Profesa Muhongo: Sitaomba radhi kwa wezi

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameapa kuwa kamwe hataomba radhi bunge kwa madai aliyotoa dhidi ya watu aliowatuhumu kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambao amewafananisha na wezi.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi juzi, Profesa Muhongo alisema yote aliyoyasema kwenye kikao cha Bunge la Bajeti kilichopita ni sahihi na ana ushahidi wa kutosha kuthibitisha tuhuma hizo.
“Kamwe sitaomba radhi kwa wezi. Subirini muone na kusikiliza kwenye kikao kijacho cha Bunge nitakachoongea kwa muda wa hizo dakika tano wanazotaka kunipa niombe radhi,” alisema Profesa Muhongo.

Alitoa kauli hiyo alipotakiwa kuzungumzia kuvuja kwa ripoti ya Kamati ya Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan Ngwilizi iliyoundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kuchunguza tuhuma za rushwa kwa wabunge zilizosababisha Kamati ya Nishati na Madini kuvunjwa.

Taarifa hizo za kuvuja kwa ripoti hiyo zinaeleza kuwa, Kamati ya Ngwilizi imependekeza Waziri aombe radhi na Katibu Mkuu wa wizara yake, Eliakim Maswi achukuliwe hatua za nidhami na mamlaka zilizo juu yake.
“Yaani watu waibie taifa, tuwagundue na kuwasema, halafu nisimame kuowaomba radhi? Sitafanya hivyo. Sitaki kuzungumza mengi, lakini Watanzania wasubiri kauli yangu siku jambo hilo litakapowekwa hadharani,” alisisitiza Profesa Muhongo.

Awali, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kikao cha Mawaziri wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuhusu mkakati wa kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme nafuu katika nchi hizo, Profesa Muhongo alisema hakuna na kamwe hautatokea tena mgawo wa umeme nchini.

Aliwataka wenye kuombea mgawo wa umeme utokee nchini kubadilisha maombi yao, kwani jambo hilo halitatokea tena kutokana na mikakati iliyowekwa na serikali kuongeza uzalishaji kupitia gesi asilia, mafuta na maji.

Alitaja vyanzo vingine vya uzalishaji umeme vinavyoendelea kufanyiwa kazi hivi sasa, kuwa ni makaa ya mawe, umeme jua, joto ardhi na mabaki ya mimea kama miwa ambayo imegundulika kuzalisha umeme.

Akitoa takwimu za uzalishaji umeme alizopokea juzi asubuhi katika utaratibu wake wa kupokea taarifa ya uzalishaji mara tatu kwa kutwa, Waziri huyo alisema zilizalishwa megawati 355.40 kwa kutumia gesi, 170
kwa mafuta na 110 kwa maji.

Alisema hadi sasa uwezo wa juu wa uzalishaji umeme nchini ni megawati 1,348 kwa siku wakati mahitaji ya ni megawati 830.

Waziri huyo alienda mbali kwa kuwataka wanaokwenda Makanisani, Misikitini au sehemu yoyote ya Ibada kuomba mgawo wa umeme utokee nchini wabadilishe maombi yao kwa sababu hayatasikilizwa.

Alitaja tatizo na changamoto pekee inayoikabili Wizara yake na Tanesco kuwa ni miundombinu ya kusambaza umeme unaozalishwa ndiyo maana nguvu kubwa sasa imeelekezwa kwenye uboreshaji wa miundombinu ili kila
Mtanzania mwenye kuhitaji umeme mijini na vijijini apate huduma hiyo.

Hivi sasa wanaopata huduma ya umeme nchini ni zaidi ya asilimia 18 ya Watanzania wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 40 milioni.

Waziri Profesa Muhongo alisema idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka mara dufu kati ya sasa hadi 2017 baada ya miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia, jua, mabaki ya mimea na joto ardhi itakapokamilika.

Alisema Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzindua mradi mkubwa wa kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka Mnazi Bay-Dar es Salaam.
 
Profesa nakuunga mkono 100% hakuna kuomba radhi mafisadi,wezi,mijitu ya hovyo hovyo.Tena inabidi wao ndio wakuombe radhi wewe.Big up profesa.
 
Wakikulazimisha kuwaomba radhi hao wezi, tafadhali linda heshima yako na mapenzi kwa nchi yako kwa kuwaachia kazi yao!! Prof. Muhongo wewe huna dhiki bali unachofanya ni mapenzi kwa nchi yako na juu ya hayo wewe ni mtaalam unaeweza kupata ajira popote duniani; hawa vilaza wasikunyime usingizi!!!
 
mgomba101 Mimi nilishasema humu JF kuwa kama ni kuomba radhi wangeanza kuombana radhi wabunge wenyewe kwa vile wao wenyewe walitajana kwa majina kuwa fulani amekula, iweje ripoti ina taarika kwamba waonewa? Waziri weka hadharani siku hiyo na hatutakubali ujiuzulu kwa sababu ya hao mafisadi.
 
Last edited by a moderator:
Hii ndio Tanzania msioijua basi somo hilo hapo juu. Tume, tume na kila siku tume lakini matokeo yake yanatia kinyaa. Tume ya Chimbi, tume ya Hassan Gwilizi hii yote ni CCM kulindana na kutotaka kuchafuka zaidi. Hapakuwa na Aja ya kuunda tume bali Mahakama ingefanya kazi kwani taarifa za kuaminika zilikuwepo na zipo kuhusu haya Majizi . Tume ni moja Tanzania iliyotoa majibu yasiyokuwa na mashaka nayo ni tume ya mweshimiwa MWAKYEMBE.
Waziri wew si MWANASIASA simama kwenye ukweli maana, hao wanasiasa uluiokupendekeza hizo ndo tabia zao za kuficha ukweli.
Watanzania Ifike wakati tukatae uundwaji wa hizi tume UCHWARA kwani ni kuhujuma KODI zetu kwa kuunda TUME zisizo na TIJA kwa TAIFA.
Waziri wewe ni msafi kataa kuomba radhi na wakikulazimisha basi kuwa tayari kuchukua maamuzi magumu kulinda heshima yako.
 
wakileta za kuleta, rudi mliman kafundishe. tatizo la wanasiasa wa tanzania wanafanya kazi kwa kuindana. mbona kabala ya kuteuliwa kwake waziri tayari akina zitto walikuwa busy kuandaa mazingira ya mgao? baada ya waziri kuingioa, mbona hatuwasikii? siasa mbaya sana
 
Kutoomba radhi nakubaliana na Prof. Mhongo 100%.

Lakini hilo la mgao sikubaliani maana kwa tafisiri nyepesi mgao ni ukosefu wa nishati ya umeme pale unapouhitaji. Sasa iwe ni ukame, mvua, miundombinu nk ukikosekana mi nadhani huo unaitwa mgao (na hasa ukizingatia historia ya miaka 10 ya Tanzania).

Akili yangu hainiruhusu kufikiri kama kuna uhalali kwenye sababu ya miundo mbinu (au nyingeneyo) kwa sababu kama Wizara kwa miaka yote hiyo ilikuwa ikitengeneza migawo feki......mimi nitaendelea kutilia shaka jibu lolote lenye kujaribu kuhalalisha ukosefu wa umeme nchini.
 
mgomba101 Ifike hatua tuache kudhalilisha taaluma za watu,big up sana Pro.heshima lazima ichukue mkondo wake
 
Last edited by a moderator:
hakuna kuomba radhi
yaani watuibie na radhi tuwaombe,huo ni ujuha,Prof komaa nao,ni wezi tu hao,hawaitakii mema nchi hii.
 
*Mimi simuungi mkono huyu Professor Muhongo kwa sababu ni mnafiki sana. Hana tofauti na kina Sitta, Mwakyembe, Kilango na Ole Sendeka kwenye issue ya Richmond, ukweli wote wanaujua halafu wanatuonjesha tu, mwingine wanabaki nao mioyoni mwao na kuuzika chini halafu wanataka sisi raia tuwaunge mkono!!

*Wakati anatoa hoja hii bungeni watu wengi tulimtaka ataje majina ya wabunge waliohusika na namna wanavyohujumu TANESCO ila yeye akakataa katakata akidai suala hilo anamwachia Spika Makinda na kamati ya wabunge wa CCM.

*Tumuache akaangwe na mafuta yake mwenyewe, hii ndio dawa ya mnafiki kama huyu, na sasa nawasiliana na mbunge wangu kumtaka apeleke hoja binafsi bungeni kushinikiza kujiuzuru kwa huyu waziri kutokana na kitendo chake cha kulidanganya bunge.
 
wakileta za kuleta, rudi mliman kafundishe. tatizo la wanasiasa wa tanzania wanafanya kazi kwa kuindana. mbona kabala ya kuteuliwa kwake waziri tayari akina zitto walikuwa busy kuandaa mazingira ya mgao? baada ya waziri kuingioa, mbona hatuwasikii? siasa mbaya sana

Kwakuongezea hapo mkuu,,,sio siasa tu bali NJAAA MBAYA SANA, HAWA VIJANA WANANJAAA NA SIASA ZAO NI ZA KUFAIDISHA MATUMBO YAO
 
Napenda viongozi wazalendo kama hawa wakikukaba sana piga chini ka kazi kao mkuu!

Hana uzalendo wowote huyu. Uzalendo wa kweli ilitakiwa kuuonyesha siku ile ile wakati anasoma budget yake bungeni kwa kumwaga kila kitu hadharani sio kutufichaficha baadhi ya mambo.
Sasa zamu yake kukaangwa kwa mafuta yake.
 
Namfahamu sana Prof. Muhongo. Kama amesema hivyo, nina uhakika hataomba radhi, hata kama kitendo hicho kitagharimu nafasi yake. Ni mtu anayependa sana kutafiti, na kama alisema kuna wizi/rushwa ni lazima ana uhakika wa hilo. Prof. ni mchapakazi kwelikweli, na siyo mtu wa kubembeleza.

Profesa nakuunga mkono 100% hakuna kuomba radhi mafisadi,wezi,mijitu ya hovyo hovyo.Tena inabidi wao ndio wakuombe radhi wewe.Big up profesa.
 
Mtu yeyote akishakua ndani ya ccm tusitegemee lolote la kushangaza zaidi ya majungu tu kwenye magazeti
 
Ukiona mambo magumu yanatokea like mapendekezo ya taarifa za kamati za bunge yanakataliwa waziwazi namna hii, kifo cha Mwangosi, RPC fataki, Ikulu kutiwa kidole na Dr. Uli then that is the start of the long journey to the promised land..!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwa nini hakuwataja kutoka mwanzo hao anaowatuhumu kuwa ni wezi?

Prof Muhongo anaweza kuwa ni kiongozi mzuri na msafi lakini katika hili na yeye amejiingiza katika siasa zile zile za kihuni za chama chake na wanaweza kumkaanga kweli asipokuwa mwangalifu...
 
Tanzania pekee ni majaabu saba ya dunia,na waziri nikusikia unaomba radhi utatufanya tuwe namba moja kwa hayo maajabu!
 
Ila mh waziri hapo kwenye mgao wa umeme bado sijakuelewa,mimi ninaishi nyakato mecco mgao upo sana toka,ijumaa usiku,jumapili toka saa moja asbh hadi jioni,jana umekatika asbh na tumelala kiza na hadi ninavyoandika hamna umeme nyakato mecco mwanza hakuna umeme!!
 
Back
Top Bottom