Promotion ya Airtel, Chali! Voda free internet kwisha kazi!

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
633
Heshima kwenu wakuu.

Nilikuwa nje ya mtandao kwa siku kadhaa, leo nimerudi tena hewani ila nimekuta mambo yamebadilika hapa kwangu.
Kwanza, ile voda tuliyokuwa tunatumia bure nimekuta wameishablock. Kwa kuanzia nikajaribu kumunua zile 400MB za Airtel, kama kawaida nikatuma neno 'INTERNET' kwenda 15444 naambiwa nimetuma neno sio sahihi, wanafanya kuorodhesha packages kadhaa eg 10mb, 25mb, 50mb, 150mb, 500mb nk. Ktika hizo 50mb ndiyo inanunuliwa kwa tsh 2000/=

Sasa naomba mnifahamishe waungwana, je, ndio kusema Promotion ya Airtel ndio basi tena jamani! Au ndio imeloga kwangu tu. Na kwa wale tuliokuwa tunakula maisha kwenye voda free, nahitaji kujua ikiwa jamaa wameishablock au ndio inakuwaje tena.

Nawasilisha...
 
Imekula kwa wote mkuu. Ni dhahiri wameamua kupandisha gharama. Sasa ni kuzichakachua modem kwenda mbele tuhamie wapi sijui. Nasikia kina yakhe bado mambo yao cheap
 
Kk jna tu mi nimeweka bando la 400mb, sijui kwa ninyi malioko dar, ila mi wa mkoani jana tu nimefanikiwa, ila cha ajabu nikiuliza salio naambiwa nimetumia mb 3 tu wakati jana nimedownload file la zaidi ya mb 129, bado nipo nipo nione itakuaje.
 
Mkuu kwani wewe shaka yako nini. Wakamue kisawa sawa kabla hawajastukia. Maana baada ya hapo utaungana nasi kuungua jua.
 
Mimi walinisahau kwa takribani wiki tatu, nilidownload vitu vya karibu 250 GB, na spidi ilikuwa fast kweli mpaka 2.95 MB/s. Hawa dawa yao ukipata chance hamna kuwaonea huruma,wameshatuibia sanaaaaa!
 
voda bado ipo sema watu hawajapata proxy zinazodownload tu.... epictunnel ni worldwide ipo down kwa hizi siku mbili ikirudi mwendo ule ule
 
voda bado ipo sema watu hawajapata proxy zinazodownload tu.... epictunnel ni worldwide ipo down kwa hizi siku mbili ikirudi mwendo ule ule
epictunnel sijui kama matatizo yapo kwao maana ukifungua page yao kawaida kwenye browser inaopen nafikiri hawajamaa watakuwa wameblock tu.
 
Mimi walinisahau kwa takribani wiki tatu, nilidownload vitu vya karibu 250 GB, na spidi ilikuwa fast kweli mpaka 2.95 MB/s. Hawa dawa yao ukipata chance hamna kuwaonea huruma,wameshatuibia sanaaaaa!

ukisema sema ukweli. sasa hiyo ni modem gani ino support speed hiyo? na hamna kampuni yeyote inotowa speed hiyo
 
mwishowe nimepata kukujua line zipigiwazo kelele zinakopatikana. zinauzwa elfu kumi kwa moja, au ukitaka mbili elfu 15. kama unataka na upo zanzibar piga 0716 999 806 nikusaidie. kama upo dar kuanzia tarehe 18 mwezi huu nitakuwepo DAR.
 
Wakuu naomba msada, me nina modem ya airtel lakini inanikatalia kujiunga na bundle yoyote, kulikoni?
 
Wakuu naomba msada, me nina modem ya airtel lakini inanikatalia kujiunga na bundle yoyote, kulikoni?

airtel wamebadili bandle zao. zimekuwa ghali kinoma, hata uungwaji wa bundle sio kama zamani. jaribu kuuliza salio *102# watakuonesha jinsi ya kujiunga na bundle mpya
 
airtel wamebadili bandle zao. zimekuwa ghali kinoma, hata uungwaji wa bundle sio kama zamani. jaribu kuuliza salio *102# watakuonesha jinsi ya kujiunga na bundle mpya

nimeshaona, lakini inanikatalia.
 
Mambo yote Voda bana.......

Kwa Tshs. 10,000/= unapata Net kwa wiki nzima......Japo wanakwambia utapata 750Mb kwa speed kubwa na baada ya hapo utapata Unlimited Internet kwa speed ya kawaida speed inakuwa ni ileile tu kwa wiki nzima......Internet bila kikomo saaaafi..........Just SMS Bomba7 to 15300 Unapata Internet isiyo na kikomo kwa wiki nzima...

KAZI NI KWAKO.....
 
Hahaha!Sasa wakuu naona kale kamsemo ketu ka 'hamia' kanakuwa replaced na 'kazi ni kwako'!Life is a JOKE!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom