Program Alert:Mwanakijiji alonga na Star TV "Live" juu ya Busanda

Status
Not open for further replies.
Huyu diwani aliye Mwanza studio za Star Tv anaonekana kuwa na point, anasema CCM kwenye uchaguzi huu wa Busanda hawakuwa na sababu ya kuwa na ahadi tena, anasema walitakiwa kuonyesha mafanikio waliyopata kabla ya uchaguzi huu mdogo.

Anadai CCM waligawa T-shirts, kofia, chumvi n.k lakini naamini Makalla akiongea ataweza kujibu hizi hoja
 
Mwanakijiji anaonekana kufurahia matokeo ya Busanda kuwa walau kura zimepungua kwa CCM kitu kinachoonyesha kuna mabadiliko
 
Vema umenena Mwanakijiji, kuzomeazomea ni tabia mbaya ambayo haistahili kuvumiliwa. Si mkakati mzuri kweli, vema watu watumie hoja.

Ukweli ni kuwa masuala ya EPA au Buzwagi hayafai majimboni wakati wa chaguzi hizi. Wapinzani wanatakiwa kuepuka na kuongelea mambo ya ufisadi tu na kusahau mikakati ya kuwainua watanzania.

CCM wajanja, wanawambia wananchi kuwa waliohusika wengi wameshafikishwa mahakamani.
 
Mwanakijiji anasema CCM wanatakiwa kutuambia nini hatma ya kesi za ufisadi.
 
Maoni ya Mwanakijiji ni kuwepo kwa chama kimoja cha kuweza kusimama kushindana na CCM badala ya utitiri wa vyama vya siasa.
 
Mwanakijiji anauma na kupuliza. Nimependa alivyomalizia kwa kuipaisha JamiiForums.com
 
Tatizo la CHADEMA ni moja, wanataka kuibeba hoja ya EPA kama yao peke yao vile
 
Kuna mdau kapiga simu anaitwa Kanyasu, anasema kuwa CCM haikuchaguliwa na wana CCM peke yake. Anasema CHADEMA walienda na dhana ya kudahani kuwa mtizamo wa kuongelea masuala ya ufisadi ndio utawapa kura zaidi.
 
Kanyasu ambaye ni mwana CCM anasema mbona CHADEMA waligawa soda n.k. Anasema CCM waligawa kofia na T-shirt. Anasema CHADEMA walikosea kwa kusema watawapa chup* na sidiria wanawake, hili liliwakera wananchi sana.
 
Kulikuwa na vitendo vya uonevu sana kwenye uchaguzi wa Busanda, watu walikamatwa ovyo, walipigwa na pia kupuliziwa dawa za sumu.

Kuzomea hakukwepeki, ndio siasa zetu
 
Mwanakijiji subiri uone unajibiwa na kina Erasto Tumbo na Makalla
 
chadema ilisema itagawa chup* na sidiria!......i luv Tanzania
 
Erasto Tumbo anasema chimbuko la EPA ni BoT na wananchi wa Busanda haiwezekani wasielezwe. Anasema kila mtanzania lazima wamfahamishe nini kimepelekea wao kuwa na umasikini walio nao.

Anasema Helicopta ni njia mojawapo ya usafiri, wanaitumia ili kuwafikia wananchi wengi na gharama zake si kubwa kama wengi wanavyofikiria.

Mwaifuge amemwambia kuwa CHADEMA wanakusanya watu wengi kwa helicopta lakini haiwaletei kura nyingi
 
CCM wanasema walilazimika kutumia helicopta Kiteto na Tarime kwakuwa walikuwa nyuma ya ratiba kwenye kampeni (Makalla ndiye kasema hivyo).

gaijin, siasa za Bongo raha tupu
 
Wakuu nimechoka kuwasikiliza hawa, wanaongea politiki za kitoto mara huyu anadanganya mara huyu aligawa t-shirt mara aligawa kahawa mara aliongea matusi, wizi mtupu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom