Project funding sources

tujenge utamaduni wa kurejesha UPDATE za proposal mbalimbali ambazo wadau waliwahi kuziainisha kipindi cha nyuma
 
Mkuu
watu wa Oxfarm wanatoa funds kwa projects kama yako. wameshafadhili na kuendeleza miradi kadhaa afrika hivyo usisite kuwatafuta.

mimi nina knowledge ya fairtrade ambapo kama ukitaka tuition na contacts usiogope kuwasiliana.
Mkuu upo??
 
Ninafarijika sana kusikia watanzania wenzangu una miradi ya kufanya ila tatizo ni fund;nitajaribu ku-check na baadhi ya venture capitalists fulanifulani halafu nione tunaendaje mbele katika kusukuma gurudumu la maendeleo.
Nitaunga nanyi nitakapofanikisha hilo.
Habari za siku,
ndugu yangu upo?
 
Hope it is well there!
Uliichochea sana hamasa nikakamata msitu kusini huko nahifadhi uasili nasubiria pensheni miaka kadhaa ijayo!!!
Mungu akutunze.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nashukuru,
Mungu awe nawe pia. Na mimi naendelea kuweka pensheni yangu misituni mkuu, maana kikokotoo kimegoma kabisa,karibu. Bila shaka umepiga eka za kutosha.
 
Habari za jioni
Naomba kujua kama zipo banks au other private financial institutions ambazo zinatoa mikopo kwaajili ya poultry projects.
 
Salam,
Ata mimi nipo katika kuanzisha mradi huohuo,na kuna wachina wanajenga viwanda vya cassava starch production dunia nzima na sasa wanajenga kimoja cha 150 tonnes per day Eddo state Nigeria.

Wamenitumia full proposal ambayo ina bei na ata matumizi ya kiwanda kwa mwaka na mapato yake.

kuna uncle wangu amenipa mabenki ambayo yapo tayari kufund icho kiwanda nimetembelea Mkuranga kule kuna umoja wa walima miogo (mohogo Saccos) hawa na Uongozi wa Wilaya(serikali) wapo tayari kuwa wabia.so tayari kumbe kuna groud ya kuifanya project ipatiwe funds.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe pia amekubali kusaidia na kutoa land ya kiwanda soko la unga wa muhogo ata apa Tanzania lipo kubwa tu, jua ya kuwa tomato paste,chill,cone za baresa na sausege azitengenezwi bila muhogo.

Let us meet and team up, tufanye pamoja mimi source ya funds ninazo.

But at this time nna other 4 projects nazifanya so hii ya kasava ningependa kuifanya na mtu
please let us meet

This is interesting!
JamiiForums is a life changer!
Nitafurahi kusikia mrejesho wa hii biashara! Let me scroll down the thread!
 
Thanx mkuu. Nadhani mpaka mwaka ujao mtakuwa tayari mmeanza rasmi.
Kwa taarifa nilizopata kilimo cha kitaalamu, hekta moja inazalisha hadi tani thelathini.
Nimepata shamba eneo fulani hapo pwani. Mkuu usichoke kutujuza maendeleo.
Thanx
Tofauti kati ya hekta na hekari ni ipi?
 
Heshima mbele wana JF,

Nimekuwa nahangaikia kupata habari au msaada wa mawazo kutoka sehemu mbalimbali nafikiri na hapa jamvini lazima kuna msaada mkubwa wa mchango naweza kupata kwani naamini hapa ni kitovu cha taaluma na ujuzi wa mambo.

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikifikiria na kutafuta njia mablimbali za kuweza kufanya sisi kama vijana wa kitanzania katika mambo ya kiuchumi (nikimaanisha kuwa na biashara kubwa) tunazoweza kuanzisha vijana na kutufanya kuondokana na mawazo ya kuajiriwa hasa kwa vijana wenye elimu ya chuo kikuu. Lakini ninasikitika sana kuona watanzania wengi tunagombea nafasi za kuajiriwa tu na serikali yetu haina msaada wowote wa kuwezesha kuleta mafanikio. Serikali yetu inatafafsiri ujasiriamali ni kumwezesha mtu kupata rizki, mi naamini bila viwanda vidogo vya kati huo ujasiriamali hautakuwa na manufaa yoyote, wazalishaji wanatakiwa wajue soko na processing ikifanyika thamani ya mazao yao inaongezeka kwenye masoko ya kimataifa.

Kwa mtazamo wangu nimekuwa nikiamini watu wenye elimu ya chuo kikuu wanatakiwa kuwa na mtazamo wa kuanzisha ajira kwani wao wamepevuka upeo tofauti na waliokosa elimu hiyo.

Kwa wanaJF wanaojua jinsi ya kupata resources jamani ninaomba msaada wa mawazo.

Nimefanya feasibility study kwa miaka kadhaa sasa na hatimaye nimeaandaa business plan ya kufanya processing ya cassava (mihogo) kutengeneza starch. Mali ghafi hakuna asiyejua inapatikana nchi kwetu popote pale unahitaji kuwahakikishia wakulima soko tu na watakufanyia mambo ya kutosha. Hii itainua uchumi wa wakulima wadogo sana na hasa kwenye maeneo ambayo kilimo cha pamba kimeanguka na mikoa kame kama ya kati isiyo na zao la biashara kwani popote inastawi

Soko lipo juu sana na lengo ku export tayari kuna watu wanahitaji sana kuimport kutoka Tanzania nimejaribu kutangaza na kupata response nzuri sana. Kuna soko kubwa sana nchini (yote inaagizwa toka nje esp SA) kuna soko kubwa sana pale TBL na viwanda vingine vinavyotengeneza madawa, nguo, bia, tambi, biscuits, noodles, almost viwanda vyote vinavyotengeneza vyakula (canned na bottled) vinahitaji starch.

Tatizo kubwa nililonalo ni kwamba natafuta source ya funds kuanzisha kamradi haka ambacho profit margin yake ipo juu sana. Nipo tayari kwa mazungumzo specific ya jinsi ya kufanya ili mradi niweze kutimiza hii ndoto. Mradi huu unaweza kuwa expanded katika muda wa miaka 2 au 3 ukawa na plant nyingine ya kuzalisha ethanol kwa kutumia waste materials baada ya kuprocess cassava na tayari nimeanza kudraft plan yake. Nimejaribu kupita Tanzania investment bank na kuongea nao wakawa na interest ya kusaidia ila nikawa sina colateral wala mdhamini mwenye assets nzuri (mimi mtoto wa mkulima tu hata elimu yangu ni ya kuungaunga tu) ninaweza kuraise kidogo tu. Nimepita na NBC ikawa vilevile tu na mradi unakubalika na tatizo siaminiki tu kwa vile sina historia ya kushika pesa kubwa.

Ninaweza kusimamia hii kazi na ikawa juu kiasi cha kuridhisha na kushindana na biashara kubwa tu hata kuanzisha zingine safi zaidi.

Haya wadau naomba reference kwenye source au tujiunege na kuona nini cha kufanya. Nipo kwa wazi nasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona

Ahsanteni sana
Kuna source moja ya grant twaweza karibu kuona kama tunaweza kupata grant nicheki kwenye namba hiyo tuwasiliane 0682866788 au 0652809292
 
72 Reactions
Reply
Back
Top Bottom