila siku mnaweza kuwa na press briefing, mkaelezea mambo mengi mazuri ya opposition lakini mkalipua jambo moja kwa watawala ambao watalazimika kutumia media. Of course mengine mazuri pia watayataja.
 
Kuna kitu ambacho Wapinzania wanaweza kukifanya na ambacho kinataka ubunifu, ni kuangalia namna gani wanaweza wakatumia power ya media ambayo watawala wame-imonopolize kwa kufanya negative campaign kwa Wapinzani i-turn out kuwa positive campaign kwa wapinzani na negative campaign kwa watawala.

Wenzetu wanasema . . . turning the negative to positive.

Hebu team ya campaign kaeni chini, umizeni vichwa na angalieni nini mtafanya . . . mfano mdogo . . .

Kila siku mnaweza kuwa na press briefing, mkaelezea mambo mengi mazuri ya opposition lakini mkalipua jambo moja kwa watawala ambao watalazimika kutumia media. Of course mengine mazuri pia watayataja.
Vyombo vya habari vya CCM na serikali yale vinaifanyia Chadema kampeni bila kujijua, Chadema haiwezi kwenda TBC au DTV au ITV au kuwaomba Habari Leo waandike habari za Slaa au waweke picha ya Slaa, lakini wanaweka bila kuombwa kwa kudhani wanamkomoa.
 


Hivi kwa sasa (wakati huu) Aminiel Mahimbo ni mkristo au Muislamu. Sheria inahukumu kulingana na aina ya ndoa na dini za wahusika kabla na baada ya ndoa.
 
Asante Mdau kufafanua kwa undani, mimi nitaongelea zaidi juu ya huyu Mwanaume naomba ajibu yafuatayo
1. Mke wake aliondoka nyumbani kwake lini?
2. Je baada ya kupotea mke wake masaa zaidi ya 24 alichukua hatua gani?
3. Vikao vingapi vya usuruhishi vya kifamilia vilikaa na maamuzi yalikuwa yapi?
4. Jee ni nini chanzo cha mkewe kuondoka nyumbani?

Mwanaume huyo ni mjinga yeye kadanganywa na kina Makamba na wanakurupukia mahamani, mambo ya ndoa ni ya kifamilia zaidi, mahakama lazima ipitie vikao vyote na maamuzi yaliyochukuliwa katika ngazi ya familia.
Masuala ya ndoa yanahusishwa familia mbili wakuu sasa yeye anafikiri CCM itamlinda baada ya kufungua kesi hiyo matokeo yake atakuwa kajijengea maadui wengi zaidi ndani ya familia na jamii kwa ujumla, labda ahamie nyumbani kwa Makamba.

Namlaumu huyu jamaa kwa kudanganywa na CCM (MAKAMBA), kwa kufikiri Makamba atamsaidia, amejitafutia matatizo makubwa mno, akiwa na aklli afute kesi hiyo mapema warudi kwenye vikao vya kifamilia, wayamalize.

Na hao wanasheria Uchara na njaa zao hawajui kwamba maamuzi ya vikao vya kifamilia pia yanatambulika kisheria, kama mtu hatii au kutekeleza wajibu wake kwenye doa lazima abaki na vyeti tu, kufunga ndoa ya kikristo siyo msalaba hadi milele mtu ana uhuru wa kuamua maisha yake pia kama hiyo ndoa imeshindikana. Midume mingi huwa haitoi taraka kukomoa wanawake kwa kisingizio kuwa " Mimi huwa naoa tu kuacha sijui"

Dr Slaa nakuomba uendelee na kampeni zako, haya yote we mwachie Ma Msapu na wanafamilia watamalizana na huyu mwanaume na hao wanasheria wa makamba.

Pia waandishi wa habari acheki udaku, magazeti yote yanaandika story hii ki udaku udaku zaidi, mtanzania ndiyo kabisaa wanafurahia wakati hawajui hii si habari ya tija kwa wananchi -

Wananchi wanataka kujua ufumbuzi wa matatizo yao siyo DR Slaa leo kala nini, kavaa nini, ameoga / hajaoga, ameongea na nani - all those are craps - tuangalie vitu vya msingi na nyie waandishi ndiyo watu wa kutupatia dira.

Mbona hamuongelei ahadi hewa za Jakaya? ngapi alizotoa 2010 kazitimiza? na sasa anaongeza zingine?

Asante kwa mtazamo wako. Ungekuwa mwanasheria HUNGESHINDWA KESI HATA MOJA!
 
Let us be serious with seriiiiooous issues!!! Hivi,tukianza kuongelea habari za wanawake wanaotembea nao nje, si watakuwa kama hawajavaa nguo tu kwenye majukwaa?? CCM mmenisikitisha, mshauri wenu kwenye hili kawaingiza mkenge...
 
Back
Top Bottom