Profesa Kikula: Niko tayari kujiuzulu

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Profesa Kikula: Niko tayari kujiuzulu
Tuesday, 11 January 2011 20:42

Habel Chidawali, Dodoma
MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Idrisa Kikula, amesema kitendo cha wahadhiri wa chuo hicho na wanafunzi kuanzisha mgomo, huenda kuna ajenda ya siri nyuma yao.

Kufuati hatua hiyo, Profesa Kikula alisema msalaba alionao ni mkubwa, hivyo yupo tayari kumwachia mtu yeyote kama atapatikana ili naye aweze kujitwisha kama wahadhiri hao wataona inafaa kufanya hivyo.

Profesa Kikula alitoa kauli hiyo jana ikiwa ni siku moja baada ya wanafunzi wa chuo hicho Kitivo cha Elimu, kuanzisha maandamano hadi Ofisi ya Waziri Mkuu Mjini hapa.

Hata hivyo, kauli ya Profesa Kikula ingekuwa ni lulu kwa wanachuo na wahadhiri wao kama ingetolewa na Profesa Shaaban Mlacha, ambaye ni Mkuu Kitengo cha Fedha na Utawala, kwani wahadhiri na wanachuo wengi wamekuwa wakimlalamiki kuwa chanzo cha migogoro yote.

Akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari jana, Profesa Kikula alisema mgomo baridi ulioanzishwa na wanachuo hao na wahadhiri, sio tatizo kubwa ambalo linaweza kumfanya amuite Rais Jakaya Kikwete kama wengi wanavyodai.

"Tatizo sio kubwa kama linavyochukuliwa na wengi, bali ni mambo ambayo tunaweza kuyamaliza ndani ya chuo sisi wenyewe, bila ya kumuita hata rais kama ambavyo watu wanataka," alisema.

Alisema wao kama uongozi wa chuo, watakaa na taasisi zinazohusika na masuala ya urekebishaji mishahara kwa upande wa wafanyakazi chuoni hapo, kama rais atahitaji taarifa uongozi utafanya hivyo, lakini syo lazima kwenda chuoni hapo.

Kuhusu suala la migogoro ya uongozi, Profesa Kikula alisema iwapo kutajitokeza watu na kudai hawana imani na yeye, basi hatasita kuitisha baraza la chuo waeleze wanayemtaka kuwaongoza.
 
Ninafikiri kama unataka kujiuzulu fanya hima ila acha domo weye........sisi tumechoshwa na madebe yasiyo na tija...................
 
Aisee,This is serious!! So why not that way!!!?
 
Tatizo ni jina lake la mwanzo linamponza na ajenda asemazo zipo na ndio zimeanza kufanya kazi nchi nzima kwa sasa.
 
Huyu Prof Kikula sounds very geniune and forthright kwasi kwamba anaonyesha kutokua na cha kuficha na ndio maana hata utayari wa kuwajibika hauko mbali sana endapo kutakwepo na haja.

Ila kuna mwingine nilisoma taarifa zake humu, anajiita MaMkwe, kila kitu anachokisema kimejaa ukakasi. Sina uhakika kama ndiye huyu mwingine, nanihii Prof Shaabani Mlacha.

Na kama huyu ndiye yule yule aliyejiita hapa jf kama MaMkwe basi haswa nilivyomsoma kauli zake na hoja zake za nguvu, ndiye mbaya wao UDOM famili nzima. Huenda huyu bwana aki-STEP ASIDE tu na mambo nyoookaaaa!!!
 
Aachie ngazi nae jk plus mwema and ngeleja wafuatie kuachia ngazi hatutaki wazembe humu.
 
Mwambie Deputy wako Mlacha ajiuzuru kwanza, yeye ndio ana makamasi kichwani, fisadi, kidampa asiye na CV ya kuwa DVC-Planning Finance and Admnistration, Profesa kilaza aliyepewa uDVC sababu ya ushemeji na Kikwete, nna wasiwasi hata huo uprofesa wake aliupataje. Mlacha asipojiuzulu, next time Mkapa au Kikwete wanakuja UDOM wataambulia kuzomewa na mawe juu. MARK MY WORDS!

Kumbe kuna ka-ushemeji tena hapo?? Aaaahhh, ndio kiburi kile kile cha msichana wa kazi nyumbani kwake waziri na ni waziri tu kiaina, toba basi akawapishe tu wenzake ili familia hiyo ya UDOM wakae kama ndugu tena katika haki na ufanisi zaidi bila mizengwe ya sijui 'unanijua mimi nani katika nchi hii' vile.
 
Sijawahi kuona mtu anataka kujiuzulu kwa kutoa taarifa kwanza ili kujiuzuru kufuate. Hapa unatafuta kuhurumiwa wala si nia ya kujiuzulu. Usitishie kujiuzulu,jiuzulu kama wewe sio tatizo basi ukikutwa u msafi utaombwa uendelee,acha woga!
 
Aisee,This is serious!! So why not that way!!!?

Hata hivyo, kauli ya Profesa Kikula ingekuwa ni lulu kwa wanachuo na wahadhiri wao kama ingetolewa na Profesa Shaaban Mlacha, ambaye ni Mkuu Kitengo cha Fedha na Utawala, kwani wahadhiri na wanachuo wengi wamekuwa wakimlalamiki kuwa chanzo cha migogoro yote.
 
Kosa sio la Kikula....kazi ipo kwa Mlacha...amabe analindwa na shem wake si wajua jamaa ameweka vilaza wenzake kila sehemu?????sasa pale ndio kazi ilipo mwingine Mwema nae shem sasa atamfuta kazi??maana issue arusha aibu kubwa sana kwa yeye kuendele kuwepo hadi leo
 
Japokua SHABAN MLACHA ndio sumu kali chuoni hapo na ndiye anayetakiwa kuachia ngazi mapema kabla hajaondolewa na nguvu ya umma ya wana udom, bado prof kikula na prof kinabo hawawezi kukwepa zigo hilo la tuhuma kwa sababu wamemuacha mlacha atambe atakavyo na hata kuingilia majukumu majukumu yao bila kumhoji. Zaidi ya hapo viongozi hao wote watu wa juu pamoja na mkurugenzi wa rasilimali watu na muhasibu wanahusika kwa pamoja na ufisadi uliotokea chuoni hapo..
 
Huu ushemeji shemeji huu ndio ulio tufikisha kwenye mauaji ya raia pale A-town sasa tena na UDOM? haihitaji kuwa na Degree kujua utawa huu sio bora ..........
 
Kosa sio la Kikula....kazi ipo kwa Mlacha...amabe analindwa na shem wake si wajua jamaa ameweka vilaza wenzake kila sehemu?????sasa pale ndio kazi ilipo mwingine Mwema nae shem sasa atamfuta kazi??maana issue arusha aibu kubwa sana kwa yeye kuendele kuwepo hadi leo
kwani hiki chuo kiko US?
 
Hivi Mlacha anawezaje akaathiri haki za walimu. Nilidhani vyuo, ikiwamo UDOM wana clear institutional administrational stucture and functions. Kama wasomi hawajui hili na kuanza kupersonalise madai kwa moja ya viongozi, nadhani tatizo litakuwa kubwa kwa vijana wanakuwa produced hapo.

Kwa mfano, maamuzi ya mwisho ya kifedha, mipango na utawala kwa ujumla hayako chini ya DVC admin. Labda mtu aniambie pesa za malipo na madai mengine yanatoka kwenye mfuko binafsi wa Kikula au Mlacha.
 
Back
Top Bottom