Profesa Muhongo: Sitaomba radhi kwa wezi

mgomba101 Mimi nilishasema humu JF kuwa kama ni kuomba radhi wangeanza kuombana radhi wabunge wenyewe kwa vile wao wenyewe walitajana kwa majina kuwa fulani amekula, iweje ripoti ina taarika kwamba waonewa? Waziri weka hadharani siku hiyo na hatutakubali ujiuzulu kwa sababu ya hao mafisadi.

hatataja chochote tumeshawazoea kujitutumua wakikutana na press ila wakienda bunge kimyaa!
 
Hivi wakweli na wapenda Taifa lao hapa Tanzania wataishi wapi?.
Kwa sasa ukionekana unatetea ukweli hapa Tanzania ni jamabo la hatari kwa maisha yako.
 
Hii ndiyo CCM ukweli mwiko! Professor hana cha kupoteza awaachie CCM uozo wao. Hajaomba ubunge, alionekana anafaa na anafaa. Kama hawataki ukweli achane nao. Majina ya wabunge waliooomba rushwa kutoka wizara yake aliwapa viongozi wa Bunge. Nadhani alifanya utaratibu mzuri tu vinginevyo Bunge lingempa nafasi awataje. Mbona hakupewa hiyo fursa? Mbona Bunge halikuwataja?

Kuhusu mgawo wa umeme watanzania tuwe na subira.Yako masuala mengi ya kuangalia kama vile misuguano ya kimfumo katika uendeshaji na utawala kutokana na mabadiliko katika sekta ya umeme, miundombinu mibovu ya kurekebisha na kuongeza, pamoja na kuongeza uzalishaji ambayo yatachukua muda. Tumpe waziri Muhogo ushirikiano. Naamini wenye nia njema hufanikiwa
 
Wakikulazimisha kuwaomba radhi hao wezi, tafadhali linda heshima yako na mapenzi kwa nchi yako kwa kuwaachia kazi yao!! Prof. Muhongo wewe huna dhiki bali unachofanya ni mapenzi kwa nchi yako na juu ya hayo wewe ni mtaalam unaeweza kupata ajira popote duniani; hawa vilaza wasikunyime usingizi!!!
Pamoja na nia nzuri aliyonayo nayo Prof Muhongo, lakini alichosahau ni kuwa mfumo wa CCM sasa ni kulinda wala rushwa, na wale watu wema wanaoitakia mema nchi hii, watatengengenezewa kila aina ya zengwe na ikibidi wanaweza wakakunyunyizia vikemiko kwenye kitaulo cha kujifkama walivyomfanyia ..
 
ndio utajua tanzania ina watu wa aina gani kweli mwizi aombwe msamaha tena. Kweli hata ningekuwa mimi nisigeomba milele Prof. usikubali utaidhalilisha taluma yako
 
“Kamwe sitaomba radhi kwa wezi. Subirini muone na kusikiliza kwenye kikao kijacho cha Bunge nitakachoongea kwa muda wa hizo dakika tano wanazotaka kunipa niombe radhi,”
Prof huu mkwara tuu, msamaha
ataomba hata nyuma ya pazia. tangu mwanzo alikua anawafaham wezi lakini hakuwataja kwa sababu ya kuwaogopa. Ile ilikua zamu yake now its their turn akileta ubishi hata amini aise.
 
Safi sana Prof Muhongo, waonyeshe kwamba wewe hubabaiki na wezi, wala rusha wakubwa.
 
Muhimu atoe ushahidi. Kama hana itabidi aombe radhi au awajibike. Kama ushahidi anao kweli itabidi kamati iwajibike kwa nini hawakuutumia huo ushahidi. Sound bites peke yake hazitatosha. Credible evidence is needed and the professor knows the importance of evidence in making such huge attributions.

1. Juzi na jana Mwenyekiti wa CCM (T) ambaye pia ni Rais wa Tz, katika vikao vya chaguzi za UWT na UVCCM alieleza kuwa, kuna watu wananunua uongozi na kura zinauzwa. Kwamba kuna watu wanatumia rushwa na kuna makundi ya wanaowania Urais ujao; akawaasa wajumbe wasiwapigie kura watu hao. Sasa wewe msomi, Mkumbo kamwambie na Rais Kikwete atoe ushahidi wa rushwa na au hayo makundi vinginevyo aombe msamaha.

2. Baada ya hicho kikao cha Bunge kuahirishwa, katika kipindi cha dakika 45 kwenye ITV, Mh. Job Ndugai (Naibu Spika) alisema waziwazi kuwa kulikuwa na sababu zaidi ya moja zilizosababisha kuvunjwa Kamati ya Bunge inayosimamia Wizara ya Nisahati na Madini. Moja wapo ni kuwa Wabunge wenyewe ndani ya kamati walikuwa wanalalamikiana kwa kuwatuhumu wenzao ndani ya kamati hiyo kuhusika na vitendo vya rushwa. Sasa kawambie na hao Wabunge waombe msamaha, kabla ya kumwambia Mh. Job Ndugai na pia Mh. Anna Makinda naye athibitishe ni akina nani hao waliokuwa wakilalamika la sivyo nao waombe msamaha kwani haiwezekani katika kadamnasi ya waelewa katika Bunge zima la nchi, Waziri mmoja ‘kichaa' akaibuka na kusema kuna harufu ya rushwa halafu Spika avunje tu Kamati kwa kauli hiyo ya mtu mmoja bila kujiridhisha na yaliyosemwa au kuwepo sababu nyingine za kimazingira au vinginevyo.

3. Julai 14, 2012 saa 10.00 jioni, Dr. Mkumbo ulisema kuwa Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigullu Nchemba ni mzinzi. Je uliweza kupeleka mahakamani ushahidi wa uzinzi? Basi kama hujawahi kutuonesha jinsi ulivyokuwa ukishuhudia kwa kupiga chabo au CCTV footage ulizokuwa umetegesha tendo la uzinzi wa mtu au kuwashawishi Mh. Mwigulu na waliyekuwa wakizini naye wenyewe wakiri kuwa ni wazinzi basi omba msamaha. Wewe Mhadhiri, Mzamivu wa Saikolojia, utajidharirisha sana Dr. Mkumbo kudoubt anachosema msomi mwenzako simply kwa kuwa wewe uko CHADEMA na yeye CCM katika suala zito la rushwa inayoitafuna nchi yetu ambalo kwa ushahidi wa kimazingira vinadhihirisha wazi pasi na shaka kuwa rushwa ipo Tanzania. Waziri Sosper alisema na kuwataka baadhi (sio wabunge wote) wenye migongano ya kimaslahi na TANESCO & Wizara wasifanye hivyo, alisema pia kuwa Mkurugenzi Mhando alikuwa anafanya biashara na mkewe ndani ya TANESCO, alisema pia kuwa kuna waliokuwa wanaiba umeme kupitia vishoka na akataja hata Shule za akina Mchungaji Lwakatare n.k, alisema pia wazi kuwepo kwa hujuma za kutunga migao ya umeme (power rationing) kwa kisingizio cha uhaba wa uzalishaji wa nishati jambo ambalo ni tofauti na kukatwa umeme tokana na uharibifu au ukarabati wa miundombinu katika baadhi za sehemu. Hayo yote hayakusemwa na Mawaziri waliopita wala Viongozi wa kamati za bunge akina Mh. Makamba au rafiki yako Mh. Zitto ambao yeye alibaki kumsifia na kumtetea Mhando kuwa ni msafi na mahesabu ya vitabu vya TANESCO kuwa ni masafi. Nawe unaingia kichwa kichwa unaunga mkono mafisadi eti oh leta ushahidi katika jambo la wazi kama hili?

4. Kwa vile wewe ni mshauri ndani ya CHADEMA, mweleze vile vile Mh. Lissu atoe ushahidi ndipo uamini akiyoyasema ambapo yeye hata aliwataja Wabunge waliohusika katika tuhuma za rushwa na za migongano ya maslahi. Usiniambie kuwa Lissu ni kilaza kiasi kile cha kusikia tu eti Waziri anasema bungeni halafu yeye naye akakimbia faster mbele ya TV na na ‘kucut na kupaste' tuhuma just kwa sababu zimesemwa na Waziri.

5. Hivi majuzi nilikusifu ukuongoza kongamano zuri UDSM la kumenzi Baba wa Taifa Nyerere. Sasa mbona baba wa Taifa, J. K Nyerere kwa shahidi tu za kimazingira kasema mara kadhaa kuwa nchi yetu inanuka rushwa au kuwa serikali ni corrupt. Na sijawahi kukusikia ukisema kuwa huamini aliyosema Nyerere maana hakutoa ‘hard evidence' za kuwepo rushwa. Sasa naamini yule kijana aliye kukumbusha kuwa Wahadhiri wengine hamufanyi tafiti na kuandika papers, ni kweli! Nakukumbusha kuwa, Nyerere alieleza kuwa dalili za serikali corrupt, ni kutokusanya kodi; hakusema kuwa ni Mkurugenzi T, tarehe U, saa V aliyeonekana katika surveillance camera W, akipokea Tsh. X, wakiwepo askari Y na Afisa wa Takukuru Z.

Sasa huu ni mfano mzuri sana wa jinsi ambavyo watu wenye maadili na uthubutu wanaweza kuona mbali kwa utafiti wa kimazingira na kusema hapa kuna rushwa kama vile mazingira aliyoyaona huyu Profesa wa ukweli Sospeter lakini akina viegeugeu Zitto wakawa wanazunguka usiku kucha wakizuia Mhando asichukuliwe hatua.


Msomeni kiona mbali, Carl Sagan, Astronomer akitamka, "Absence of evidence is not evidence of absence!"

Waziri Sospeter hakuna kuomba radhi wala hakuna ku regret whatsoever! Mh. Spika unda Kamati nyingine na watuhumiwa wasogezwe kwenye vyama vyao. Mh. Kikwete wale Mawaziri na Watendaji wakuu wengine wanaolala na kuamka business as usual na kukuita tu Dr. Dr. bila mpango fukuza! Wanaochakalika bila uwoga kama huyu Sospeter (ambaye ni wewe ulimleta in the first place) na anaonekana kusimamia maadili na maendeleo wape support ya nguvu, maana hawa ndiwo watakaoiokoa CCM (kama inaokoka) wala sio UVCCM maana hawa Mawaziri na Makatibu wakuu ndio wasimamizi wakubwa wanaoweza kuhakikisha kuwa kero za wananchi zinapungua na viwango vya maisha ya wananchi vinapanda. Wananchi hawajali uprofesa wake wala ustadi wa kuomba miongozo bungeni bali wanataka kuona nguzo na bili za umeme zinapungua kwa mwananchi wa chini, umeme unawaka wakati wote, wachimbaji wadogo wanawezeshwa, mikataba yote inakuwa wazi na iwe ya kumfaidisha Mtanzania zaidi ya mwekezaji. Mambo kama haya ndiyo darubini yetu kwa huyu Profesa. Akianza kukatishwa tamaa tu, mafisadi nao (bila kujali itikadi za vyama) wanaanza kupeperusha bendera zao. Hii ni karne nyingine hatukubali kupotoshwa!
 
Babykailama:

Hayo yote uliyoeleza ni sawa katika mazungumzo ya kawaida. Lakini ukitaka kumtia mtu hatiani ni lazima upeleka ushahidi wa kushikika. Tume iliyoundwa ni kama mahakama. Huwezi kwenda mahakamani ukatoa maneno ya jumlajumla kama hayo uliyoeleza hapo juu ndiyo yatoshe kumtia mtu hatiani. Kumbuka makosa ambayo Profesa Muhongo amewatuhumu wenzake ni ya kuwafukuzisha ubunge na wakienda mahakama ikathibitika wanafungwa. Katika utawala wa sheria hakuna shortcut. Yeye kama kweli walimwomba rushwa ana ushahidi anao kwa nini asiutoe?

Hata mimi kwa hiyo issue ya Mwigulu ambaye umei-cite hapo juu ipo mahakamani na kesi inaendelea. Na sasa hivi sina sababu ya kujetete kwenye social media kama nilimtukana au ala, kwa sababu sasa tupo katika chombo chenyewe hasa na ukweli utajulikana hukumu itakapotoka. Ni mahakama pekee inayoweza kuthibitisha kama nilimtukana mhe MN au la, hakuna mwingine. Nakualika uendelee kufuatilia hiyo kesi na inaanza kusikilizwa rasmi tarehe 5 Novemba.

Narudia tena katika utawala wa sheria hakuna njia ya mkato ili utende haki. Tatizo letu watanzania sasa hivi tunapenda mno njia ya mkato katika kila jambo, hatutaki kuhangaika. Na kwa kuwa wanasiasa wetu wanapenda sifa za haraka haraka ndiyo hivyo tena wanatumia udhaifu wetu kupiga maneno barabarani ili tuwapigie makofi. Na wala mie sitetei wala rushwa, nawachukia na kuwalaani sana hasa inapokuja swala la viongozi. Lakini vilevile napinga sasa tabia unayoibuka ya kuwatuhumu na kuwahukumu watu barabarani, na kukataa kutumia vyombo halali katika kuthibitisha au kukanusha tuhuma zao. Hatuwezi kujenga nchi ambapo kila mtu ni hakimu, tutakuwa tunaingia kwenye the Republic of the Jungle, na baadhi yetu hatutaki tufike huko!
 
Chezea wizara ya vigogo wewe!Unataka kuyumbisha nchi kwa kusema ukweli!Peleka uprofesa wako shule huko waachie wenye kujua ulaji waendeleze harakati zao!Wizara imeshindikana hiyo ina wakubwa wengi mno!Pole ndugu yangu Prof. ukitaka tukuunge mkono kwa maandamano sie tuko tayari vijana wa nyerere!ambao mpk leo tunatembea na azimio la arusha!
 
Kitila Mkumbo- quoted:

Hayo yote uliyoeleza ni sawa katika mazungumzo ya kawaida.


Rais wa nchi kasema kuna rushwa mbele ya vyombo vya habari katika chaguzi za UVCCM & UWT ni mazungumzo ya kawaida? Naibu spika alisema katika kipindi cha dakika 45 ITV (tafuta huo mkanda) kuwa Wabunge wenyewe wa hiyo kamati walitoa lawama kuwa miongoni mwao kuna waliopokea rushwa ni mazungumzio ya kawaida?
Mh. Lissu alizungumza kwa kuwataja mafisadi wenye maslahi binafsi kuhujumu TANESCO & Wizara ni mazungumzo ya kawaida?
Nilikuuliza kuwa mara nyingi unamtolea mfano baba wa Taifa Nyerere kuwa mwadilifu alipokuwa wazi kuzungumza kuwa nchi inanuka rushwa, je alitoa ushahidi wa namna unaousema au nawe uwa unatuletea mazungumzo ya kawaida Nkurumah Hall?



Tume iliyoundwa ni kama mahakama.

Umesema vema kuwa ni kama mahakama lakini si mahakama. Mahakama gani uliona inatoa hukumu wakati yenyewe ni tuhumiwa? Aidha kama huwezi hata kupima legitimacy ya mfumo wa kutoa haki ambapo unakuta eti Gosbert Blandes ndiye anatengemewa humo kutoa haki basi na wewe utakuwa na matatizo makubwa sana ya uchambuzi wa mifumo ya kutoa haki.


Huwezi kwenda mahakamani ukatoa maneno ya jumlajumla kama hayo uliyoeleza hapo juu ndiyo yatoshe kumtia mtu hatiani. Kumbuka makosa ambayo Profesa Muhongo amewatuhumu wenzake ni ya kuwafukuzisha ubunge na wakienda mahakama ikathibitika wanafungwa. Katika utawala wa sheria hakuna shortcut. Yeye kama kweli walimwomba rushwa ana ushahidi anao kwa nini asiutoe?

Bungeni pamekuwa mahakamani? Kwa taarifa yako kama kuna mtu ameumia kutokana na kauli za Prof. yeye ndiye sasa aende mahakamani ashitaki kuwa amekashifiwa kama ambavyo wewe unavyoshitakiwa kwa kosa la kumuita Mh. Mwigulu kuwa ni Mzinzi hadharani.

Pili huwezi kumsemea Prof. kuwa alisema kijumlajumla alipoitwa na kuhojiwa maana mimi nawe hatukuwepo unless nawe umekutana na Blandes mapema. Lakini nikukumbushe tena kuwa kuvunjwa kwa kamati kusingetokana na mtu mmoja tu (Waziri) kuwatuhumu baadhi ya Wabunge. Unajifanya kuwa husomi kauli ya Naibu Spika akieleza wazi kuwa kulikuwa pia na wabunge tena wa ndani ya kamati hiyo ya Nishati na Madini ambao walilalamika. Tatu angalia sana Mhadhiri usijechichora, unafikiri kazi ya kuwatia hatiani mafisadi ni ya yule pekee anayejaribu kutoa taarifa juu ya hao mafisadi? Let you be assured kuwa kwa tabia hiyo ndio maana mafisadi wataendelea kupeta maana TAKUKURU, POLISI na wananchi wenye tabia kama yako mnaokaa pembeni na kusema haya ‘alete ushahidi sasa tuone' hata pale mnaposhuhudia mazingira ya rushwa nyote ni janga la Taifa!

Nakuuliza kuwa kuna vyombo gani vingine vya dola (TAKUKURU na Polisi) wamesha waita hao wote waliotuhumiwa au kutuhumu na kuwaprobe kwa kina na kufuatilia nyendo za hao watuhumiwa siku hizo na hata mawasiliano yao kwa kutumia mbinu za kipelelezi za hali ya juu zilizoko katika nchi yetu hata na za kuazima? Hivi unafurahia tu unaposikia vyombo vya wenzetu wameibua skandali kubwa zilizokuwa zimefichika ambazo zimefanywa na wakubwa hata miaka mitano hata kumi iliyopita? Unafikiri matokeo yake huwa yanapatikana kirahisi rahisi kwa kuwaita watu kwenye kamati ya bunge ambayo hata ndani mwake kuna watu vihiyo na walaghai kama Blandes? Kama tuna vyombo na wananchi serious wanaotaka kupambana na rushwa kweli, basi watu kama Prof. Sospeter, Mh. Lissu kwenye mukhtadha huu wanatumika kama whistle blowers, na vyombo husika vinaanzia hapo ku dig deeper hata kwa kurejea maamuzi mbalimbali yaliyofanywa, nyendo za hao watuhumiwa pamoja na wale Magabachori waliojaa Dodoma, financial transactions zilizofanywa kutoka TANESCO au kwa watuhumiwa kutoka akaunti zao za benki na hata kupitia mitandao ya simu, mikutano na makutano yaliyokuwa yakifanywa katika mahoteli siku zile kabla ya kuwasilishwa bajeti ya hii Wizara, uchambuzi na tafsisri ya taarifa mbalimbali kutoka kwenye media za aina zote ziku zile nk. Je hiyo tume ilifanya hayo? Mwalimu Mzamivu Mwandamizi wa Saikolojia, Mkumbo, ukiamua kuchunguza tuhuma ya rushwa, hakuna short cut! utapaswa kuzama katika forensic intelligence na siyo kuita tu watu wachache na kuwauliza maswali kama vile mko kwenye interviewing panel ukategemea kuwa huo ndio uchunguzi kamili wa tuhuma za rushwa!

Narudia tena katika utawala wa sheria hakuna njia ya mkato ili utende haki. Tatizo letu watanzania sasa hivi tunapenda mno njia ya mkato katika kila jambo, hatutaki kuhangaika.
Na kwa kuwa wanasiasa wetu wanapenda sifa za haraka haraka ndiyo hivyo tena wanatumia udhaifu wetu kupiga maneno barabarani ili tuwapigie makofi.

Nami narudia msomeni kiona mbali, Carl Sagan, Astronomer akitamka, "Absence of evidence is not evidence of absence!" na ni kweli Mkumbo unaonekana hupendi kuhangaisha kichwa chako tumeshakuona maana unawaona Prof. Sospeter na Mh. Lissu kuwa type ya wanasiasa wanaopiga maneno barabarani na kumuona mwanasiasa mtuhumiwa kigeugeu Zitto aliyekwenda kuchukuwa riporti kwa Blandes hata kabla haijatoka kuwa ndio wanasiasa wa kupigiwa makofi! Umenisikitisha sana mwalimu wangu na uki-coordinate kongamano lingine Mlimani nitakukumbusha tena jinsi ambavyo mnapenda short cut kwa kutojishughulisha kufanya tafiti za kisayansi na kuziandika.
 
Amethubutu kwa kweli PROF. Big up lakini tumeona viongozi wengi wakithubutu tuu kusema maovu wanaishia katikati hawatufikishi mwisho wa tukio lenyewe sasa tunabaki kujiuliza ni nini hatma ya kila kitu katika nchi hii ,eti ndio mkakati wakauweka wa kuwaambia wananchi watoe maoni yao wanataka Tanesco ijiendeshe vipi,jamani hivii wanaoihujumu tanesco mnawajua sasa ni vipi mnataka maoni ya wananchi,maoni ni kwamba watu wawajibishwe kwa kutolewa sehemu hizo walizopo walizovurunda ,nachelea kusema kwamba msituchoshe wananchi kwa kuwaambia wachangie mambo ambayo yako waziiiiiiiiii kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,tuko bize na mchakato wa katiba tunaomba utulivu.
 
*Mimi simuungi mkono huyu Professor Muhongo kwa sababu ni mnafiki sana. Hana tofauti na kina Sitta, Mwakyembe, Kilango na Ole Sendeka kwenye issue ya Richmond, ukweli wote wanaujua halafu wanatuonjesha tu, mwingine wanabaki nao mioyoni mwao na kuuzika chini halafu wanataka sisi raia tuwaunge mkono!!

*Wakati anatoa hoja hii bungeni watu wengi tulimtaka ataje majina ya wabunge waliohusika na namna wanavyohujumu TANESCO ila yeye akakataa katakata akidai suala hilo anamwachia Spika Makinda na kamati ya wabunge wa CCM.

*Tumuache akaangwe na mafuta yake mwenyewe, hii ndio dawa ya mnafiki kama huyu, na sasa nawasiliana na mbunge wangu kumtaka apeleke hoja binafsi bungeni kushinikiza kujiuzuru kwa huyu waziri kutokana na kitendo chake cha kulidanganya bunge.

watanzania sijui uwafanye nini? hizi standard za kutaja majina umezitoa dunia gani? kila taifa lina protocol zake za uendeshaji serikali, huu ushabiki wako wa kijinga wa mtaani haupo kwenye practical realities za utendaji wa kazi kubwa serikalini. Kama ulipata kuangalia bunge la UK wakati wa scandal ya ufisadi wa perks za wabunge, hamna mtu alitajwa jina, ila wenyewe walijipima na wakaresign. Na hii ni UK supposedly imeendelea zaidi kwa uwazi na demokrasia. Unataja majina mbele ya kadamnasi tu pale unapotaka cheap popularity kwa sababu taratibu ni kumkabidhi kiongozi mkuu wa maadili ya bunge (spika) majina hayo au unayapeleka mahakani kufungua kesi au utataja pindi unapotakiwa kuyataja na chombo ambacho kitakua na mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria.

Hata Mwakyembe na tume yake hakutaja majina ila ofisi za wahusika na wale waliojipima na kuona wamekosa walijiuzulu.

Big up Sitta, Mwakyembe, Muhongo kwa kujaribu kua wazalendo ndani ya mazingira magumu ya kinafika ya watz.


mungu ibariki Tanganyika
 
Mzee Concrete!
Amedanganya wapi? Kutokutaja majina ndiyo huko unakokusema kuwa n ni kudanganya? Kwako wewe kipi kinaonekana kuleta uzito zaidi na tija, kutotajwa majina na Waziri au Waziri kutangaza kuwa hapatakuwepo na mgawo wa umeme tena katika nchi yetu? Anyway sisi wengine wapitaji tu,...., mwenye nguvu mpishe,..., nchi yenu hii, wengine tupo hapa kama observers, hatuna letu,...., mnachoamua nyie wengine hatuna hata chembe ya nguvu ya kukizuia, WASILIANA NAYE MH. MBUNGE WAKO APELEKE HIYO HOJA, ili ufurahi na roho yako!

Mkuu naona haujanielewa.
Tetesi zinasema kamati ya bunge iliyoundwa haikukuta chochote chenye ukweli katika yale aliyoyasema bungeni!!! (yaani hakuna wabunge wanaofisadi TANESCO!!), sasa basi kanuni za bunge zifuate mkondo wake. Lengo langu ni;
1/Kumfundisha kuacha unafiki(Kuogopa kusema ukweli wote)

2/Kumshinikiza kuja hadharani sasa japokuwa amechelewa kusema ukweli wote anaoujua kuhusu Ufisadi ndani ya Tanesco
 
Mkuu jenga hoja au bomoa hoja ya mtu kwa hoja. Watu hatuogopi kusema ukweli katika lolote. Ni ajabu kujaribu kuhusianisha hili na Pro-Lowassa.
 
Mwanaume unapokuwa na haraka, wanawake wanapunjika sana wanaishia kukudharau halafu mnawalaumu.
Do you think retreats is surrendering? or do you think buying time is equal to not knowing what to do? never!!!!
Bado sijakupata mkuu.
I don't understand if the problem is the language or the context?
Funguka zaidi tukupate vema.
 
Hata mimi ka labtop changu kamekaribia kukatika chaji kwasababu jana na juzi kumetokea mgao
 
watanzania sijui uwafanye nini? hizi standard za kutaja majina umezitoa dunia gani? kila taifa lina protocol zake za uendeshaji serikali, huu ushabiki wako wa kijinga wa mtaani haupo kwenye practical realities za utendaji wa kazi kubwa serikalini. Kama ulipata kuangalia bunge la UK wakati wa scandal ya ufisadi wa perks za wabunge, hamna mtu alitajwa jina, ila wenyewe walijipima na wakaresign. Na hii ni UK supposedly imeendelea zaidi kwa uwazi na demokrasia. Unataja majina mbele ya kadamnasi tu pale unapotaka cheap popularity kwa sababu taratibu ni kumkabidhi kiongozi mkuu wa maadili ya bunge (spika) majina hayo au unayapeleka mahakani kufungua kesi au utataja pindi unapotakiwa kuyataja na chombo ambacho kitakua na mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria.

Hata Mwakyembe na tume yake hakutaja majina ila ofisi za wahusika na wale waliojipima na kuona wamekosa walijiuzulu.

Big up Sitta, Mwakyembe, Muhongo kwa kujaribu kua wazalendo ndani ya mazingira magumu ya kinafika ya watz.


mungu ibariki Tanganyika
Mkuu usitake kutupotosha kwa makusudi.
*Hakuna sheria iliyokuwa inamkataza kutaja majina ya wahalifu au kumwaga ushahidi hadharani.
Mbona wahujumu wengine wa TANESCO ambao sio wabunge aliwatajwa kwa majina na uhusika wao? Why double standard?

*Hali ya nchi yetu unaiona jinsi ilivyo sasa, Tume ni kitu cha kuchelewesha, kuficha na kupotosha ukweli. Huwezi kulinganisha na UK, USA.
Kwa tulipofikia ni kumwaga mchele kwenye kuku wengi ndio Protocol zingine zifuate.

*Sasa ushahidi wake huko kwenye tume alikong'ang'ania kuufichia umegonga mwamba, vipi sasa tena anataka kurudi kwenye njia aliyoikataa awali ili tumtetee?
 
Back
Top Bottom