Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 733
Chanzo chetu cha habari kilieleza kwamba msanii huyo anayeheshimika na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, alikamatwa na askari akiwa na mdogo wake aitwaye Wilfred Haule na rafiki yao aitwaye Robert Mugisha wakati wakiwa njiani kuelekea Kijitonyama, nyumbani kwa msanii mwingine wa Bongo fleva aitwaye Hamis Mwinjuma au maarufu kama Mwana FA.
Imedaiwa kuwa Profesa J na wenzake wakiwa ndani ya gari lenye namba za usajili CA 196-748, aina ya BMW, waliligonga gari jingine ambalo namba zake hazikuweza kupatikana mara moja wakati wakiwa njiani kuelekea Kijitonyama na baada ya kusababisha ajali hiyo, polisi waliwaona na kutaka kuwaweka chini ya ulinzi, lakini Profesa J na wenzake walikataa kutii amri na kuanza kucharuka, hali iliyowalazimu polisi kutumia nguvu.
Habari zinadai katika purukushani hiyo ya aina yake, Profesa J na wenzake walionekana kutaka kuwazidi nguvu polisi na kutaka kumnyanganya mkuu wa kituo silaha, hali iliyowalazimu polisi kufyatua risasi hewani. Licha ya kuwatisha kwa kufyatua risasi, lakini bado walikataa kusalimu amri na kukataa kuwekwa chini ya ulinzi, ndipo polisi walipopiga simu kwa wenzao kuomba msaada.
Muda mfupi baadaye gari la polisi Defender liliwasili eneo la tukio likiwa na askari wengine, na kufanikiwa kuwakamata Profesa J na wenzake kisha kuwapeleka hadi Kituo cha Polisi cha Kijitonyama, ambapo walifunguliwa jalada la lenye namba KJN/2257/2010, kwa kosa la kujaribu kunyanganya silaha.Hadi tunakwenda mitamboni msanii huyo alikuwa korokoroni.
Source: Globalpublisherstz.com