Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Zakumi,
May be hujasoma hicho kipande vizuri maana kimezungumzia kwa kiasi mapungufu ya katiba. Pia jamaa anaonyesha mapungufu ya katiba toka kipengerecha kwanza.
Kwa vile umekubali kuwa katiba si msaafu au biblia hivyo inaweza kubadilishwa. Kwa nini sasa hukubali kuibadilisha yote badala yake unataka vipengele tu. Sasa labda na wewe ungetusaidia hivyo vipengere unavyofikiri vinapaswa kubadilishwa. Ingawa binafsi sijawahi kuipitia katiba lakini uchambuzi unaonekana kuwa katiba yetu ina contradiction nyingi na ina mapungufu mengi. Vilevile ni katiba ya mkoloni.
Mr. Zero:
Kwenye rangi nyekundu unampa points Mzee Mwinyi bila yeye kuja hapa. Unaomba mabadiliko ya katiba kwa kusikiliza mtu fulani. Wakati katiba yenyewe hujaisoma.
Na sio wewe peke yako ni watanzania wengi tu. Mpaka wabunge hawasomi na kuelewa katiba inasema nini.
Na kwa taarifa yako katiba ya sasa sio ya mkoloni. Katiba aliacha mkoloni ilitoa ruhusa ya vyama vingi. Ilitoa ruhusa ya mgombea huru. Ilitoa ruhusa mbunge kuhama kambi bila kupoteza ubunge wake.
Mapungufu yaliotolewa na jamaa yako hapo yanahitaji marekebisho ya katiba (amendments) na sio katiba mpya.