Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni; aanza kwa kasi!

Nampenda huyu Mama kwa kuwa makini katika utendaji wake, lakini naiomba Serikali impe ulinzi wa hali ya juu.
 
Mmiliki Palm Beach amvimbia Tibaijuka Wednesday, 15 December 2010 20:46

prof%20anna%20tibaijuka.jpg
Nora Damian
MMILIKI wa kiwanja kilicho jirani na hoteli maarufu ya Palm Beach iliyoko jijini Dar es Salaam ambaye Serikali imemtaka abomoe ukuta wake kwa kuwa ni eneo la wazi, ametishia kumshtaki Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akidai kuwa analimiki eneo kihalali.

Mmiliki huyo alikutana jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa anakusudia kumshtaki Waziri Tibaijuka kwa kuwa ameidharau Mahakama.

Mmiliki huyo, Taher Muccadam alisema Waziri Tibaijuka amedharau amri ya mahakama kwani alishinda kesi mahakamani na kuruhusiwa kuendelea na ujenzi katika kiwanja hicho.

Alisema kiwanja hicho namba 1,006 kilichopo Upanga anakimiliki kihalali na kwamba ana uthibitisho na vielelezo vyote vinavyomhalalisha kumiliki eneo hilo.
"Tibaijuka awe makini sana, hasa anapotaka kufanya maamuzi. Anaweza akaisababishia hasara Serikali kwa kulipa fidia,"alisema Muccadam.

Alisema eneo hilo si kiwanja cha wazi bali ilipendekezwa tu lakini, baadaye Manispaa ya Ilala ilitoa hati namba 186164/25 kwa wamiliki wa kwanza ambao ni Shantaben Narottambahi Patel na Nilaben Girishumar Patel mwaka 1975.

Alisema Desemba 6, 1975, Wizara ya Ardhi iliwazuia wamiliki hao kukiendeleza kiwanja hicho kwa sababu kilitakiwa kiwe cha wazi na kwamba waliahidiwa kiwanja mbadala namba 1019 kama fidia.

Muccadam aliendelea kueleza kuwa lakini, kiwanja hicho namba 1019 walichotakiwa kupewa wamiliki hao, kilichukuliwa na kumilikishwa kwa AMREF.

"Baadaye wizara iliamua kuwaruhusu waendeleze kiwanja chao cha zamani kwa kuacha upana wa futi 20 kati ya barabara ya Magore na Upanga.

Katika mkutano huo Muccadam alionyesha vielelezo mbalimbali kuhusu kiwanja hicho, ikiwemo barua ya Kaimu Kamishna wa Ardhi F. Luvanda yenye kumbukumbu namba LD/75708/101/LK ya Mei 25 mwaka 2005.

Katika barua hiyo, Kamishna huyo alipendekeza kuwa ili kumaliza mgogoro huo, kiwanja hicho kigawanywe na wamiliki wapate sehemu ya kuendeleza kwa matumizi ya ofisi na hoteli na eneo lingine libaki wazi.

Kwa mujibu wa Muccadam, tayari amemwandikia barua Waziri Tibaijuka kumjulisha suala hilo lakini hakuijibu barua hiyo wala hataki kukutana naye.

Alisema alinunua kiwanja hicho ili ajenge jengo la ghorofa 22, lakini tangu wakati huo, ameshindwa kuanza ujenzi kutokana na kuwepo kesi mbalimbali mahakamani kubishania kiwanja hicho.

Muccadam alisema mwaka 2000, kiwanja hicho kilifutwa kwa makosa, hivyo suala hilo lilipelekwa Mahakama Kuu na kufunguliwa kesi namba 70/2004 na baadaye Wizara ya Ardhi ilipendekeza mgogoro umalizwe nje ya mahakama.

Alisema aliendelea na malumbano hayo Mahakama Kuu kwa muda wote huo na hatimaye alishinda kesi na kurudishiwa kiwanja hicho na kwamba mahakama ilikubali alipwe fidia ya dola za Marekani 6 milioni kama gharama za ujenzi huo.

Katika hatua nyingine mmiliki wa kiwanja namba 1072 kilichoko Upanga Magharibi jijini Dar es Salaam kinachodaiwa kuwa hakina sifa ya kuwa kiwanja, amedai kuwa waziri Tibaijuka amedanganywa na watendaji wake kuhusu umiliki wa kiwanja hicho.

Paul Anthony aliliambia gazeti hili jana kuwa alipewa ‘ofa' ya kiwanja hicho na wizara ya Ardhi tangu Januari 24, 1989 na kwamba ameendelea kukilipia kodi hadi leo.

Alisema kiwanja hicho kiko katikati ya viwanja viwili vilivyopimwa vya Salender Bridge Club na uwanja wa shule ya Muntazir lakini, kiwanja chake hakijapimwa hadi leo.

"Mkurugenzi wa Makazi ana ajenda ya siri juu ya kiwanja changu na jana (juzi) alimdanganya Waziri,"alieleza Anthony.

Alisema kabla ya kutakiwa kupewa hati, wizara ilimtaka kwanza atoe maelezo ya tathmini ya athari za mazingira kuhusu Mikoko iliyoko nje ya kiwanja hicho na alifanya hivyo.

Mmiliki huyo alionyesha vielelezo mbalimbali zikiwemo barua zilizoandikwa na J. Kombe kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (Nemc) na ile ya Mali Asili na Utalii iliyoandikwa na Dk Tango kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

Barua hizo zimeeleza kuwa kiwanja hicho kiko nje ya msitu wa mikoko na kwamba mradi unaotaka kutekelezwa hautakuwa na madhara yasiyoweza kudhibitika.

Barua hizo zilielekeza upimaji wa kiwanja hicho usisitishwe kwa kigezo cha kuharibu mikoko kwani kiwanja chenyewe hakina mikoko.

Alisema pia mchoro wa mipango miji namba 1/504/569 Dar es Salaam Area 2 ambako ndiko kiliko kiwanja chake bado haujaidhinishwa hali inayochangia kuchelewa kupimwa kwa kiwanja hicho.
Juzi Waziri Tibaijuka alitoa siku 30 kwa wananchi waliojenga nyumba kwenye maeneo ya fukwe ya Bahari ya Hindi kuzibomoa kabla ya kuanza kuchukua hatua.

Akizungumza katika ziara ya kukagua hali ya makazi na mipango miji katika jijini la Dar es Salaam jana, Waziri Tibaijuka alisema viwanja vya Serikali vilivyokuwa wazi haviruhusiwi kuwa makazi watu kwa kuwa viwanja hivyo ni kwa ajili ya michezo na bustani za kupumzika wananchi wa maeneo husika.

"Nasikitika kusikia kuwa wananchi wanaoishi hapa wamenunua maeneo haya. Hivi viwanja si vya watu ni vya Serikali na kila aliyenunua anapaswa kubomoa na kurudisha kiwanja kwa wahusika," alisema Profesa Tibaijuka.

Alisema miongoni mwa viwanja hivyo ni eneo la wazi lililopo Ocean Road ambalo lilikuwa linamilikiwa na Shree Hindu Mandal, kiwanja namba 59 kitalu 1 kilichokuwa kinatumika kuchomea maiti mwaka 1952 mpaka 1967 na kuhamishiwa Kijitonyama na kutaka eneo hilo lilirudi mikononi mwa serikali.

Alisema katika hali ya udanganyifu Shree Hindu Mandal waliibuka na kudai mabadiliko ya matumizi ya kiwanja hicho na baadaye kupewa kibali na rais cha kutaka matumizi ya awali yafutwe na msajili alikifuta kwa nyaraka namba 131942 ya Septemba 2 mwaka huu kisha kuagiza manispaa ya Ilala ivunje ukuta uliopo.

Katika eneo jingine lililopo Palm Beach kiwanja namba 1006 ambalo lilikuwa la matumizi ya wazi mwaka 1975 kabla ya kubatilishwa kuwa eneo la mtu binafsi mwaka 2002 na mpaka sasa kinamilikiwa na mtu huyo.

"Mtu hawezi akajenga kwenye eneo la serikali kubwa kama hili wakati wananchi wanaoishi katika maeneo haya hawana sehemu ya kupumzikia wala sehemu ya watoto kucheza. Hii ni hujuma na wahusika wanapaswa kuchukuliwa hatua," alisema Tibaijuka.

Alisema kiwanja namba 1072 kilichopo eneo la Upanga ambacho ni cha nyongeza, kilibuniwa pasipo kufuata utaratibu. Alisema kiwanja hicho kiko eneo la mikoko na hakijawai kupimwa rasmi.
 
SAKATA LA VIWANJA DAR


Tibaijuka akwaa kisiki

*Maagizo aliyotoa juzi kurudisha maeneo yapingwa
*Wahusika watumia barua Ofisi ya Rais kujitetea
*Wasema Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye alibariki
*Watishia kumburuta mahakamani endapo atavunja uzio
*Yeye asema hakukurupuka, atasimamia maamuzi yake


Na Grace Michael
SIKU moja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kuamuru kuvunjwa ukuta wa kiwanja
namba 1006 kilichopo Palm Beach jijini Dar es Salaam kuna kila dalili za kuibuka sakata la mgogoro katika kiwanja hicho ukihusisha Ofisi ya Rais Ikulu na watendaji katika wizara yake akiwemo Mkurugenzi wa Mipango Miji.

Ofisi ya Rais imetajwa kuhusika katika sakata hilo kwa kutoa maelekezo kwa Wizara kutekeleza amri ya mahakama ambayo inampa uhalali Bw. Taher Muccadam kuwa ni mmiliki halali wa kiwanja hicho na pia apewe hati miliki mpya kumiliki eneo hilo na aruhusiwe kuzungusha uzio na kupewa kibali cha ujenzi.

Maelezo ya malalamiko ya Bw. Muccadam kwa Ofisi ya Rais yanathibitishwa kupitia barua yenye kumbukumbu namba CEA 157/638/IV/01 ya Juni 2, mwaka jana iliyosainiwa kwa niaba ya Katibu wa Rais na G.M. Masaju ikiwa na kichwa cha habari kisemacho 'Ucheleweshaji wa kutekeleza uhuru wa sheria katika kiwanja namba 1006 Upanga'.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Bw. Muccadam alisema kuwa atamfikisha mahakamani Prof. Tibaijuka endapo atavunja uzio wa kiwanja chake bila kutengua amri halali ya Mahakama Kuu iliyopo na atafanya hivyo kwa kuwa ana uthibitisho wa vibali vyote vya ujenzi na amevipata kihalali.

"Tibaijuka asipokuwa makini ataingia kwenye scandal (kashfa) mapema, asikurupuke katika maamuzi kwa kuwa ataifanya Serikali kuingia kwenye gharama kubwa za ulipaji fidia," alisema Bw. Muccadam.

Alisema kuwa mbali na Ofisi ya Rais kutaka amri ya Mahakama itekelezwe, Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye alishauri kutekelezwa kwa amri ya mahakama baada ya Wizara kuomba ushauri kwake.

"Kwanza eneo hilo si la wazi kama wanavyosema bali ilipendekezwa tu lakini baadaye Manispaa ilitoa hati kwa wamiliki wa kwanza kwani eneo hilo lilipaswa kuchukuliwa na AMREF...je kama hao wangejenga wangewabomolea?" Alihoji.Alisema Kamishna wa Ardhi ndiye mwenye mamlaka makubwa ya ardhi kwa kuwa ana uwezo wa kumshauri Rais kubatilisha lakini baada ya kuona uhalali wa kiwanja hicho, alisaini hati ya kiwanja 1006 kilichopo Upanga.

Akizungumzia suala la hati hiyo kubatilishwa na Rais Mkapa kama Prof. Tibaijuka alivyoelezwa na wataalam wake, alisema kuwa si kweli kwamba Rais yupo juu ya sheria kwa kuwa nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria na Katiba ya nchi, ndio maana hata wakati akila kiapo aliapa kuilinda katiba na sheria za nchi.

"Kwa misingi hii ndio maana Mahakama ilitoa uamuzi huo kwa kuwa ubatilishwaji haukufuata taratibu husika," alisema.Mbali na hayo, pia Bw. Muccadam alimtaka Prof. Tibaijuka kufuatilia uhalali wa upatikanaji wa kiwanja namba 305 ambacho ni kiwanja jirani na kiwanja hicho ambacho kimeamuriwa kuwa eneo la wazi kwa kuwa taratibu za tenda hazikufuatwa.

Barua nyingine ambayo nakala yake Majira linayo, imeelekezwa kwa Mrungenzi wa Manispaa ya Ilala ambayo ilisainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo yenye kumbukumbu namba CA87/01/52 ya Septemba 28 mwaka jana ambayo inatoa maelekezo ya kugawanywa kwa kiwanja hicho ili kupatikana sehemu ya kuegesha magari na ikaruhusiwa ujenzi wa jengo la ghorofa kumi kwa matumizi ya makazi.

"Mchoro namba 1/504/369 inaonesha mgawanyo wa kiwanja tajwa umeidhinishwa na Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Septemba 25, 2009, kiwanja hicho kilichogawanywa kwa kufuata amri ya mahakama, imepatikana sehemu ya kuegesha magari na ujenzi wa jengo la ghorofa kumi," ilisema sehemu ya barua hiyo.

Majira lilipowasilina kwa njia ya simu na Prof. Tibaijuka kutaka ufafanuzi kuhusu kauli ya Bw. Muccadam, alisema kamwe hawezi kubadili msimamo wake katika kushughulikia sakata hilo, ndio maana wakati anatoa amri hiyo alikuwa na wataalam wote wa Wizara akiwemo Mkurugenzi wa Mipango Miji.Alisema kuwa endapo mlalamikaji anaona ana haki, watakutana mahakamani kwa kuwa mahakama zipo kwa ajili ya kutoa haki kwa pande zote mbili na haijalishi kama ni Serikali.

"Niseme tu kwamba sikukurupuka na siwezi kukurupuka katika uamuzi wowote na katika hilo naona hana haki hata kidogo kwa kuwa hana hati halali ya eneo hilo na kama ameruhusiwa ni kinyume cha sheria hivyo sitabadili uamuzi wangu," alisema Prof. Tibaijuka na kuongeza;

"Ndio maana wakati nafanya maamuzi hayo sikuwa peke yangu, nilikuwa na Katibu Mkuu, Wataalam wengine wa wizara, Naibu Waziri wangu na wadau wengine hivyo nitahakikisha nasimamia uamuzi wangu kwa ajili ya Watanzania," alisema Prof. Tibaijuka.
 
je muccadam ana right of occupancy kwa jina lake? na mabadiliko ya matumizi ya hicho kiwanja yalifanyika lini? maana 1975 ilionekana kwamba kibaki wazi, sasa kama walihaidiwa kupewa kingine ambacho amref wamechukua basi wao wanaweza kupewa hicho cha ahadi sehemu nyingine ya mji, kama hawataki basi waende wanako ona kunawafaa.
na huyo wa mikoko naye analipia kiwanja ambacho hakija pimwa? kisa majirani zake viwanja vime pimwa? hii ni dhahiri rushwa imetumika kuanzia kwa huyo kamishana, mpaka mwanasheria mkuu wa serikali, hii inataka kufanana na kesi ya dowans wala rushwa kuacha kupeleka ushahidi wa kutosha au makini ili ushindi uende kwa mtu wanaye mtaka.
 
Kwani matumizi ya open space hayaangukii katika masuala ya Public Good ambayo yanampa uwezo Rais kurevoke whatever right alizopewa mtu binafsi. Na kama siyo hivyo ni kwanini hatuna sheria ya kurevoke haki zote za watu binafsi katika viwanja ambavyo vilipangwa kwa matumizi ya umma na kubadilishwa. Wote tunajua kuwa hakuna mtu anayepata kiwanja kilichowahi kuwa kwa matumizi ya umma bila ya kuhonga, iwe madiwani ama mabwana ardhi wilayani ama hata makao makuu. Sasa kama suala ni uwezekano wa serikali kulipishwa fidia kutokana na uzembe wa watumishi wake na tamaa za hao waliomilikishwa, kuna ugumu gani wa kutunga sheria kuwezesha waziri kuwachukulia hatua na kurudisha maeneo haya kwa matumizi ya umma?
 
hivi raisi akibadili matumizi ya ardhi si inatakiwa itangazwe kwenye gazeti la serikali? na kama ni hivyo je hili suala lilitangazwa? na je haya matatizo ya kuwaaingiza mjini viongozi ni sa tatuliwe kwa kuongezea kwamba masuala kama haya yapitishwe kwenye kamati za bunge kama husika ili kuwepo na kuangalia masilahi ya taifa yanaangaliwa
 
Namshauri Tibaijuka abomoe vya Mahanga kwanza halafu amwombe Mahanga ampe list hiyo atafaulu, fasta tu maana mahanga atafurahi kuona tunakosa wote
 
Kwani matumizi ya open space hayaangukii katika masuala ya Public Good ambayo yanampa uwezo Rais kurevoke whatever right alizopewa mtu binafsi. Na kama siyo hivyo ni kwanini hatuna sheria ya kurevoke haki zote za watu binafsi katika viwanja ambavyo vilipangwa kwa matumizi ya umma na kubadilishwa. Wote tunajua kuwa hakuna mtu anayepata kiwanja kilichowahi kuwa kwa matumizi ya umma bila ya kuhonga, iwe madiwani ama mabwana ardhi wilayani ama hata makao makuu. Sasa kama suala ni uwezekano wa serikali kulipishwa fidia kutokana na uzembe wa watumishi wake na tamaa za hao waliomilikishwa, kuna ugumu gani wa kutunga sheria kuwezesha waziri kuwachukulia hatua na kurudisha maeneo haya kwa matumizi ya umma?

Wewe Ilyas kwani unaishi nchi gani bana? Unadhani kama ingekuwa wewe ndiye mmiliki wa kiwanja hata wangeongea mara mbili? Ungeona tingatinga linakuja linabomoa kisha unaarifiwa ulivamia kiwanja cha wazi. Kwani Loliondo nini kimetokea? Wale wakazi wa Kigamboni waliouzwa kwa wawekezaji?

Lakini ukumbuke kiwanja kilicho na ubalozi wa marekani kilinyanganywa kwa amri ya rais mkapa ndiyo wkapewa ubalozi. mmiliki halali alikwenda mahakamani akashinda kesi na serikali ikaamuriwa kumlipa fidia lakini hadi leo hawajafanya hivyo.

Usijeshangaa Tibaijuka anatafuta pa kutokea. Anatingisha kiberiti ili wale wote wana viwanja isivyo halali wamfuate, unajua tena. Tena ameshasema wale wote wenye viwanja isivyo halali wajisalimishe, we unafikiri nini kitakachotokea. Kwani wizara haina orodha ya viwanja vinavyomilikiwa isivyo halali. Kumbe walijuaje hicho cha Palm Beach kinamilikiwa kihalali. Mpe muda, wamiliki wakishajisalimisha kwake hutamsikia tena!
 
Mama Tibaijuka, ya open space ni luxury kwa wale wakazi wa kigamboni. Maisha ya watu yamekuwa duni sana tangu serikali ilipotangaza kuwauza wakazi wa kigamboni kwa mwekezaji. Kama biashara ya utumwa vile. Sasa muda walioweka umekwisha na hakuna kauli yoyote kutoka serikalini.

Wananchi wanaotaka kuuza maeneo yao wahamie shamba hawawezi kwa sababu wanunuzi wanasita. Walliokuwa wanajenga wamesitisha hivyo hakuna maendeleo yoyote. Biashara zimedoda kwa sababu mzunguko wa fedha ulikuwa unachochewa na uuzaji na ujenzi haupo tena. wizi umezidi kwa sababu vijana hawapati tena vibarua vya ujenzi, wanashinda tu mitaani wanakula bangi usiku wanaiba

Tafadhali tuokoe, wananchi wengi wa kigamboni wanaathirika sana
 
Hamna jipya hapa! huyu mama hana ubavu wa kupambana na waliomuweka madarakani....! hizi ni kelele tu za chura hazimzui tembo kunywa maji...! Anyways days wl tell....
 
Prof. Tibaijuka, nakuonea huruma sana. Ulishasema kama Rais akishaamua jambo hakuna kuliingilia according to KATIBA. Sasa Mama utaweza????????????Mbona maeneo mengi ni ya Waheshimiwa!!!!!!!!!!!!!! Utaweza???????????????????? Au ni nguvu ya soda tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tatizo letu ni kuwa na viwanja vitupu bila kuviendeleza. Manispaa wangeendeleza viwanja hivyo kwa kuweka bustani na sehemu za kuchezea watoto haya yote yasingetokea. Kama Rais aliisha revoke hati hiyo, Muccadam hana lake. Hakuna mmiliki ardhi nyumbani ( Freehold) wote ni wapangaji tu na tunavishika kwa ridhaa ya mheshimiwa Rais.

Amandla......
 
Nobody is above the law ..... ..... khe khe kheeee hivi Ikulu yetu wanalijua hilo?
 
Prof. Tibaijuka, nakuonea huruma sana. Ulishasema kama Rais akishaamua jambo hakuna kuliingilia according to KATIBA. Sasa Mama utaweza????????????Mbona maeneo mengi ni ya Waheshimiwa!!!!!!!!!!!!!! Utaweza???????????????????? Au ni nguvu ya soda tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Maeneo nyeti kushikwa na waheshimiwa ndio sababu inayokufanya udoubt juhudi na harajkati za mama T?

Mpe ushauri unaotia nguvu kuelekea kwenye mafabnikio ya jambo hilo.

Kudoubt mapema kunachangia kukata tamaa hata kiama jambo husika linawezekana.
 
Naona huyu jamaa anajitakia matatizo. Huyu mama alimwandikia ripoti mbaya MUGABE pamoja na watu wengi kutegemea angemfunikia! Unfortunately Muccadam kwa kufanya anavyofanya anawaharibia hao so-called wawekezaji wenzake. Angejikalia kimya tu.

Amandla......
 
Back
Top Bottom