Profesa Sospeter Muhongo ni kweli kwamba hujui watanzania wanahitaji Tanesco ya namna Gani?

Wild fauna

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
461
189
Kuna matangazo kwenye luninga na magazeti yanayohusu Tanesco.
Hili tangazo linawataka watanzania kuwapa ushirikiano wafanyakazi wa tanesco pindi watakapopita kukusanya maoni ya wao wanahitaji tanesco iweje?
Tangazo linauliza Je unataka TANESCO IWEJE?.
Wametoa mawasiliano mbali mbali kama e mail adress,facebook KEY WORK (TANESCO IWEJE) ili kutuma maoni jinsi tanesco unavyotaka iwe.
My take: hivi hawa viongozi wa tanesco hawajui watumiaji wa umeme wanataka nini? Au hizi ndio mbwembwe tu za huyo waziri?
Watu wanahitaji huduma bora na bei nafuu thats all.
 
Kwanini sekta ya umeme ina tanesco pekee? Ifanyike kama mashirika ya simu yawepo makampuni mengi ya kufua umeme nchini ili kuwe na ushindani wenye tija.
 
Nani alitoa hilo wazo la door to door questioning? TANESCO hawajui umuhimu wa scientific research? Na watauliza watu wangapi? 200, 40m?
 
Eti mgao utakuwa historia, labda kwa nchi nyingine bt sio TZ yetu hii iliyojaa wachakachuaji
 
Profesa muhongo mie nahitaji ile tanesco ya akina Ngeleja na muhando.
 
Duh!! amaaa kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo. Yaani ni mwendo wa mbwembwe mwanzo mwisho. KWANI MALENGO YA TANESCO KUANZISHWA YALIKUWA NINI??? INA MAANA PROF. MZIMA HAJUI HILO??? HAKUNA MAKABRASHA OFISINI??? Au anataka tumshauri namna ya kupitisha nyaya za umeme kama iwe underground au iendelee tu hii ya nguzo hadi nguzo huku nguzo moja ikiuzwa milioni moja??? Itabidi nifanye mpango nione wameomba mapendekezo kwenye maeneo gani hasa, lakini bado nashindwa kuelewa umuhimu wa hili zoezi??? huyu si anasema yeye yupo kivitendo zaidi na si kisiasa???
 
kwenye luku mnatuibia kwani luku ikifungwa kila mwezi unachajiwa 3500 je mkataba huo sio wa kifisadi? Pili kwanini mnatuunganishia umeme kwa bei kubwa sana?. Ebu tubadilishie huu mfumo wa kiwizi!!
 
kuna mengi sana ya kurekebisha tanesco yaliyo wazi kabisa kabla ya kutaka maoni ya wateja.
Tatizo viongozi wengi wanapenda ujiko hata ktk majukumu yao ya kawaida.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom