Mhache
JF-Expert Member
- Jun 20, 2008
- 345
- 24
Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Haroub Othman amefariki dunia leo alfajiri. Hizi ni taarifa nilizozipata kwenye TBC One. Kifo hiki ni pigo kubwa kwa wanasiasa na wanafunzi wa chuo hicho. Kifo hiki kimenigusa kwani alikuwa mmoja wa walimu wangu wakati nikisoma chuoni hapo. Ninachoweza kusema ni kwamba tulimpenda sana Profesa Haroub Othman lakini Mungu alimpenda zaidi. Mungu ailaze roho ya Profesa Haroub Othman mahali pema peponi.