Promotion ya UmojaSwitch ATM

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
UmojaSwitch wamekuja na promotion tatu zitazodumu kwa miezi mitano, kuanzia mwezi wa 8 hadi wa 12.

  1. Mtu atayekua amefanya transactions nyingi kwa huo mwezi atapewa 1M kila mwezi
  2. Kila mwezi, watu watano kutoka watumiaji wa mara ya kwanza au ambao hawajatumia ATM card zao kwa muda mrefu watapata laki 200,000 kila mmoja
  3. Kila mwezi watu 10 watapata 100,000 kila mmoja, kila transaction moja itakuingiza kwenye droo mara moja, kadiri unavyotumia ATM card yako ndio unavoongeza nafasi yako ya kushinda.

Karibuni, tumieni kadi zenu, mtu mwenye wazo nitafurahi kusikia toka kwako.

kutakua na zawadi nyingine tofautitofauti wakati wa promosheni
 
Safi sana ubunifu ukiwa juu mafanikio lazima!

wateja wetu wamekua nasi toka 2007 wakati tunaanza, hawajatuangusha, sasa tunataka kusogea karibu zaidi na wateja wetu, tunataka kama ulivyoita 'kuleta ubunifu kidogo' hii promosheni ina lengo la kuisogeza UmojaSwitch kwa wateja wake zaidi kuliko hapo nyuma.
 
bank business is like gospel business.........!
vijijini watu wasio na kitu wanazidi kuachwa huku huduma hizi zikiwaendea wenye nazo na wenye nafasi!
 
Mahesabu, watu wa vijijini tuko nao pamoja, kwa sasa UmojaSwitch inaunganisha zaidi ya 70% ya community banks zote nchini. Lakini pia lazima nikiri, it is a challenge na si tu kwa umojaswitch bali national challenge
 
Vigezo vya watu kumi kupata laki moja moja ni vipi? Halafu hiyo namba mbili, muda mrefu ni miaka/miezi mingapi?
 
Vigezo vya watu kumi kupata laki moja moja ni vipi? Halafu hiyo namba mbili, muda mrefu ni miaka/miezi mingapi?

Catherine,
  1. Watu kumi watapata 100,000 kila mmoja, Kila mwisho wa mwezi itachezwa droo ya kupata hawa watu, kila unapochukua pesa au unapotuma pesa kwa kutumia ATM zetu za Umoja unaingia kwenye hii droo, (kila transaction moja inakuingiza kwenye droo mara moja) kadiri unavyotumia ndivo unavyoongeza entries zako kwenye droo yetu na ndivyo unavyoongeza nafasi zako za kushinda
  2. Muda mrefu ni kwa watu ambao hawajatumia ATM zao kuanzia 31st December 2011 kurudi nyuma.



 
washindi wa mwezi wa nane kupatikana tarehe 4.Sept.2012
 
Back
Top Bottom