Profesa Haroub Othman afariki duniya

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,323
inna lillahi wainna illaihi rajihunna
marehemu profesa haroub othman miiraji

profesa haroub othman, mmoja wa wahadhiri waandamizi wa chuo kikuu cha dar es salaam, amefariki dunia asubuhi hii huko unguja akiwa usingizini.


marehemu amekutwa amefariki asubuhi hii ambapo jana alilala akiwa buheri wa afya.


habari toka unguja zinasema marehemu profesa haroub othman usiku wa kuamkia leo alihudhuria uzinduzi wa tamasha la majahazi (ziff) katika ngome kongwe na hakuonekana na matatizo yoyote kiafya.


msiba uko nyumbani kwake sehemu za michenzani eneo la baraste, jumba namba 4 kwenye kona ya mbonde telecom (kibanda cha kupigia simu )na haijajulikana kama atazikwa lini. Habari za mazishi yake tutawalete mara zitapopatikana.

 
INNA LILLAHI WAINNA ILAIHI RAJIHUNNA.

Hakika tumepoteza msomi, mwanaharakati na mtaaluma mzuri sana. Hakika kwa sisi tunaofahamu na kusoma na kufatilia paper zake tuna majonzi makubwa.

Hakika alisaidia sana katika mambo mengi toka pale UDSM wakati wa BCOM na hata PhD yangu.

hakika yeye ametangulia nasi tupo nyuma yake.

Dr Hamza Yousuf Al Naamani
Safarini Znz
 
Goooossssssshhhhh!!!!!!!!

RIP Prof. Moja ya nguzo muhimu sana ya Wasomi na Wanataaluma wa Tanzania waliokuwa na udhubutu wa kulisemea jambo lolote bila kumwogopa mtu toka enzi zile . . .

Hakika kila nafsi itaonja mauti . . .
 
Ni loss kubwa kwa wanaharakati na wanataaluma hapa nchini. Pumzika kwa amani Profesa.
 
Mungu amlaze mahali pema Prof Haroub Othman, sisi wanafunzi wake wa DS pale UDSM tutamkumbuka sana.
Kwa hakika Watanzania tumepoteza kichwa cha nguvu.
Kazi ya Mungu haina makosa.
 
Mod tunaomba hii post ingeunganishwa na ile nyingine kwenye jukwaa la siasa...!
 
Inalillah wainaillah rajioun.
naona thread ilitakiwa iwe eneo la siasa kwani marehemu alikuwa nguli kwenye mijadala ya kisiasa na mustakabali wa nchi yetu.
 
Marhum Prof Haroub Othman Miiraj atazikwa hapo kesho na maiti itatokea baraste.

Inna lillahi wainna ilaihi rajihuna.

Dr Hamza Yousuf Al Naamani.
Znz
 
Rip prof, kwa kweli bado hoja zako na upeo wako ulikuwa unahitajika sana, bwana alitoa na bwana ametwaa
rip prof
 
R.I.P Prof. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
 
Back
Top Bottom