Professionalism versus Age!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Jana nilimpeleka mgonjwa wangu Hospitali ya Mount Meru akiwa na shida inayohusiana na allergy.

Lakini nilikatishwa tamaa na mganga niliyemkuta kwenye chumba kimojawapo nilichoelekezwa!
Kwa ufupi mganga huyo ni kisichana kidogo kabisa(around 25) ambacho hakijui wala kujali maana ya mtu kuumwa au kuugua, mapozi meengi na maneno ya mkatomkato!
Nilipodadisi niliambiwa kuwa "HAWA NI KIZAZI KIPYA, wameajiriwa juzijuzi mwanzoni mwa mwaka, na wako wengi sana"

Tulisubiri takriban dakika tano akiwa anaongea na simu na mtu, ambapo ilionekana wazi ni mwandani wake, au mtu fulani wa nasaba yake aliyemuudhi sana katika jambo fulani huko mtaani kwake!
Kwa kuisoma tu hali aliyokuwa nayo huyo 'mganga' nilipata shaka kama angeweza kutoa tiba sahihi!

Sasa wanajamvi ninachotaka tujadili ni ishu ya mahusiano ya UMRI wa mganga na KAZI anayoifanya!
Je, kwa vile kidada kama kile kimemaliza shahada yake pale MUCHS, na kikafaulu vizuri kwenye makaratasi yake, basi kianze kazi, huku kikiwa na ma'frustration ya wachumba, na kinabipiwa kila dakika kikiwa kazini, au je labda umri wa daktari kuanza kazi uwe stipulated kwenye maadili ya uganga?
 
Age is just a number, though sishauri mtoto wa under 18 atumike hapa, kuna watu wana miaka zaidi ya 50 lakini utendaji wao ni mbovu kupita maelezo, tena utakuta sometimes wanaingia kutabibu huku wamelewa ua wana frustration kibao za familia, la maana hapa ni hao madaktari wawe na maadili ya kazi ili kuweza kutoa huduma nzuri na kwa kiwango husika, ukizingatia hii sekta ni sensitive sana.
 
Umri sio hoja bali kinachotakiwa ni usisitizaji/usimamiaji wa maadili. Hata hivyo, mwanafunzi anayeanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka 6 huwa daktari kamili (baada ya internship) akiwa na umri usiopungua miaka 25. Huu si umri mdogo kwa kuanza kazi ya udaktari.
 
PJ...

tatizo laweza lisiwe ni umri, tatizo kubwa na preservice trainings zetu ambazo haziwekei mkazo wajibu, nafasi na matarajio ya kazi tunazosomea. Huyo binti nimfano tu, wako wengi balaa, si majeshini, mashuleni, viwandani na service sector

Sababu nyingine kwenye hizi public instituion ni culture vijana wanayoikuta na hii husababisha kudhani that is the way of life. inasikitisha sana
 
Ndio sana mkuu. Huyo dr ni uakisi wa watendaji wa umma kwa ujumla. Unapoona dola inayumba usitegemee sekta nyingine zilizo chini ya dola zinaweza kuwa imara. Imarisha bunge, mahakama, serikali na [vyombo vya habari] uone kama kuna zege italala. Hakuna mtu atakayechezea kazi kwani dr akileta mchezo ikaleta madhara mahakamani then Ukonga, Keko, Segerea. Vinginevyo huyo dr wala haoni kama ni tatizo
 
Pole PJ
Ndiyo nchi yetu ilivyo. No standards. Siku moja nilikuwa na shida ya kumwona DC katika Mkoa mmoja kanda ya Kaskazini nilishangaa kukuta binti kajikwatua/kajiremba kama anakwenda kwenye shindano la u miss au kama amepanga kwenda disco baada ya kazi. Huyo ni Mkuu wa Wilaya ambaye anapigiwa saluti na Makamanda wa jeshi Wilayani humo n.k. Inasikitisha sana.
 
Age is just a number, though sishauri mtoto wa under 18 atumike hapa, kuna watu wana miaka zaidi ya 50 lakini utendaji wao ni mbovu kupita maelezo, tena utakuta sometimes wanaingia kutabibu huku wamelewa ua wana frustration kibao za familia, la maana hapa ni hao madaktari wawe na maadili ya kazi ili kuweza kutoa huduma nzuri na kwa kiwango husika, ukizingatia hii sekta ni sensitive sana.

Kama ndivyo unataka kunambia kwamba bado dhana ya 'Uganga Ni Wito' bado inahold?
Maana kama Umri hauna tija, na pia kama MAADILI ya kazi yapo, kinachosababisha shida hizi ni nini!
 
Pole PJ
Ndiyo nchi yetu ilivyo. No standards. Siku moja nilikuwa na shida ya kumwona DC katika Mkoa mmoja kanda ya Kaskazini nilishangaa kukuta binti kajikwatua/kajiremba kama anakwenda kwenye shindano la u miss au kama amepanga kwenda disco baada ya kazi. Huyo ni Mkuu wa Wilaya ambaye anapigiwa saluti na Makamanda wa jeshi Wilayani humo n.k. Inasikitisha sana.
ulipita lushoto nini?

angalia usijewekwa kwenye rada mazee

binafsi sijali amevaaje as long as anatimiza majukumu yake ipasavyo
 
Pole PJ
Ndiyo nchi yetu ilivyo. No standards. Siku moja nilikuwa na shida ya kumwona DC katika Mkoa mmoja kanda ya Kaskazini nilishangaa kukuta binti kajikwatua/kajiremba kama anakwenda kwenye shindano la u miss au kama amepanga kwenda disco baada ya kazi. Huyo ni Mkuu wa Wilaya ambaye anapigiwa saluti na Makamanda wa jeshi Wilayani humo n.k. Inasikitisha sana.

Pole na wewe mkuu!
Naamini mtu kama Mkuu wa Wilaya ni mtu anayetafutwa kwa shida kubwa wastani zinazohitaji mtu very rational, na mwenye ujuzi na aliyeona situations nyingi za kiutendaji maishani ili aweze kusizolve!
Sasa anapokuwa ni kidada kilichovaa hivyo, bila shaka anaweza ku'divert wazo la msingi kichwani mwako, ukakuta unawaza mengineyo, na pia inapofikia wakati wa kutoa maamuzi mazito kiutendaji nina shaka kama atajiamini!...huh!
 
Jana nilimpeleka mgonjwa wangu Hospitali ya Mount Meru akiwa na shida inayohusiana na allergy.

Lakini nilikatishwa tamaa na mganga niliyemkuta kwenye chumba kimojawapo nilichoelekezwa!
Kwa ufupi mganga huyo ni kisichana kidogo kabisa(around 25) ambacho hakijui wala kujali maana ya mtu kuumwa au kuugua, mapozi meengi na maneno ya mkatomkato!
Nilipodadisi niliambiwa kuwa "HAWA NI KIZAZI KIPYA, wameajiriwa juzijuzi mwanzoni mwa mwaka, na wako wengi sana"

Tulisubiri takriban dakika tano akiwa anaongea na simu na mtu, ambapo ilionekana wazi ni mwandani wake, au mtu fulani wa nasaba yake aliyemuudhi sana katika jambo fulani huko mtaani kwake!
Kwa kuisoma tu hali aliyokuwa nayo huyo 'mganga' nilipata shaka kama angeweza kutoa tiba sahihi!

Sasa wanajamvi ninachotaka tujadili ni ishu ya mahusiano ya UMRI wa mganga na KAZI anayoifanya!
Je, kwa vile kidada kama kile kimemaliza shahada yake pale MUCHS, na kikafaulu vizuri kwenye makaratasi yake, basi kianze kazi, huku kikiwa na ma'frustration ya wachumba, na kinabipiwa kila dakika kikiwa kazini, au je labda umri wa daktari kuanza kazi uwe stipulated kwenye maadili ya uganga?

Labda Muhimbili kuna matatizo. Kitoto cha sister nacho kimemaliza muhimbili, kina mapozi hata cm hakipokei kisa kiko busy!! lakini kabla kilikuwa kikija nyumbani kupiga 'mkuki'( kuomba pesa ya kujikimu)
 
Duh... Nyange umesema neno ambalo ni zito sana

Kuna attitude fulani ya watoto waliosoma MUHAS aisee... iko noted sana hasa na sie wazee-vijana!!! Nadhani kuna kitu hakiko sawa... NI bora ukutane na mtaalam wa fya aliyesoma India, Russia, China, Cuba, Europe yote au hata america...

In short ni waliosoma MUHAS ndio wana matatizo zaidi
 
PJ

tatizo sio hospitali tu, kila kona ya nchi kuna uozo wa aina yake. Tusiwalaumu sana vijana kwa sababu hawa vijana wanapoanza kazi, wanawakuta wazoefu wanafanya utumbo kuliko hata huo wanaoufanya wao. na vijana wanafikiri ule ndio ujuzi unaotakiwa kuuonyesha kazini.

kuanzia walimu, madaktari, tra, mpaka wabunge na mawaziri hakuna anaejua sheria na kanuni pamoja na wajibu wake kazini.

hilo ndio tatizo linalotukabili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom